Lengo la Rais Magufuli kuzuia makinikia ni ili Smelter inunuliwe hapa nchini. Prof. Muhongo alifukuzwa uwaziri kwa kushindwa kununua Smelter

Lengo la Rais Magufuli kuzuia makinikia ni ili Smelter inunuliwe hapa nchini. Prof. Muhongo alifukuzwa uwaziri kwa kushindwa kununua Smelter

"Magufuli ni mwizi kuliko marais wastaafu wote.

Anachokifanya kwa mawaziri, makatibu na wakuu wa mikoa kawaambia kabisa nyie pigeni lakini mnijulishe na mnipe mgao wangu

Ana kakikundi fulani ivi kazi yake kula nchi."
Haya tumekusikia!
 
Kwahiyo Mark kwa kusema vile umemwamini kweli kabisa? Yani mtu aaminiwe kuongoza Barrick Afrika kisha aje kuangalia maslahi ya watanzania? Kiukweli wana CCM wengi sana huwa tunafeli hapa! Kuamini kuwa kiongozi wa serikali au mtu akiongelea upande wetu kwa uchungu na kujipiga piga kifua basi huyo na baba wa kweli. Tujifunze kutoka nje ya miili yetu ya asili ili tujue mengi zaidi.

Yani kweli kwa ulichoandika nimekudharau kabisa! Kwamba kwakuwa jamaa alijiita mwafrika basi kwako amemaliza kila kitu? Shame!
Kama uliisoma body language ya kabudi ni kuwa korongo alishammeza chura, chura nae akashika koromeo, alisema barrick walishatafuta wachina watuuzilie mbali bahati nzuri/mbaya hawakufika bei, ni mungu saidia prof Thornton kapatwa maradhi ka step down ndio Mark kupata fursa na kuamua kututoa mdomoni mwa korongo, sasa tuache kumwamini kwa lipi? sisi tumempa ulaji nayeye katutolea mwiba.

Katika Corporate management its all about trust, Jack Mar alisema, alibaba its all about trust, why not Twiga to be all about trust? Mtu kavunja ofisi London kaileta Mwanza mji uliomtoa kimaisha.
 
Leo miaka miwili imepita, umesaini makubaliano ya hovyo hovyo kuwahi kutokea, ACACIA wamepata mgao wao bila kwenda mahakamani. Barrick anapeleka makinikia nje kuyachenjua kiulaini kabisa na mambo yanaendelea vyema huku Barrick akipiga bao la nguvu.

Sisi tunakuuliza kuwa, lengo lako hasa lilikuwa ni lipi? Au ulikuwa tu hulipendi jina ACACIA? Lilikukosea nini?
Ninakubaliana na sehemu kubwa ya mada yako huko juu.

Ila haya uliyoweka kwenye mistari hii minne yanavuruga kwa kiasi kikubwa mada nzima. Tunajua uongo mwingi uliowekwa kwenye ripoti ya Mruma, na hakika ilikuwa ni "Professorial garbage," iliyokuwa na lengo la kuwatishia tu ACCACIA, huku ikituzubaisha sisi walala hoi wa Bongolala; hasa tulipokuwa tukiambiwa yale malori ya tani saba saba yamajazwa dhahabu tupu!

Lakini,wewe hapa una maana kwamba hakuna lolote lilobadilika katika mikataba ile iliyokuwepo inatumiwa na ACCACIA? Mbona hilo liko wazi, na sheria mpya zimetungwa,...au una maana gani!
 
Wakati wa ripoti Prof.Osoro/Mruma raisi alikuwa kama anatoa tangazo kuingia vitani kijeshi. Mikataba juzi hatima kamanda Kiongozi Kabudi, karudi mkia nyuma, mwenye hofu ,uoga kwamba anashukuru hisani ya Wadau Barrick.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Magufuli ni mwizi kuliko marais wastaafu wote.

Anachokifanya kwa mawaziri, makatibu na wakuu wa mikoa kawaambia kabisa nyie pigeni lakini mnijulishe na mnipe mgao wangu

Ana kakikundi fulani ivi kazi yake kula

aiseee...
 
Sasa hivi hakuna anayeongelea issue ya smelting plant. Hawa watu wakiondoka ndiyo tutajua tumepata hasara kiasi gani. Kwa sasa wacha waendelee kusema wao ndiyo wazalendo
 
Teh teh teh...

"Upumbavu ni kipaji kuna watu wanazaliwa nacho".Mwalimu Nyerere...

Unamuamini "Mzaliwa wa AFRIKA KUSINI" , mwenye asilia ya UYAHUDI".?

Unaijua dunia ya siri inavyoendeshwa kwa maslahi ya wazungu wewe.???

