Leo kilele cha Wiki ya Maji, tuorodheshe changamoto hapa

Leo kilele cha Wiki ya Maji, tuorodheshe changamoto hapa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Mgeni rasmi Mheshimiwa Rais mahali ni Mlimani City kauli mbiu ni maji chini ya ardhi hazina isiyoonekana. Ratiba ya shughuli hio hapo katika picha.

Ushauri wangu mimi kama mdau wa hii sekta nashauri bodi za Bonde ziachane na mapendekezo ya ada mpya na leseni hasa za visima.

Wamiliki wanalalamika sana kipindi cha kulipia maduhuri wanadai hio hela kubwa sana, bora hii 250000 ya water use permit ila hii ya matumizi ya kila mwaka ada kutokana na maji anayo abstract wanaona kubwa sana taasisi za dini hali mbaya kutokana na Vita ya Ukraine hawapati Tena misaada toka Ulaya.

Bora wamiliki wa sheli wapo tayari kulipia wao Wana pesa ila sio hawa wafanyabiashara wa lodge na wengineo wanalalamika sana. uangalie Sana hiki kipengele tupunguze hii fees walau iwe 50000.

Wadau changamoto nyingine tuorodheshe wahusika wazione. Nawasilisha

Screenshot_20220322-064302.jpg
 
Nimewambia RUWASA inaandaa utaratibu wa kuwashirikisha jamii kuchanga maji [kulipia] matumizi ya maji ambapo watawekewa mita
Naomba kufahamu. Hawa wananchi wa vijijini wanaohudumiwa na RUWASA watakuwa wanalilia kwa kiwango Gani kwa kila unit au mita ya ujazo?

Watalipa sawa na malipo ya mjini?
 
Nimewambia RUWASA inaandaa utaratibu wa kuwashirikisha jamii kuchanga maji [kulipia] matumizi ya maji ambapo watawekewa mita
Naomba kufahamu, Hawa wananchi wa vijijini wanaohudumiwa na RUWASA watakuwa wanalilia kwa kiwango Gani kwa kila unit au mita ya ujazo?
Watalipa sawa na malipo ya mjini?
Inategemea na mradi husika maana jumuiya ya watumia maji nyingine inavuta maji kwa pampu za umeme wengine solar wengine mafuta so lazima Bei itofautiane kila cbwos inaenda kivyake.bei haiko flat rate
 
Inategemea na mradi husika maana jumuiya ya watumia maji nyingine inavuta maji kwa pampu za umeme wengine solar wengine mafuta so lazima Bei itofautiane kila cbwos inaenda kivyake.bei haiko flat rate
Nashukuru sana kwa maelezo hayo.
 
Back
Top Bottom