Leo hujaenda kanisani? Kwa nini?

Socw

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2016
Posts
1,329
Reaction score
2,644
Jamani kama mnavyojua kuwa Leo ni siku ya kwenda kuabudu kwa wakristo wa madhehebu yaliyo mengi. Lakini najua tupo ambao hatujaenda. Kama hujaenfa, kwa nini hujaenda church Leo?
Mimi niwe mkweli ni kuwa sijaenda kanisani Nina kama miezi mitatu hivi na sina sababu ya msingi sana, labda Ni baada ya kuona viongozi wa dini wamekuwa waswahili sana.
 
Mi nimechelewa kuamka ndio maana sijaenda,alafu napenda ile ibada ya saa moja
 
Huu uzi umenigusa moja kwa moja.

Mara ya mwisho kwenda kanisani ilikua jumapili baada ya kupata Kipaimara, kisha nikaenda mara moja nikiwa form six. Halafu sijaenda mpaka sasa hivi ninapoukuta huu uzi.

Anyway katika mafunzo yangu ya kipaimara niliambiwa kanisa ni mimi siyo jengo, hivyo naweza kusali popote
 
Ekaristi Takatifu unapokelea wapi kama kanisa ni wewe ?
 
Ekaristi Takatifu unapokelea wapi kama kanisa ni wewe ?
Yesu aliwapa watu mkate wapi?

Mgonjwa ambaye hawezi kunyanyuka hua anapelekwa kanisani au anafuatwa hospitali?
Hospitali ni kanisa?

Jengo la Mama Rwakatare tukitoa ile misalaba na kuweka vitanda vya wagonjwa utaita kanisa?
 
Juzi walitutukana tunaotoa jero kisa haijaandikwa fedha halali...na mm nimewawekea vikwazo hawayoniona kanisani kwao ntasali na kuabudu getoni mwangu.
 
Yesu aliwapa watu mkate wapi?

Mgonjwa ambaye hawezi kunyanyuka hua anapelekwa kanisani au anafuatwa hospitali?
Hospitali ni kanisa?

Jengo la Mama Rwakatare tukitoa ile misalaba na kuweka vitanda vya wagonjwa utaita kanisa?
Ok

Na wewe ni mgonjwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…