Habar zenu wakuu.
Leo nmeshangaa sana, mida ya sa11 jioni nilipokea simu kutoka kwa mwanamke nisiemjua, alijieleza vizuri nikamkumbuka vizuri kua ni alienisajilia lain week moja nyuma.
Tuliongea sana, akaniahidi ipo siku atakuja kwangu kunitembelea, nakumbuka siku ile nilisajili laini na akaniwekea vocha ya 1,000 kwahyo akawa ananidai 2,000
Nikampa 10,000 ili anirudishie 8,000 yangu. Lakini akadai chenchi hana kwakua biashara siku hiyo haikua nzuri, basi nikamwambia asijali hiyo 8,000 anaweza tuu akabaki nayo bila tatizo kwakua namimi nilikua busy nawahi job sikua na mda wa kusubiri akatafute chenchi.
Nqmba yangu anasema aliisave baada ya kunisajilia laini
Hivi na nyie huwaga mnapigiwa simu msalimiwe na wanaowasajilia laini zenu?