Leo hii ni Januari 2021, hivi gesi ya Mtwara imefikia wapi?

Gas awamu ya kikwete ilifanya usanii wa kutisha nyie acheni tu! hawakutosheka na Escraw
 
Na hio pia dakika za mwisho tutaambiwa imeshatekwa na mabeberu
Mataga ni balaa kama korona
 
Wapinzani hasa CHADEMA walikua wanakwamisha mchakato mzima wa gesi ndio maana tumewaengua ili kukamilisha mchakato huo
 
Wewe tulia umesikia kama cabodelgado kumechafuka sasa hio gesi tusiifanyie haraka wacha mambo yakitulia tutaanza kuipulizia tena kwenye mapaipu,mazuri hayataki kishindo.
 
Hii gesi inapigwa vita sana na makaka wa dunia ndio maana unaona wanamgambo wenye mapanga na marungu wameweza kuteka mradi mzima wa LNG kule msumbiji na hakuna wa kuwatoa
 
Ikiwa kweli unataka kujua kinachoendelea kuhusu gesi ya Mtwara nakushauri ukasome bajeti ya wizara ya nishati ya mwaka huu wa fedha. Kuna shughuli zitafanyika mwaka huu na zimetengewa mabilioni ya pesa.

Bali ikiwa lengo lako ni kupiga siasa tu hapa ninakushauri uendelee kusubiria updates kutoka kwa wanaharakati wa hapa na pale mitandaoni.
 
Mbona mkataba wa madini kama Barick walifurukuta furukuta kuwakabili mabeberu? Jpm mbona kwenye gesi ana act kinyonge hivi?
Mkuu, haja-act kinyonge. Ni ile tu hataki kupiga makelele. Kuna vitu vinaendelea underground. Fanya ukasome bajeti ya wizara ya nishati ya mwaka huu neno kwa neno utaelewa namaanisha nini.
 
Kwa saiv tuiache kwanz iwe pending... Lakin kama ingekuwepo hapa kwetu chato tungefanya jambo
 
Na hakuna chombo chochote cha habari kinachotupa updates au kumbukumbu ya gesi ya Mtwara.
mkuu kwa sasa uzalishaji wa gas unaendelea vizuri kwa PROCESSING PLANT ILIYOPO MADIMBA, na ile iliyopo kisiwa cha songosongo mkoani LINDI. Hiyo gas inasafirishwa hadi pale KINYEREZI ambapo inagawanywa kwenda kwenye plants za kuzalisha umeme za TANESCO (UBUNGO, KINYEREZI n.k) pia gas hiyo imepelekwa katika viwanda binafsi kama dangote cement, goodwil ceramics, rodhia steel n.k na mwisho kwa sasa raia wa kawaida wanaendelea kuunganishiwa katika mikoa ya dsm, mtwara na lindi kwa matumizi ya kupikia.
unaweza kupitia sites za TPDC >>>> www.tpdc.co.tz na instagram check @tpdctz

NB. mimi ni raia tuu niliyeona ni vyema niseme ninachojua kwa uchache.
 
Upload doc yake kama una-acces nayo mkuu.
 
Unaleta majungu mzee siyo,hivi kila kiongozi anashughulikia gesi ya mtwara?

Acha uchochezi katembee kwa miguu kutoka lilipoanzia lifute utajua limeishia wapi
 
Kwani wewe unadhani hiyo gesi iliyopo Kinyerezi, DSM, ikituzalishia zaidi ya MW 1,000 za umeme inatoka wapi kama si Mtwara?

Mpango mwingine uliopo ni wa kuiuza nje (export) kiasi fulani ya hiyo gesi ya Mtwara ughaibuni ikiwa kwenye LNG form kama wanavyofanya Russia.
 
Mkuu, haja-act kinyonge. Ni ile tu hataki kupiga makelele. Kuna vitu vinaendelea underground. Fanya ukasome bajeti ya wizara ya nishati ya mwaka huu neno kwa neno utaelewa namaanisha nini.
Mkuu, kama hutojali, tuwekee humu. Ukiondoa matatizo yaliyojitokeza, ule mradi uliukuza sana mji wa Mtwara, na kiukweli pamoja na korosho, Mtwara ilitisha na kama ile move ingechukua miaka kama 10 hivi, Mtwara ilikua ni tishio. Tuombe ile miradi irudi tena ili kukuza uchumi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…