SoC02 Lengo la kufanya biashara au kuanzisha biashara

SoC02 Lengo la kufanya biashara au kuanzisha biashara

Stories of Change - 2022 Competition

Ibrahim Quan

Member
Joined
Jul 24, 2020
Posts
6
Reaction score
0
kwanini tunafanya biashara?

Mfanya biashra ambae hufanikiwa ni mfanya biashara ambaye huanzisha biashara akiwa amejiwekea malengo yake binafsi. Malengo aliyojiwekea mfanya biashara ndicho kitu pekee kitakacho mfanya au kitakachoonyesha kuwa mfanya biashara huyo amefanikiwa atafanikiwa. Ni kweli kua kila mtu anaanzisha biashara kulingana na malengo na matakwa yake binafsi alio jiwekea. Kama mpaka leo unataka kuanzisha biashara au umeanzisha biashara unapaswa kukaa chini na kuanza kutafakari na kutambua lengo lako ni nini? Lengo la biashara yako ni lipi? Na utachukua hatua gani ili kufanikisha malengo yako. Baadhi ya malengo au sababu zinazo mfanya mtu aanzishe biashara ni hizi

Kuwa tajiri au kujitengenezea utajiri
. Ni kweli kwamba hakuna mtu katika dunia hii mwenye utajiri mkubwa kama mfanya biashara kama huniamini jaribu kufuatilia na kuwajua matajiri wakubwa duniani wanafanya nini ama wana jishughulisha na nini. Watu ambao huanzisha biashara kwa lengo la kutengeneza utajiri au kuwa tajiri mara nyingi huamini kwamba biashara ndicho kitu pekee kinachoweza kumfanya mtu aweze kuwa tajiri au kujitengenezea utajiri.

Watu wa aina hii mara nyingi huwa waajiriwa au watu ambao maisha yao si ya chini sana nikimaanisha kuwa wana uwezo wa kujitimizia mahitaji yao muhimu yote. Mfanyabiashara yoyote anaweza akawa tajiri au kujitengenezea utajiri endapo atatambua ni kitu gani sahihi kukifanya na kwa wakati sahihi.

Kukuza kipato. Mtu anaweza akaanzisha biashara kwa lengo la kukuza kipato chake mara nyingi watu wa aina hii hufanya biashara ili waweze kukuza kipato chao na kutimiza mahitaji yao muhimu, watu hawa hawana uhitaji sana wa kuwa matajiri au kujitengenezea utajiri japo kuwa wana uwezo na nafasi ya kufanya hivyo. Mtu huyu huamua kuanzisha biashara yake na kukuza kipato chake anacho kipata kwa siku, kwa wiki kwa mwezi au mwaka.

Watu wa aina hii pia huwa na shughuli nyingine ambayo huwa wanazifanya kuacha biashara aliyo ianzisha au anayo taka kuianzisha au anaweza akawa muajiriwa. Ni vizuri kama wewe ni mwajiriwa au mfanya biashara yeyote ambae unajishughulisha na majukumu ya aina zaidi ya moja ni vizuri kwa wewe kutafuta aina ya biashara ambayo utaweza kuiendesha pasipo kuathiri kazi yako ya mwanzo au kazi ulio kuwa ukiifanya au kama una uwezo wa kumpata msimamizi wa biashara yako mtu ambae una muamini unaweza ukaianzisha ila kama huna unaweza ukaanzisha biashara ambayo haitatumia muda wako mwiki na kuharibu au kuathiri kazi uliyokuwa ukiifanya mwanzo.

Msukumo kutoka kwa familia, ndugu, jamaa au marafiki. Moja ya sababu ya vijana wengi na watu wengi kufanya ni kutokana na misukumo. Mtu anaweza kufanya biashara kwa kuwa rafiki yake, ndugu ama jamaa zake wamemhimiza kufanya hivyo au wamemshauri. Maranyingi watu ambao huanzisha biashara kutokana na msukumo huwa wanaambiwa na kushauriwa ni ai a gani ya biashara ni nzuri na itakayo mfaa yeye, pia watu hawa hufanya biashara ambayo watakuwa wameipenda au pia kuifanya kutokana na msukumo. Unaweza ukawa unajiuliza ni kwanini au inakuwaje mtu anaanzisha biashara kutokana na msukumo kutoka kwa watu wengine?

Watu wa aina hii ambao hufanya biashara au huanzisha biashara kutokana na msukumo huwa ni watu wenye pesa, mtaji toshelezi au huwa wanaomba ushauri kuhusu ni aina gani ya biashara ambayo ataweza kuifanya au kuianzisha kulingana na pesa na mtaji alio nao. Au watu hawa hupewa mtaji au hufunguliwa biashara na ndugu, jamaa, familia au marafiki. Kufunguliwa biashara si kitu kibaya. Lakini je! ni kwa jinsi gani itaweza kukusaidia wewe na kukusaidia kukutoa hapo ulipo na kukupeleka pale ambapo walio kufungulia hiyo biashara wanataka ufike? Wewe kama mfanya biashara au mtu ambaye umeamua kujitoa na umeamua kuwa mfanya biashara unapaswa kujiwekea malengo na mikakati amabayo itakusaidia wewe pamoja na watu wanao kutazama na kukuzunguka.

Kusaidia wengine, ni kweli na niwazi kuwa mtu anaweza kufungua au kuanzisha biashara kwa lengo la kusaidia wengine. Mtu huyo anaweza akaanzisha biashara hiyo kwa ajili ya kuisaidia familia yake au jamii yake kwa ujumla. Unaweza ukajiuliza ni kivipi mtu anaweza akaanzisha biashara kwa lengo la kuwasaidia wengine? Acha mimi ni kuambie ni kivipi na ni kwa namna gani? Je hujawahi kusikia mtu ameanzisha biashara kwa ajili ya kusaidia familia yake au kuiendeleza familia yake?

Au kwa namna nyingine ninaweza kukuambia kuwa kutokana na ugumu wa kimaisha ambao unaikumba familia yako mtu anaweza akafikiria ni kwa jinsi gani ataweza kuwasaidia. Mtu huyo anaweza akaanzisha biashara na kuwaajiri watu kutoka kwa familia yake au jamii anayo taka kuisaidia. Mfano unakuta mtu kutoka katika familia fulani au ukoo fulani kafungua duka au biashara fulani na kuwakabidhi watu anao taka kuwasaidia na kunufaika kutokana na biashara hiyo.

Historia historia pia inaweza ikawa ni sababu ya jamii au watu wa jamii fulani kufanya biashara au kupenda kujishughulisha na shughuli za kibiashara. Mara nyingi watu ambao hufanya biashara kutokana na sababu ya historia watu hawa huwa ni moja kati ya asili au wana uhusiano katika historia hiyo. Historia ambayo inaweza ikampelekea mtu kuwa mfanyabiashara ni historia za kifamilia, za ukoo jamii au kabila.

Mfano mtua anaweza akawa na kiu au akawa na lengo la kuendesha na kuanzisha biashara kwa sababu baba yake au mama yake alikuwa mfanya biashara. Katika biashara haijalishi ni sababu gani iliyo kupelekea wewe kufanya biashara ila kitu muhimu ni kutambua malengo yako ni yapi na ni hatua gani unapaswa kuzifuata ili uweze kufanikiwa na kutimiza malengo uliyojiwekea.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom