Leo katika historia

Leo katika historia

Joined
Apr 12, 2013
Posts
6
Reaction score
5
Tarehe kama ya leo mwaka 1954 TANU ilizaliwa. Mkutano wa uzinduzi wa TANU ulihudhuriwa na kikundi kidogo cha takriban watu 20 miongoni mwao Julius Nyerere, Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani, Schneider Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Iddi Faiz Mafongo, Iddi Tulio, Denis Phombeah na wengineo.

Julius Nyerere alichaguliwa rais wa TANU tarehe 17 Aprili, 1953; badala ya Abdulwahid Sykes ambae ni mtoto wa Kleist Sykes.
Kasella Bantu ndiyo mtu aliyempeleka Julius Nyerere kwa Abdulwahid kumtambulisha. Hii ilikuwa mwaka wa 1952. Bantu na Nyerere walikuwa wakijuana toka huko nyuma walipokuwa wakifundisha Tabora.

Ally Sykes ndiye aliyechora kadi ya TANU na kuchagua rangi na nembo yake. Rangi alizochagua zilikuwa nyeusi ikiwakilisha taifa la Kiafrika na kijani kwa ardhi ya Tanganyika. Mfano wa kadi ya TANU ilitokana na kadi yake ya Tanganyika Legion. Baada ya kumaliza kuichora ile kadi, aliwaendea Tanganyika Standard Newspapers ili wamchapishie.
Kutoka mfukoni mwake mwenyewe alichapisha kadi 1000 za kwanza na akitumia fedha za TAGSA alichapisha kadi nyingine 2000. Kadi nambari 1 ilitolewa na Ally Sykes kwa rais wa TANU, Julius Kambarage Nyerere na Ally aliweka sahihi yake kama afisa aliyeitoa. Ilipendekezwa kwamba kadi chache za mwanzo lazima zipigwe mnada na fedha zitakazokusanywa zitiwe kwenye hazina ya chama. Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz, Rupia na wengine walipanda dau kununua kadi hizo. Ally alimshinda kaka yake Abdulwahid kwa bei akapata kadi ya TANU nambari 2; Abdulwahid alipewa kadi nambari 3; Dossa Aziz kadi nambari 4; Phombeah kadi nambari 5; Dome Okochi, mmoja wa wale wazalendo kutoka Kenya katika TANU alipata kadi nambari 6 na Rupia kadi nambari 7. Bibi Titi kadi nambari 16; Iddi Tosiri kadi nambari 25.

Mara baada ya kuundwa kwa TANU ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulikuja Tanganyika mnamo Agosti, 1954. Kamati kuu ya TANU iliwakilisha madai yake kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliokuwa ukizuru Tanganyika.

TANU ilionyesha katika madai yake kuwa kwa Waafrika wa Tanganyika suala muhimu sana kwao lilikuwa kutafuta uvumbuzi wa ule mgogoro wa ardhi ya Wameru kwa njia za amani. Uzito wa jambo hilo kwa TANU unaweza kuonekana katika maneno ambayo inasemekana yaliandikwa na Abdulwahid, Nyerere, Stephen Mhando na Earl Seaton.

Huo ndio ulikuwa mwanzo wa Ukombozi wa Taifa letu. TANU ikamzaa CCM tarehe 5.2.1977. Mafanikio ya CCM yanatokana na nguzo imara iliyowekwa na TANU.
 
Nyie mmeshaiacha misingi ya TANU , historia haiwafundishi lolote nyie ......
 
Well said...tanu na hatimaye ccm ndio wajenzi halisi wa nchi hii
 
Mapunda
wewe ndio katibu mkuu wa uvccm,lakini kuna mada na mijadala mingi sana humu inayohusu ccm na uvccm huwa inajadiliwa bila majibu ya chama wala ya jumuiya...angalau nape anajitokeza tokeza...
swali1. Kazi yenu kama vijana ni nini hasa????
2. Wewe umejiunga jf mwaka mzima na zaidi sasa lakini sio active member kwanini? Wakati una smart phone ambayo ina access na internet?
3. Wenzenu wa upinzani wanawapiga kweli hapa, nyie mnatumia forum gani kutoa ufafanuzi na majibu ya hoja mbalimbali zinazoelekezwa uvccm na ccm?
4. Je ni kweli uvccm inakufakufa? Nawe ukiwa mtendaji mkuu??

cc
mapunda sixtus
 
Kwikwii , password imeibiwa huku jama, mbona kama unaelekea kukata Tamaa ? Au siku hizi no more buku 7 baada ya ziara za Kinana na Nnape kukomba fedha yote ?
 
Tarehe kama ya leo mwaka 1954 TANU ilizaliwa. Mkutano wa uzinduzi wa TANU ulihudhuriwa na kikundi kidogo cha takriban watu 20 miongoni mwao Julius Nyerere, Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani, Schneider Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Iddi Faiz Mafongo, Iddi Tulio, Denis Phombeah na wengineo.

Julius Nyerere alichaguliwa rais wa TANU tarehe 17 Aprili, 1953; badala ya Abdulwahid Sykes ambae ni mtoto wa Kleist Sykes.
Kasella Bantu ndiyo mtu aliyempeleka Julius Nyerere kwa Abdulwahid kumtambulisha. Hii ilikuwa mwaka wa 1952. Bantu na Nyerere walikuwa wakijuana toka huko nyuma walipokuwa wakifundisha Tabora.

Ally Sykes ndiye aliyechora kadi ya TANU na kuchagua rangi na nembo yake. Rangi alizochagua zilikuwa nyeusi ikiwakilisha taifa la Kiafrika na kijani kwa ardhi ya Tanganyika. Mfano wa kadi ya TANU ilitokana na kadi yake ya Tanganyika Legion. Baada ya kumaliza kuichora ile kadi, aliwaendea Tanganyika Standard Newspapers ili wamchapishie.
Kutoka mfukoni mwake mwenyewe alichapisha kadi 1000 za kwanza na akitumia fedha za TAGSA alichapisha kadi nyingine 2000. Kadi nambari 1 ilitolewa na Ally Sykes kwa rais wa TANU, Julius Kambarage Nyerere na Ally aliweka sahihi yake kama afisa aliyeitoa. Ilipendekezwa kwamba kadi chache za mwanzo lazima zipigwe mnada na fedha zitakazokusanywa zitiwe kwenye hazina ya chama. Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz, Rupia na wengine walipanda dau kununua kadi hizo. Ally alimshinda kaka yake Abdulwahid kwa bei akapata kadi ya TANU nambari 2; Abdulwahid alipewa kadi nambari 3; Dossa Aziz kadi nambari 4; Phombeah kadi nambari 5; Dome Okochi, mmoja wa wale wazalendo kutoka Kenya katika TANU alipata kadi nambari 6 na Rupia kadi nambari 7. Bibi Titi kadi nambari 16; Iddi Tosiri kadi nambari 25.

Mara baada ya kuundwa kwa TANU ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulikuja Tanganyika mnamo Agosti, 1954. Kamati kuu ya TANU iliwakilisha madai yake kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliokuwa ukizuru Tanganyika.

TANU ilionyesha katika madai yake kuwa kwa Waafrika wa Tanganyika suala muhimu sana kwao lilikuwa kutafuta uvumbuzi wa ule mgogoro wa ardhi ya Wameru kwa njia za amani. Uzito wa jambo hilo kwa TANU unaweza kuonekana katika maneno ambayo inasemekana yaliandikwa na Abdulwahid, Nyerere, Stephen Mhando na Earl Seaton.

Huo ndio ulikuwa mwanzo wa Ukombozi wa Taifa letu. TANU ikamzaa CCM tarehe 5.2.1977. Mafanikio ya CCM yanatokana na nguzo imara iliyowekwa na TANU.

Mapunda you must be sick or seeking attention.Sherehe hizi mnaweza fanya huko huko CCM maana mnayo sema hamyatendi you ate just pretenders wezi wakubwa wa mali zetu .
 
Inashangaza Sana Kuona Ccm Ya sasa Kukosa Muelekeo, Sasa Najiuliza Kwanini Viongozi Wa Ccm Hawarejei Historia Ya Asili Ya Chama Chao
 
Tarehe kama ya leo mwaka 1954 TANU ilizaliwa. Mkutano wa uzinduzi wa TANU ulihudhuriwa na kikundi kidogo cha takriban watu 20 miongoni mwao Julius Nyerere, Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani, Schneider Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Iddi Faiz Mafongo, Iddi Tulio, Denis Phombeah na wengineo.

Julius Nyerere alichaguliwa rais wa TANU tarehe 17 Aprili, 1953; badala ya Abdulwahid Sykes ambae ni mtoto wa Kleist Sykes.
Kasella Bantu ndiyo mtu aliyempeleka Julius Nyerere kwa Abdulwahid kumtambulisha. Hii ilikuwa mwaka wa 1952. Bantu na Nyerere walikuwa wakijuana toka huko nyuma walipokuwa wakifundisha Tabora.

Ally Sykes ndiye aliyechora kadi ya TANU na kuchagua rangi na nembo yake. Rangi alizochagua zilikuwa nyeusi ikiwakilisha taifa la Kiafrika na kijani kwa ardhi ya Tanganyika. Mfano wa kadi ya TANU ilitokana na kadi yake ya Tanganyika Legion. Baada ya kumaliza kuichora ile kadi, aliwaendea Tanganyika Standard Newspapers ili wamchapishie.
Kutoka mfukoni mwake mwenyewe alichapisha kadi 1000 za kwanza na akitumia fedha za TAGSA alichapisha kadi nyingine 2000. Kadi nambari 1 ilitolewa na Ally Sykes kwa rais wa TANU, Julius Kambarage Nyerere na Ally aliweka sahihi yake kama afisa aliyeitoa. Ilipendekezwa kwamba kadi chache za mwanzo lazima zipigwe mnada na fedha zitakazokusanywa zitiwe kwenye hazina ya chama. Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz, Rupia na wengine walipanda dau kununua kadi hizo. Ally alimshinda kaka yake Abdulwahid kwa bei akapata kadi ya TANU nambari 2; Abdulwahid alipewa kadi nambari 3; Dossa Aziz kadi nambari 4; Phombeah kadi nambari 5; Dome Okochi, mmoja wa wale wazalendo kutoka Kenya katika TANU alipata kadi nambari 6 na Rupia kadi nambari 7. Bibi Titi kadi nambari 16; Iddi Tosiri kadi nambari 25.

