Leo CCM watalala usingizi mnono sana kwani wanayemmudu amechukua fomu ya kugombea.

Leo CCM watalala usingizi mnono sana kwani wanayemmudu amechukua fomu ya kugombea.

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
357
Reaction score
686
CCM hakuna mtu anawanyima usingizi kama Lissu. Hata siku ile Lissu anachukua fomu CCM walipata taabu sana. Wanamjua Lissu kuwa si mwepesi wa kukubali ujinga kwa lugha yoyote ile. Wakati ule maridhiano yakiendelea, Lissu aling'amua mapema kuwa kinachoendelea kwenye maridhiano ni danganya toto tu, kitu ambacho Mbowe hakung'amua mapema. Kwa eneo hilo, Lissu aligundua njama mapema zaidi kuliko Mbowe ingawa alipigwa vita.

CCM wanamtaka Mbowe zaidi kwa sababu wanammudu kikamilifu.
Mbowe anaweza kufanya maridhiano na CCM hata miaka 3 mfululizo, kitu ambacho Lissu hawezi kukubali ujinga huo hata kidogo.

Kwa maoni yangu, CCM watampa Mbowe full support ili aweze kushinda uchaguzi huo mwakani.
 
Mbona ipo wazi. CCM hawawezi kumruhusu Lisu awe Mwenyekiti kwa sababu atawasumbua na kama unavyojua CCM hawapendi kuonekana wabaya Jumuiya ya Kimataifa, hivyo hawamtaki kabisa Lisu ili asije kuleta hata maandamano ya man show kama Kiiza Besigye wa Uganda.

Ukishakuwa Mwenyekiti wa upinzani mfano CHADEMA unamolikwa ndani na nje, hivyo ni ngumu kutekwa hivyo Lisu akiwa mwenyekiti atasumbua sana.
 
CCM hakuna mtu anawanyima usingizi kama Lissu. Hata siku ile Lissu anachukua fomu CCM walipata taabu sana. Wanamjua Lissu kuwa si mwepesi wa kukubali ujinga kwa lugha yoyote ile. Wakati ule maridhiano yakiendelea, Lissu aling'amua mapema kuwa kinachoendelea kwenye maridhiano ni danganya toto tu, kitu ambacho Mbowe hakung'amua mapema. Kwa eneo hilo, Lissu aligundua njama mapema zaidi kuliko Mbowe ingawa alipigwa vita.

CCM wanamtaka Mbowe zaidi kwa sababu wanammudu kikamilifu.
Mbowe anaweza kufanya maridhiano na CCM hata miaka 3 mfululizo, kitu ambacho Lissu hawezi kukubali ujinga huo hata kidogo.

Kwa maoni yangu, CCM watampa Mbowe full support ili aweze kushinda uchaguzi huo mwakani.

Wanavyo msifia mpaka kero
 
Sasa hivi wasimlambishe tena asali ya kidole wala ya kwenye Kibuyu,wampelekee Mzinga kabisa ili aukumbatie kabisa huku sisi na Lissu wetu tukitafuta kufungua chama kupya KITAKACHO AMINIKA katika Macho ya Watanzania.
 
Ukiondoa kummudu,Kwa sasa CHADEMA hawana mtu wa kushika ile nafasi.
Japo MBOWE NA LIPUMBA’vu tumewachoka katika tasnia ya siasa
 
Nimeondoka Lumumba Lori linashusha creti nyingine za lager 😂😂

Niliowaacha wanakesha mi na Mzee Mgaya tutawahi Supu asubuhi maana wamechinjwa mbuzi wa kutosha
 
Back
Top Bottom