Leo Karia una mtihani lakini Mambo mengine unajitakia

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Kwa bahati nzuri Mungu alinijalia kuipenda soka bila mahaba ya timu za Kariakoo. Utashangaa nimewezaje lakini kwangu halikuwa Jambo kubwa kuamua zaidi ya kuupenda mpira wa miguu na kuufuatlia katika Nyanja nyingine ya Uamzi.

Leo ni Tamasha kubwa la timu ya Simba (S. S. C DAY) linaloazimishwa August 8 Kila mwaka Tangu mwaka 2009. Ni Tamasha kubwa linalovuta hisia si Kwa wapenzi na mashabiki wa Simba pekee bali wa vilabu vyote ndani na nje ya Tanzania Kwa jinsi linavyovuta hisia za Soka.

Tarehe 6/08/2022 siku mbili tu zilizopita Yanga walikuwa na Tamasha kubwa kama hili pale pale Uwanja wa Mkapa Temeke Dar es salaam. Mgeni rasmi katika tukio Lao alikuwa Kinana Makamu mwenyekiti wa CCM Taifa. Mbali ya ukubwa wa Tamasha lile na umuhimu wa timu hiyo kama ilivyo Kwa Simba kuhusu soka la nchi hii, Viongozi wote wa juu wa TFF hususan Karia Kwa upekee kabisa hawakufika, hawakuhudhuria.

Leo Simba Wana tukio kubwa na naambiwa mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Patrice Motsepe, Rais wa CAF ambaye yuko njiani kuelekea Arusha kuhudhiria Mkutano wa Mwaka wa CAF unaoanza Jumatano 10/08/2022.

Kuwepo Kwa Motsepe kwenye Tamasha Hilo kunamlazimisha Kwa njia moja au nyingine Karia naye kuwa karibu na bosi wake. Hii itajenga picha gani hasa Kwa mashabiki watafuta sababu? Karia ni Simba ndo maana hakuhudhuria Tamasha la Yanga.

Ukiwa kiongozi huwezi kukosa upande, lakini mara nyingi Karia umekuwa ukichanga vibaya karata zako na naamini ipo siku utalamba Galasa.
 
Una Uhakika Kweli kuwa Nao huu ni Mtihani Kwa Karia?

Mashabiki Wa Mpira Tz huwa tunajichosha mno pale tunapojifanya eti na sisi ni Wachambuzi.. Kumbe ni chawa Wa Aidha Yanga au Simba.

Dogo Kaa Ufurahie tamasha haya Mengine achana nayo.
Mwache Msukule aendelee kujipiga Matukio!
 
Huo uSimba na uYanga mwenzio sina na sikubahatika. Ukiangalia Kwa jicho jepesi utaona ni Jambo dogo lakini kama kweli Karia atakwenda uwanjani Leo, nawajua Watanzania Kwa kelele, labda asije Aug.13.
Naomba mgeni rasmi awe mwingine ili hili Jambo lisitokee.
 
Karia kuhudhuria Simba day ndio mtihani?
Kwani hajawahi kuhudhuria Yanga day?
 
Hawakumwalika
Hilo ni Jambo lisilowezekana Mkuu Dabil. Wewe ni shabiki mkubwa unayeheshimika kisoka JF unadhani Yanga wanaweza kufanya kosa Hilo? Yaani Nyamuhokya aalikwe Karia asahaulike na timu yake yote?
 
Yanga kipindi kile malinzi anawabeba mnachukua ubingwa back to back ulisikia simba wanalalamika yaani yanga kila kitu mnalalamika kipindi mnaenda taifa kuwapokea wageni wanaokuja kucheza na simba ulimsikia nani analalamika ndo maana Morrison anasema hamjasoma.
 

Kwa .uonekano tu Karia ni mshamba na hajitambui hiyo nafasi ya rais wa tff aliipataje mara 2 mfululizo?

Ninamiss uongozi makini wa Leonard Tenga.
Karia ni mharo tu tukiweka ushabiji pembeni
 
Sasa kama alishawahi kwenda Yanga day, kuna shida gani kwenda Simba day?
Na juzi alishatoa sababu kabla ya tamasha la yanga alipohojiwa TBC alisema wanaandaa mapokezi ya wageni arusha kwa ajili ya mkutano ila mshazoea kulalamika mlitaka mpaka kwenda ikulu kwa mama samia hamuwezi kuwa na akili.
 
Kwa .uonekano tu Karia ni mshamba na hajitambui hiyo nafasi ya rais wa tff aliipataje mara 2 mfululizo?

Ninamiss uongozi makini wa Leonard Tenga.
Karia ni mharo tu tukiweka ushabiji pembeni
Wa malinzi huumisi kama kweli alikuwa anatenda haki.
 
Mbona mama yenu hakuhudhuria na hamlalamiki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…