Mara baada ya kuundwa kwa TANU ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulikuja Tanganyika mnamo Agosti, 1954. Kamati kuu ya TANU iliwakilisha madai yake kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliokuwa ukizuru Tanganyika.

TANU ilionyesha katika madai yake kuwa kwa Waafrika wa Tanganyika suala muhimu sana kwao lilikuwa kutafuta uvumbuzi wa ule mgogoro wa ardhi ya Wameru kwa njia za amani. Uzito wa jambo hilo kwa TANU unaweza kuonekana katika maneno ambayo inasemekana yaliandikwa na Abdulwahid, Nyerere, Stephen Mhando na Earl Seaton.

Huo ndio ulikuwa mwanzo wa Ukombozi wa Taifa letu. TANU ikamzaa CCM tarehe 5.2.1977. Mafanikio ya CCM yanatokana na nguzo imara iliyowekwa na TANU.

Unasema mwa 1954 TANU ilizaliwa, afu unasema tena Julius Nyerere alichaguliwa rais wa TANU tarehe 17 april, 1953. Swali 1953 nyerere alichaguliwa kuwa rais wa TANU ipi na hiyo iliyozaliwa 1954 ni TANU ipi?
Mi sikufahamu ila lazima tu utakuwa kiongozi wa CCM
 
Mapunda
wewe ndio katibu mkuu wa uvccm,lakini kuna mada na mijadala mingi sana humu inayohusu ccm na uvccm huwa inajadiliwa bila majibu ya chama wala ya jumuiya...angalau nape anajitokeza tokeza...
swali1. Kazi yenu kama vijana ni nini hasa????
2. Wewe umejiunga jf mwaka mzima na zaidi sasa lakini sio active member kwanini? Wakati una smart phone ambayo ina access na internet?
3. Wenzenu wa upinzani wanawapiga kweli hapa, nyie mnatumia forum gani kutoa ufafanuzi na majibu ya hoja mbalimbali zinazoelekezwa uvccm na ccm?
4. Je ni kweli uvccm inakufakufa? Nawe ukiwa mtendaji mkuu??

cc
mapunda sixtus

Sio lazima niaapie na ac ya jina langu mfano nikitumia ac fek kama hii utajua ni nani mimi na lengo la jf ninkutumia ak feki watu wawe huru au sio mkuu nipo saaana humu kivingine tuuu
 
Unasema mwa 1954 TANU ilizaliwa, afu unasema tena Julius Nyerere alichaguliwa rais wa TANU tarehe 17 april, 1953. Swali 1953 nyerere alichaguliwa kuwa rais wa TANU ipi na hiyo iliyozaliwa 1954 ni TANU ipi?
Mi sikufahamu ila lazima tu utakuwa kiongozi wa CCM
ni katibu wa uvccm taifa
 
Umesema JK Nyerere ndo rais aliyechaguliwa na sio kuteuliwa?je kina nani alikuwa anachuana nao kwenye hiyo nafasi na nani alikuwa mpinzani wake mkubwa?
 
Wadau samahani kidogo nilibanwa na majukumu hivyo ikasababisha nijelewe kurespond baadhi ya hoja zenu kwa kifupi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alichaguliwa kuwa Rais wa TAA mwaka 1954. Chini ya uongozi mpya, Katiba ya TAA ilionekana kwamba isingeweza kukidhi malengo ya kisiasa. Mwalimu alipewa jukumu la kuandaa Katiba mpya ya TAA ambayo ingezingatia malengo ya kisiasa. Baada ya uandaaji wa Katiba hiyo kukamilika, haja ya kubadili jina ilionekana dhahiri na majina mengi yalipendekezwa likiwemo la TANU. Nafasi ya TAA ilichukuliwa na TANU iliyozaliwa tarehe 7 Julai, 1954. TANU ilirithi matawi ya TAA, wanachama na viongozi wa TAA katika maeneo mengi.
 
Kwa wale wanaotaka kujua uhai wa Jumuiya yetu ya Vijana kuwa upo hai au umekufa, ukweli ni kwamba UVCCM ipo hai ina nguvu nainaendelea vizuri kutekeleza majukumu yake ya kikanuni na kikatiba ingawa changamoto katika taasisi yeyote ni jambo la kawaida kutokea.
 
Back
Top Bottom