Kama una mtoto ,mtizame kisha mwambie "NAOMBA USIRITHI UJINGA WANGU"...
Mkuu kaisikilize kwa umakini speech ya Mark Bristol, Mzaliwa wa africa ya kusini mwenye asili ya uyahudi, kasema yeye ni mwafrica halisi tena mzulu, alimaanisha kuwa africa tunapaswa kuwa wamoja yanapokuja maslahi ya africa. isingelikuwa kukomaa kwa magufuli Mark asingekuwa ceo wa barrick, na Mark asingekomaa na Geleta tusingepata huyu mtoto twiga minerals, na huu ndio ushirikiano wa kikanda akasema, either we win together or we loose together na hii ndio africa mpya chini ya magufuli. Umeelewa?

Msafwa,
Uporoto, Mbeya..
 
Hawa jamaa wa CCM wakishaona Magufuli kakubali kitu basi ni Mungu kapitisha. Yani myahudi akusainie documents halafu akupongeze na wewe ucheke? Muda utaongea tena kama jinsi ambavyo umeongea!
Tena wayahudi hawahawa ambao hata wazungu wenzao wana waogopa kibiashara kwa jinsi walivyo wajanja?
Tunatia huruma sana sisi kwa kukubali kumsikiliza mtu mmoja na ambaye uwezo wa kuchambua mambo kama kiongozi hanao kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi sasa kuna matukio ya uhujumu uchumi na rushwa za kutisha zinafanywa wazi wazi na kwa kificho kuliko utawala mwingine wowote!!
 
Ninakubaliana na sehemu kubwa ya mada yako huko juu.

Ila haya uliyoweka kwenye mistari hii minne yanavuruga kwa kiasi kikubwa mada nzima. Tunajua uongo mwingi uliowekwa kwenye ripoti ya Mruma, na hakika ilikuwa ni "Professorial garbage," iliyokuwa na lengo la kuwatishia tu ACCACIA, huku ikituzubaisha sisi walala hoi wa Bongolala; hasa tulipokuwa tukiambiwa yale malori ya tani saba saba yamajazwa dhahabu tupu!

Lakini,wewe hapa una maana kwamba hakuna lolote lilobadilika katika mikataba ile iliyokuwepo inatumiwa na ACCACIA? Mbona hilo liko wazi, na sheria mpya zimetungwa,...au una maana gani!
Mkuu hope muda utafika ukishaona kila kilichopitishwa tutakuwa upande mmoja.
 
Kama uliisoma body language ya kabudi ni kuwa korongo alishammeza chura, chura nae akashika koromeo, alisema barrick walishatafuta wachina watuuzilie mbali bahati nzuri/mbaya hawakufika bei, ni mungu saidia prof Thornton kapatwa maradhi ka step down ndio Mark kupata fursa na kuamua kututoa mdomoni mwa korongo, sasa tuache kumwamini kwa lipi? sisi tumempa ulaji nayeye katutolea mwiba.

Katika Corporate management its all about trust, Jack Mar alisema, alibaba its all about trust, why not Twiga to be all about trust? Mtu kavunja ofisi London kaileta Mwanza mji uliomtoa kimaisha.
Yani Kabudi ni muongo muongo anayedhani watu hatuna akili kabisa.
 
Dawa ya mjinga ni kumchanganyia changanyia mambo hadi unamsahaulisha asijue mlikuwa mnafanya nini na kwanini..
 
"Mimi ni muafrika mwenzako" waliposema hivyo beki zote zikalegea.

Barrick "kauza" kwa randgold kisha randgold baadae "atauza" kwa barrick. Mtu yule yule ila kabadili nguo.
 
"Mimi ni muafrika mwenzako" waliposema hivyo beki zote zikalegea.

Barrick "kauza" kwa randgold kisha randgold baadae "atauza" kwa barrick. Mtu yule yule ila kabadili nguo.
Na wana CCM wamechukua ile quote wanaitembeza kwenye mitandao ila wamejisahau wakaweka na picha ya huyo mwafrika mwenzao!
 
Na wana CCM wamechukua ile quote wanaitembeza kwenye mitandao ila wamejisahau wakaweka na picha ya huyo mwafrika mwenzao!
Ukiona mzungu anapambana ujue chini bado kuna mzigo mwingi sana wa dhahabu na makinikia ya madini ya kutengenezea simu na computer.
 
Kukuru kakara zoote za kukimbilia bungeni kutunga sheria mpya ya madini halafu baadae mnakuja kuingia mkataba ns kampuni moja ya madini ambayo wala haitaguswa na masharti ya sheria hiyo, sasa kama siyo jambo la ajabu hili ni kitu gani?

Walituambia kuwa kwenye makinikia kuna copper, zink, cobalt, sulphur na madini mengineyo ambayo ACACIA walikuwa hawadiklei, sasa leo tumeingia mkataba ambao hauna kipengele chochote cha kuelezea hayo madini mengine tutanufaika nayo vipi.

Lakini kubwa kuliko yote, ni kutokutueleza zile Trilion zetu 425 tutazipatajepataje!. Ina maana ripoti ya Mruma na Osoro ilitudanganya au serikali hii ya CCM imeamua kuwa serikali ya kuhujumu uchumi. Itasemehe vipi mihela yote ile?
 
Back
Top Bottom