Lengo la kuanzishwa TAKUKURU lilikuwa ni nini?

Lengo la kuanzishwa TAKUKURU lilikuwa ni nini?

Kwasasa TAKUKURU inashughulika na wahasibu wa Halmashauri na wale wasaidizi wa hesabu kwenye vituo vya Afya...nafikiri mbeleni huko itaingia na kwa Wakugenzi na viongozi wengine wa ngazi za juu itakuwa zamu yao kila kitu kwa hatua...haya ndo malengo kwa sasa na yametimia kuhusu vigezo vya kuwapata watumishi wa TAKUKURU Nadhani wachangiaji wengine watakujibu.
 
Tatizo sio mwanzilishi tatizo ni walioanzishiwa..ni kama vile Africans hatuwezi kusimamia sheria na kutimiza majukumu effectively.
Huwa tunawanyooshea mikono polisi na kuwasema but in realty government agencies nyingi ni shida tupu
 
Isije ikawa imeanzishwa ili iwashughulikie chadema mmh! Dunia hii
 
Sasa nashangaa ma CAG kila mwaka wanawatafunia hao takukuru lakn hata kumeza wanashindwa hawatoi ripoti ya kesi hata kwa mwaka mzima yan ni kitengo cha kubaini wala rushwa ili watoe rushwa zaidi kuzima ubadhilifu wao
 
Ukimaliza jiulize na TBS nayo lengo ilikuwa nini? Kukusanya mapato? Au?
 
1. TAKUKURU ilianzishwa kwa malengo gani? Mwenye kujua tafadhali.

2. Je malengo (angalau moja) ya uanzishwaji wake yametimia?

**Vigezo gani hutumika kupima utendaji bora wa watumishi wa TAKUKURU?
TAKUKURU NG'ATA
 
1. TAKUKURU ilianzishwa kwa malengo gani? Mwenye kujua tafadhali.

2. Je malengo (angalau moja) ya uanzishwaji wake yametimia?

**Vigezo gani hutumika kupima utendaji bora wa watumishi wa TAKUKURU?
Hicho kitu ni cha kukifuta kabisa hakina kazi tena,kiliundwa kwa ajili ya kudhibiti Rushwa na ufisadi sasa bahati mbaya kimegeuka chenyewe kuwa ndio rushwa na ufisadi.
 
1. TAKUKURU ilianzishwa kwa malengo gani? Mwenye kujua tafadhali.

2. Je malengo (angalau moja) ya uanzishwaji wake yametimia?

**Vigezo gani hutumika kupima utendaji bora wa watumishi wa TAKUKURU?
Awali ilianzishwa na kuitwa Taasisi ya Kuzuia Rushwa (TAKURU) au 'Prevention of Corruption Bureau' (PCB). Lakini ugumu wa kazi ya Taasisi hii ni katika kuzuia; na hakika lengo hili halijawahi kufanikiwa, hasa kwa rushwa kubwa na ufisadi. Baadaye Taasisi ilibadililishwa kwa sheria namba 11/2007 na kuitwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) au 'Prevention and Combating of Corruption Bureau' (PCCB). Hapa waliongeza kipengere cha kupambana, na hiki ndicho kinaendelea nchini, yaani Taasisi inapambana na walarushwa pia wanapambana na Taasisi. Ipo haja Taasisi hii kuwa na chombo huru cha kuisimamia katika utendaji wao wa kila siku.
 
Back
Top Bottom