Lengo la Ndondo ni promotion ya soka au uchawi?

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Kwa muda wa miaka miwili nimekuwa nikifuatilia post za watu wa Clouds kuhusu hicho wanachoita Ndondo Cup.

Moja ya jambo linalotawala sana ni zile picha za waganga ama wao wanaita kamati za ufundi. Hizi zimepewa kipaumbele sana kiasi kwamba, utamaduni huu unaonekana kama ni muhimu sana kwa timu shiriki na kwamba bila mambo hayo basi mpira hauchezwi.

Nguvu na muda vilivyopewa kuzungumzia ushirikina, imenifanya nishindwe kujua lengo la ndondo ni nini. Maana kuna mchawi mmoja anasema wao na timu yake wamewekeza nje ya uwanja asilimia 60 na ndani ya uwanja 40%.

Tuambieni lengo la mashindano hayo ni nini? Kuibua wachawi ama vipaji vya soka?
 
Huu uwekezaji katika ushirikina kuliko kwa wachezaji na soka lenyewe,ni dalili kubwa kwamba bado tuna safari ndefu sana.

Hao waandaaji wa ndondo ukiwakuta wanafanya uchambuzi wa mpira na matukio yake kwa ujumla,huwa wanajidai wako smart sana.Inapofikia suala la ndondo wote wanashabikia ushirikina kama kivutio cha muhimu katika mashindano hayo
 
Kwa muda wa miaka miwili nimekuwa nikifuatilia post za watu wa Clouds kuhusu hicho wanachoita Ndondo Cup.

Moja ya jambo linalotawala sana ni zile picha za waganga ama wao wanaita kamati za ufundi. Hizi zimepewa kipaumbele sana kiasi kwamba, utamaduni huu unaonekana kama ni muhimu sana kwa timu shiriki na kwamba bila mambo hayo basi mpira hauchezwi.

Nguvu na muda vilivyopewa kuzungumzia ushirikina, imenifanya nishindwe kujua lengo la ndondo ni nini. Maana kuna mchawi mmoja anasema wao na timu yake wamewekeza nje ya uwanja asilimia 60 na ndani ya uwanja 40%.

Tuambieni lengo la mashindano hayo ni nini? Kuibua wachawi ama vipaji vya soka?
Kutafuta/ kuibua wachawi watakao tumika ligi kuu na mechi za kimataifa.
 
Back
Top Bottom