Tayari makampuni ya uwekezaji yalijiandaa kuwekeza dola bilioni 30 kwenye mradi wa ujenzi wa LNG. Huu ungekuwa mradi mkubwa wa uwekezaji ambao haujawahi kuwepo katika kanda ya Afrika.
Alipoingia Kivuruge, kama kawaida, miradi yote iliyosainiwa na watangulizi wake, akasimamisha kwa madai kuna ufisadi. Kama alivyofanya kwenye SGR. Wenzake walisaini ungejengwa kwa dola dola bilioni 11, yeye mpaka Singida tayari ni bilioni 9. Kufika Mwanza utajengwa kwa dola bilioni ngapi? Na bado anawadanganya wajinga kuwa anapiga vita ufisadi. Wachina aliowakataa, sasa anawapigia magoti.
Wawekezaji wa gas waliamua kuondoka na kwenda kuwekeza Mozambique. Huko wanajenga LNG, ni uwekezaji wa dola bilioni 28, na ni uwekezaji wa pili kwa ukubwa Duniani kwenye sekta ya gas kwa mwaka 2020/2021.
Wameombwa sana kurudi lakini wamekataa. Muda wa karibu kabisa kuweza kufikiria kuwekeza tena Tanzania, wanasema ni baada ya miaka 5.
Kwa hiyo uchumi wa gas umeyeyuka. Nchi tajiri kabisa Duniani kwa kuzingatia wastani wa mapato ni Qatar. Kinachosababisha wawe matajiri hivyo, ni gas. Sheria yetu ya gas kabla ya 2016, ilikuwa ni copy and paste ya Qatar na Norway. Lakini jamaa akasema ni ya kifisadi. Kama Qatar na Norway, sheria hiyo hiyo imewatajirisha, inakuwaje ya kifisadi kwetu?
Kutafuta umaarufu kwa kisiasa kwa mtu mmoja kumeliletea hasara isiyoelezeka Taifa.
Kiongozi atakayefuata atakuwa na kazi kubwa ya kurekebisha mambo mengi ili kuirudisha nchi kwenye uchumi wa kisasa na kistaarabu.
Sent using
Jamii Forums mobile app