View attachment 864420
USHUJAA #3
Mmamo April,1943 majeshi ya washirika yalipanga kuteka mji wa Zwolle,uholanzi. Ilitolewa tangazo na commander wa kikosi chao kuwa wajitolee kwenda kukusanya taarifa za adui na ngome zake ili jeshi zima likivamia basi wawe na taarifa za uhakika kuhusu adui. Wengi kwa kujua nguvu ya jeshi la ujerumani waliogopa ila leo major na mwenzie mmoja bwana willy arseneault walikubali kujitolea. Usiku walipokwenda kupeleleza bwana willy alionekana na wanajeshi wa kijerumani hivyo alidunguliwa na risasi za adui na kufariku hapo hapo. Tukio hili lilimuumiza sana leo major na licha ya kukimbia sababu alikuwa ameonekana aliamua kuvamia "kijiwe" hicho cha adui na kufanikiwa kuua wawili huku wengine wakikimbia na gari. Hakuishia hapo alisonga mbele na kuteka gari ya kijeshi la ujerumani hivyo aliweza kupenya hadi ndani ya mji wa zwolle ambapo alifanikiwa kuingia kwenye bar ambayo ina askari mwenye cheo wa ujerumani, ambapo alimpiga mkwara kuwa jeshi la washirika limeshazingira mji na litashambulia muda wowote hivyo akamuachua yule kamanda aende kuwataarifu wenzake. Alipotoka humo alienda kutega mabomu kwenye maeneo tofauti (sio makazi ya watu) na yalipoanza kulipuka moja baada ya nyingine wanajeshi wajerumani walifikiri ndio majeshi ya washirika yamevamia hivyo wakaanza kupanick sababu hawakuwa wameona majeshi yakija mji huo ila bado wanasikia milipuko so walipigwa na butwaa. Alichokifanya Leo major ni kubadilisha maeneo ya mashambulizi yaani anadungua mwanajeshi mmoja mtaa huu alafu anahamia mtaa wa pili na kushoot .mwingine hii ikajenga picha kuwa majeshi ya washirika yameshajipenyeza kwenye ngome na ukiongezea na ili milipuko basi wajerumani wakajua hawana chao hivyo askari zaidi ya 800 wakautekeleza mji ili wakajipange upya. Hivyo leo major kwa mara nyingine badala ya kurudi na taarifa za kiintelijensia kuhusu ADUI yeye alirudi na taarifa kuwa HAKUNA ADUI katika mji wa Zwolle. Kwa ushujaa huu alipewa kwa mara nyingine medali ya juu ya heshima jeshini ya DCM maana aliokoa mji mzima dhidi ya umwagaji damu kama jeshi la washirika lingevamia mji huo. Kitendo hiki cha kishujaa kilisababisha jina la mtaa huko uholanzi lipewe kwa heshima yake kama mkombozi wao.
View attachment 864422
USHUJAA VITA YA KOREA
Leo major baada ya vita ya pili ya dunia hakuishia hapo bali alishiriki na vita ya korea iliyotokea mwaka 1950 ambapo korea kusini ilivamiwa na vikosi vya kikomunisti kutokea upande wa kaskazini wa korea hivyo marekani na washirika wake wakiwa chini ya bendera ya UN walivamia korea ili kuzuia wakomunisti. Leo major hakuwa nyuma kwenye vitendo vyake vya kishujaa tena hasa katika Battle ya Maryang san ambapo ilikuwa ni mission ya kuteka mlima ambao ulikuwa muhimu sana kwani ulikuwa unaona mzunguko wa mile 14. November 22,1951 jeshi la China lilivamia likiwa na kikosi cha wanajeshi 40,000 na kufanikiwa kuwafurumusha vikosi vya wamarekani kutoka kilima hicho. Na siku kadhaa baadae jeshi la marekani lilifanya shambulizi kuukomboa mlima huo ili walikutana na kipigo kikali hivyo mission ikaishia hapo. Kwa kuona haya kamandi ya brigade yake ikaamua kumteua Leo major na vijana wake kama 20 ambao ni wadunguaji/snipers waweze kupata upenyo na kuvuruga ngome ya adui. Leo major na vijana wake waliweza kutambaa na kujipenyeza kwenye ngoma ya adui hadi juu ya kilima. Walipofika juu wakaanza kudungua wanajeshi wa kichina mmoja baada ya mwingine hii ilitengeneza panick kwenye kambi ya wachina maana walijiuliza kivipi shambulizi litokee katikati ya ngome yao ilihali adui yupo chini ya mlima? Aliweza kupambana na vikosi hivyo vya wachina usiku kucha huku akiwasaidia majeshi yaliokuwa chini kupata urahisi wa kushambuli ngome hiyo na mwisho wa siku kuwezesha Leo major na kikosi chake kuweza kuteka kilima hicho na kuletea ushindi vikosi vya washirika dhidi ya jeshi la china. Na kwa ushujaa huu alitunukiwa medali ya juu ya heshima ya kijeshi kwa mara nyingine tena sababu ya ushujaa wake.
View attachment 864423
HITIMISHO
Kupitia mtu huyu tunaweza jifunza kutokukata tamaa kwenye maisha maana licha ya changamoto za kupata ulemavu wa jicho na baadae kuvunjika mgongo ila bado aliweza endelea na vita hadi kushinda medali hizo. Pia story kama hizi najua watanzania tunazo mfano ya yule askari wa Tanzania kule Darfur ambaye alipambana na "brigade" ya waasi na kuwapunguza hadi risasi yake ya mwisho ndipo akauawa ila shida nyingi zinafanywa siri ila ni wakati na sisi tuanze kuwatambua mashujaa kama hawa ili hata watoto wa vizazi hivi wajengewe moyo wa kujitoa kwa ajili ya nchi yao licha ya changamoto zingine.
Naomba kuwasilisha.