Leo Mlimani city imekuwa kama Tandale kwa mfuga mbwa, nyie wenzetu hamna ustaarabu?

Leo Mlimani city imekuwa kama Tandale kwa mfuga mbwa, nyie wenzetu hamna ustaarabu?

Tukio la siku moja ambalo linawahusisha watoto wengi lisikutoe imani, kuna watu bila shaka wameajiriwa au wamepewa tenda kufanya usafi hapo, kwa hiyo ni swala ambalo katika hali ya kawaida halistahili mtu timamu kufungua uzi wa kutoa povu.....
 
Tatizo la waekezaji...

Wameweka Mlimani City moja tuu miaka yote hiyoo...

Hivi hakuna muwekezaji anayetaka liwekeza Moli huku Mbagala kwetu ili sikukuu tuache kwenda kuwachafulia Moli yao....

Halafu muwekezaji mwingine awekeze swimming puli kubwaaa hukuhuku Mbagala tuache kwenda coco bichi kubakwa na wakodisha matairi khaa....!

Wawekezaji tafadhali mkuje Mbagala.
... kwani hapakuwa na NAKUMAT? Hapakuwa na mall nyingine kubwa pale Nyerere Rd. baada ya Kiwanda cha Sigara kama unaelekea mjini? Hizo zote ziliishia wapi? Awamu ya 5!
 
... kwani hapakuwa na NAKUMAT? Hapakuwa na mall nyingine kubwa pale Nyerere Rd. baada ya Kiwanda cha Sigara kama unaelekea mjini? Hizo zote ziliishia wapi? Awamu ya 5!

Muwekezaji anatakiwa aje awekeze Moli Mbagala sio Pugu Mall, ile ni ya watu wa Gongolamboto.
 
Muwekezaji anatakiwa aje awekeze Moli Mbagala sio Pugu Mall, ile ni ya watu wa Gongolamboto.
... nani mwekezaji wa maana atawekeza kwenye nchi ambayo haitabiriki kesho rais akiamka ataamua nini kuhusu uwekezaji? Awamu ya 5 imefumbua wengi macho.
 
We jamaa unaumia kuona wenzako wanafurahi, ulijua umejichanga peke yako?

Mlimani City sehemu nzuri ni kwa nje upande wa samaki samaki, sio humo ndani.
 
Tangu lini watu wa uswahilini wakawa na ustaarabu.

Mlimani city wawe wanapiga marufuku watu wa uswazi kwenda hapo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hapo tatizo ni wewe na ushamba wako wa kwenda Mlimani City siku ya sikukuu, hapo utarudi tena mwakani... Hilo jambo la kawaida hasa idadi ya watu inapokua kubwa kuliko matarajio
 
Lakini sisi wamatumbi wengi wetu uchafu tumeuzoea. Mpe nyumba mpya mmatumbi baada ya miezi sita hamu nayo huna.
 
Hapo tatizo ni wewe na ushamba wako wa kwenda Mlimani City siku ya sikukuu, hapo utarudi tena mwakani... Hilo jambo la kawaida hasa idadi ya watu inapokua kubwa kuliko matarajio
Ustaarabu ni siku zote, hata kama ni sikukuu
 
Back
Top Bottom