Lengo la kuwapeleka form 6 leavers jkt

fiter

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
1,144
Reaction score
79
eti ili wawe wazalendo mbona hao wote waliopitia jkt zamani NDIO MAFISADI WAKUU na wasiokua na uzalendo kwa sasa.,....uzalendo haufundishwi mtu anazaliwa nao
....ILA WAPELEKENI TU MWAPE MAFUNZO ILI WAJIAJIRI KWA KUVAMIA BANK NA KUWAPIGA ROBA ZA MBAO....
 

cdhani uzalendo kwa kuwapeleka jeshini uzalendo ni kwenye minds za watu mbona wote walioenda jeshini ndo mafisadi wakubwa
 
mi nadhani ni kuwafunza ukakamavu na kuwajengea mazingira ya kufanya kazi katika sehemu yoyote ile itakapoitajika kufanya, bila kusahau uzalendo ambao unaendelea kupotea siku hadi siku
 
Hivi Feza Boys,St . Marys na nyingine zenye watoto wa kiarabu nao wanaenda Jkt
 
Jkt ni sehemu nzuri sana ya kujifunza maisha unaishi popote unajua usawa unakula chochote na unapata mbinu nyingi kwenye shida mimi nimepitia naona faida zake wataacha kukaa uchi kwenye fb hakuna fb wala ist huko kukomaa kwenda mbele wapelekeni mrudishe maadili ya watoto wa kitanzania
 
Hivi kuchukua sehemu tu ya vijana na kuwapeleka jkt kuna impact gani katika nchi na sehemu hiyo ya vijana ni wale wasomi tu na mamilioni wako mtaani hawana kazi wala ujuzi wowote wa kuweza hata kujiajiri so kwanini option isiwe kwa wale wasiokuwa na elimu ndo waende wakapate hayo mafunzo na baadaye waweze kujiajiri kuliko kuchukua hili tabaka la wasomi ambao baadaye ndo wanakuwa mafisadi wapya halafu pia katika mazingira haya ya ubepari nani yuko tayari kupata shida wakati wengine wanakula raha na pia rais wetu kikwete alipitia jkt na zaidi alikuwa mwanajeshi so huo uzalendo wake uko wapi kwa watanzania tunalazimisha kurudi kwenye siasa za ujamaa kitu ambacho hakiwezekani na pia serekali isipokuwa makini inajitengenezea bomu la kujilipua yenyewe kwa kufundisha hichi kizazi cha nyoka kutumia silaha.na pia hawa vijana walioenda jkt walioko vyuoni ni wahuni wengine wanavaa milegezo hawana mabadiliko yoyote chanya so watz tuache kudanganyana na viongozi wakiwa wazalendo na wananchi nao wataiga sio jkt!!!!
 
Matokeo yake watoto wanabakwa na kufa kama yule wa Tabora
 
Labda uniambie kujenga uwezo wa kujiajiri kwenye kazi zinazohitaji nguvu kama kulima, But uzalendo hauhitaji cheti.
 
nimeenda mwaka jana, jkt ni zaidi unavyofiria,nimejifunza mengi kule. Acha kuwapotosha watu, hata mm nilikuwa na mawazo finyu kama yako pindi nilipochaguliwa kwenda,ckupenda kabsa kwenda wazazi walinilazimisha tu,ila nimekuja kuona umuhimu wake baadaye......
 
Wewe unae fahamu eleza jamii basi nayo ijue kama wewe,laikoini kwa upande wangu hilo ni dili la watu fulan fulani.OVER!

Primary objective ya jkt ni kutengenza askari wa ziada(reserves).

Ukichambua kwa umakini siasa za afrika mashariki hivi karibuni utajua kuwa at any time t Tanzania yaweza kupigwa at multiple fronts.Rwanda,Kenya,Uganda wamesaini mkataba wa kijeshi.Akishambuliwa mmoja wanashambulia wote

Southern front unakutana na Malawi na kelele zake.Jua pia kuwa hizi zote ni flashpoints.Wote hawa wanaisuburi Tanzania at its moment of weakness kui attack

Akianza mmoja watatupiga wote kutoka kaskazini na kusini.Ili ku counter hii threat wana stratejia wa jeshi letu pendwa wakaamua kuanza kutengeneza foot soldiers at a massive scale

Ndo tunakutana na hii kitu ya jkt kwa mujibu wa sheria.Tunahitaji askari wakutosha kupigana front zote hizi kwa mpigo

Analysis hii ni on worst case scenerio.Pamoja mkuu
 

Well said comrade!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…