geofreyngaga
JF-Expert Member
- Sep 7, 2014
- 658
- 946
Vitu tunavyomiliki au umasikini tulionao leo ni matokeo ya jinsi tulivyo fikiri na kutenda jana. Leo ni siku ya kupata matokeo halisi ya jinsi gani kila mmoja wetu kwa wakati wake alivyoweza kufanyakazi ili kutimiza kile alichokua anakiwaza jana kiwe, pia leo ni siku ambayo kesho haina maana sana kama leo haitendwi inavyopasa itendwe.
Matokeo mazuri leo ni zao la mawazo mazuri yalivyotendewa haki jana. Bahati nzuri karibu wote tunamawazo mazuri tatizo ni kuyabadilisha mawazo yetu yawe katika uhalisia, hapa ndipo shughuli ilipo. Kimsingi tumekosa uthubutu na ujasili wa kubadilisha mawazo yetu mazuri kuwa katika vitendo kisingizio kikubwa "SINA MTAJI" na hofu ya kuogopa kushindwa. Eti watu wataandamana huku wamebeba mabango wakipita barabara ya Jangwani wakifurahia Ngaga bakery imekufa!!!!!! hakuna hii kitu labda unaishi na watu vibaya tena sana.
Siku moja baada ya maongezi mengi na ndugu yangu yaliyoonyesha kutokukubaliana na wazo langu aliniuliza unadhani utachukua muda gani mpaka kijiwanda chako kianze kazi?
Nilimjibu hivi:
''Sitajali itachukua muda gani ila kama Watanzania tunajenga nyumba inaisha baada ya miaka 10+ basi na mimi ntafanya hivyo hivyo lakini LAZIMA nikamilishe nachokifikiria'' Nashukuru nimekamilisha ndani ya miaka 5.
Moja ya njia zinazoweza kukujengea uthubutu baada ya kupata wazo(idea), jipe muda wa kutosha ulipitie wazo mara kwa mara, lirudie mara kwa mara, soma maandiko yakutosha yanayohusiana na hilo wazo, ongea na watu wenye uelewa na hilo wazo, waogope kama ukoma wote ambao unajua/unahisi watakukatisha tamaa na fanya kila uwezalo kupata taarifa zaidi zitakazo kusaidia kukuimarisha.
Ukishakua na wazo ulilolitafiti vya kutosha na uthubutu, mtaji si tatizo sana kwani utajua vichochoro vya kupita kufanikisha lengo japo bado juhudi kubwa inahitajika. Msisitizo: Wengi tunasingizia hatuna mitaji, tukiulizwa tunahitaji mtaji kiasi gani bado jibu tunakosa kwasababu hatuna wazo au tunalo ila hatujalifanyia uchunguzi wa kutosha hivyo hatujui kiasi gani cha pesa kinahitajika tofauti na mtu mwenye wazo lililotimia anajua nn afanye na wapi apite.
Basi kama leo imejengwa na Jana na leo yenyewe iko iko tu kimtindo, basi leo tufikiri vizuri na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa pamoja na ubunifu bila kuchoka na kukata tamaa ili kesho ikae sawa.
Leo imejengwa na jana karibuni.:welcome: