kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,634
- 7,015
Kwa muda wa miaka miwili nimekuwa nikifuatilia post za watu wa Clouds kuhusu hicho wanachoita Ndondo Cup.
Moja ya jambo linalotawala sana ni zile picha za waganga ama wao wanaita kamati za ufundi. Hizi zimepewa kipaumbele sana kiasi kwamba, utamaduni huu unaonekana kama ni muhimu sana kwa timu shiriki na kwamba bila mambo hayo basi mpira hauchezwi.
Nguvu na muda vilivyopewa kuzungumzia ushirikina, imenifanya nishindwe kujua lengo la ndondo ni nini. Maana kuna mchawi mmoja anasema wao na timu yake wamewekeza nje ya uwanja asilimia 60 na ndani ya uwanja 40%.
Tuambieni lengo la mashindano hayo ni nini? Kuibua wachawi ama vipaji vya soka?