Leo katika historia yangu miaka mingi iliyopita, nilivyousumbua mtaa mzima usiku wa manane

Leo katika historia yangu miaka mingi iliyopita, nilivyousumbua mtaa mzima usiku wa manane

O
Katika makuzi yetu tunapitia changamoto nyingi sana, tunapitia moments/vituko ambavyo ni ngumu sana kuzisahau

hicho ni kituko changu nilichowahi kukifanya miaka fulani nikiwa katika foolish age, kama nawe unacho changia.

Baada ya kumaliza kupuliza nilienda ndani kulala, baada ya kuingia ndani nikawasha taa kisha nikanywa maji,sasa ile naenda kuzima taa kutupa macho kwenye kikabati cha viatu si nikaona Sneaker yangu nayoipenda(niliifua kama wiki hivi iliyopita nikawa nimeipumzisha kwanza)

Ghafra akili ikanijia ikiniambia "kwani ukilala umevaa viatu kuna ubaya gani? Si nikaenda nikavaa ile Sniker , nikazima taa kisha nikalala.

Katikati ya usingizi nikaota nakimbizwa na majini, yanataka yanivalishwe kwato ili niwe memba mwenzao,
Basi nikawa kila navyojaribu kukimbia nashindwa mpaka yakanikamata.

Yaliponikamata ikabidi yanikate miguu yote miwili kile kikanyagio(kiganja cha mguu),sasa ile yanaanza kunikata nikastuka usingizini, kutazama miguu naona kama damu, kujaribu kuitikisa naiona mizito halafu kama ina ganzi.

Nikaogopa sana nikapiga kelele, nyumba nzima wakaamka, ile wanakuja kunicheki nalia huku nimevaa viatu basi wakajua ni wachawi wamenivamia basi nyumba nzima wakaanza maombi kwa sauti kubwa sana mpaka majirani mtaa mzima wakaamka.

Mie tena kuona ndugu wanaomba, nikiunganisha na ndoto ya majini kunikata miguu, nikitikisa miguu(in reality) ni mizito, ukichanganya na wenge la usingizi na bangi, nikitizama miguu naona damu tupu basi nikapagawa mara 1000, nikazidi kupiga ukunga kwa nguvu.

Majirani/mtaa mzima wakapagawa, maana wanasikia makelele(ukunga) halafu wanasikia maombi ya maana, baadhi ya wazee waheshima wakaja mbio mbio(nasikitika sana nilivisumbua mpaka vizee vya watu) mpaka nyumbani kujua nini kinaendelea.

Upande wangu mie baada ya kupagawa kama dk 2 hivi ndo nikastuka kuwa zile sio damu ni sneaker zangu ninazozipenda(duh! niliishiwa pozi, nikitizama familia yangu ya kilokole wapo bize wanakemea, tazama madirishani watu wanachungulia wasijue nini kimetokea

Hapo ndo nakumbuka picha zima kuanzia kuvuta bangi mpaka nikipokuja kuingia ndani na kisha mawazo ya kuvaa sneaker

Ilikua simulizi ya wiki nzima mtaani, lakini walichokua wanasimuliana(nimevalishwa na wachawi) haikuwa kweli, ukweli nilibaki nao mimi.

Aisee mangi ulipiga ukungae....
 
Kwa taarifa yako jini hana kwato yupo kama wewe ila tofauti ni yeye kaumbwa kwa moto wewe umeumbwa kwa udongo.....
 
Kwa taarifa yako jini hana kwato yupo kama wewe ila tofauti ni yeye kaumbwa kwa moto wewe umeumbwa kwa udongo.....
mie sijawahi kumuona, hivyo kichwani nilikua na picha ya kusimuliwa
 
Back
Top Bottom