Lengo la Serikali ya CCM ni kuona Mbowe akisalimu amri na kuomba msamaha kwa Kesi ya ugaidi inayomkabili?

Lengo la Serikali ya CCM ni kuona Mbowe akisalimu amri na kuomba msamaha kwa Kesi ya ugaidi inayomkabili?

Mbona hamsubiri kazi ya wakili msomi @kibatala?

Mbona hamtaki Demokrasia wakati nyinyi ni wana demokrasia?

Si msubiri mwisho wa kesi na muone nini kitatendeka!

Au mna wasiwasi kwa sababu kuna ukweli mnaoujua!
 
K
Kama shujaa Mandela alihukumiwa kifungo cha Maisha jela, kwa makosa ya kubambika ya uhaini.

Hatimaye akatoka jela baada ya kutumikia miaka 27 na akawa mwafrika wa kwanza mweusi kuwa Rais wa Afrika Kusini.

Kwa hiyo kuna ajabu gani kwa Mbowe kuendelea kusota rumande kwa makosa ya michongo, hadi pale atakapohakikisha kuwa Haki imetendeka?
Kesi ya Mandela haikuwa ya kubambika! Ilikuwa ya kweli ya uhaini, alitaka kuangusha utawala wa Afrika kusini wa wakati ule kwa kutumia nguvu. Alikuwa anawaongoza wapiganaji wa Umkhontho weSizwe. Ila ugaidi wa Mbowe siyo ule kama wa Mandela. Ukilinganisha ni kama Armed robber na kibaka (mwizi wa kuku)!
 
Tulishuhudia hapo majuzi, Jaji Tigana akifanya uamuzi ambao umekuwa kinyume cha matarajio ya mamilioni ya watanzania, kuhusu Kesi ndogo inayohusu Kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema na wenzake 2 ya kutaka kuchoma moto vituo vya mafuta na kutaka kupanga njama za kutaka kuwadhuru baadhi ya viongozi waandamizi wa Serikali hii ya awamu ya 6.

Kwa kuwa Kesi hiyo inafuatiliwa kwa karibu Sana na watanzania walio wengi na Jumuiya za kimataifa, watu wengi walidhani kuwa maamuzi ya Jaji Tigana, yatakuwa ya haki na kuyatupilia mbali madai ya mashitaka ya Jamhuri na kuachiliwa watuhumiwa wote.

Hata hivyo watanzania hao walishikwa na mshtuko baada ya kusikia maamuzi hayo ya Jaji Tigana!

Kwa waliofuatilia Kesi hiyo kwa muda wote wa miezi kadhaa tokea ianze, walishuhudia mashahidi wa Jamhuri namna walivyokuwa "wakihenyeshwa" kwa maswali magumu na jopo la mawakili wa utetezi, wakiongozwa na wakili msomi Kibatala, hadi baadhi yao kushindwa kuhimili vishindo hivyo na kupata homa za ghafla, hadi wengine kulazimika kukimbizwa hospitali kupata matibabu!

Lakini pamoja na mtiririko huo wa mwenendo wa Kesi, Jaji Tigana akaamua "kuziba masikio" na kuamua kuwa kina Mbowe Wana Kesi ya kujibu Katika Kesi hiyo ya ugaidi na hivyo wanatakiwa kuanzia tarehe 4 mwezi ujao waanze kijitetea wenyewe.

Ndipo hapo ninajiuliza hivi Mahakama kusema kuwa ni lazima Katika Kesi za jinai, kuwepo ushahidi usiokuwa na shaka yoyote Ili kumtia hatiani mtuhumiwa, hivi Katika ushahidi uliotolewa na mashahidi wa Jamhuri, ni kweli kuwa walitoa ushahidi usio na mashaka yoyote?

Hivi unadhani ni nini kilichokuwa kikisababisha baadhi ya mashahidi, kushikwa na homa za ghafla hadi kulazimika kukimbizwa hospitalini??

Hiyo haitokani na hao mashahidi, kuunga unga ushahidi wao na hivyo kufanya kuwa penye ukweli, uongo hujitenga??

Ndipo hapo ninadhani kuwa watawala wetu ingawa nafsi zao zinawasuta Sana kutokana na mateso ambayo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake 2 wanayapata kwa kusota rumande kwa zaidi ya siku 250, lakini wanachotaka wao ni kuwa Mbowe asalimu amri na kuomba msamaha Ili atoke jela.

Kwa hilo watawala wetu watasubiri Sana, kwani mategemeo yao ya kuwa Mbowe ataomba msamaha na hivyo kuhalalisha wao watawala watembeze propaganda yao kuwa chama cha Chadema ni cha kigaidi na hivyo kamwe Mbowe hataomba msamaha kama watawala wetu wanavyofikiria na atahakikisha kuwa anaendelea kukaa rumande hadi hatimaye haki itendeke Katika Kesi hiyo na kumwachia huru.

NO RETREAT NO SURRENDER
Without Fear or Hate,Mbowe isn't a Terrorist-Masuala ya utalii?
 
Mbona hamsubiri kazi ya wakili msomi @kibatala?

Mbona hamtaki Demokrasia wakati nyinyi ni wana demokrasia?

Si msubiri mwisho wa kesi na muone nini kitatendeka!

Au mna wasiwasi kwa sababu kuna ukweli mnaoujua!
Hakuna wasiwasi,kinachotusikitisha ni jinsi mahakama,Jaji na waendesha mashtaka wa serikali wanavyolazimisha kuwe na kesi wapige mpunga wa Wadanganyika-kodi vs posho ilhali ushahidi walioleta ni wa kuunga unga.Hata hivyo natambua kuwa unaufahamu ukweli ila unajibaraguza tu.
There were No Case to Answer.
 
Back
Top Bottom