LEO MWISHO
“ Hivi Jacob lini utaelewa Kwamba maisha sio kitu cha mchezo, leo mimi nipo kesho na keshokutwa nitakufa , hivi utakuwa mgeni wa nani?”
kama kawaida Martin alirudia wimbo ule ule kwa Jacob ambaye ndo mtoto wake wa kiume na wa pekee.Martin alijaaliwa kupata mtoto mmoja tu ambaye anaishi nae kwenye nyumba ya vyumba viwili waliyopanga. Mama yake Jacob aliondoka kipindi Jacob ana miaka mitatu kwani alichoka vipigo na matusi ya Martin aliyekuwa mlevi wa kupindukia. Kila usiku ulipoingia kulikuwa na vurugu iliyoambatana na matusi yasiyokuwa na msingi wowote. Hayakuwa maisha rahisi kwa sofia hivyo aliamua kumtelekeza Jacob na baba yake na yeye kuondoka pasipojulikana .
Martin hakuwa na lakufanya ila kumlea Jacob, jambo amabalo halikua rahisi kwani mtu pekee aliyekuwa msaidizi wake alikuwa ni sofia ambaye hayupo nae tena. Jacob aliyekuwa na miaka kumi na nne sasa alifanikiwa kufika mpaka darasa la sita tu kwani maisha yalimlazimu kuingia mtaani na kuanza kujitafutia kitu kwa ajili yake na baba yake. Mzee Tino kama Jacob alivyokua anamuita wakati wote hakua mtu wa kutegmewa, na pesa yake yote aliyoipata kwenye kazi yake ya kubeba mizigo viwandani aliimalizia kwenye pombe kwani ndo kitu pekee kilichokuja kichwani kwake mara tu alipopata pesa yoyote ile. Jacob aliishi chini ya paa lililoshuhudia matusi na ugomvi wa baba na mwana uliotokea kila iitwapo leo na haikuonekana kama Martin alijifunza baada ya mkewe kumkimbia kwani vipigo viligeuka kwa Jacob badala yake.
Leo ilikuwa ni siku nyingine ambayo haikuonekana kuwa salama kwani Martin aliyekuwa amekwishalewa tayari alikuwa akimwambia maneno ya busara Jacob na kujifanya kama mtu kweli. Jacob alikwisha zoea maigizo kama haya kutoka kwa baba yake aliyelewa hivyo hakusumbuka hata kumjibu. Alipita pale ukumbini na kuingia chumbani kwake moja kwa moja.
“ Haa! Jacob unanidharau mimi baba yako mzazi, Unanigeuzia mgongo . Ngoja nitakuonyesha kama mimi nimeliona jua kabla yako”
Martin alifoka kwa sauti na kuinuka kutoka kweye kiti alichokuwa amekaa huku akiyumba yumba, alisogea mpaka kwenye mlango wa chumba cha Jacob na kuupiga teke la nguvu lililosababisha komeo la ule mlango kuachia na kufunguka kwa kasi.
“Njoo hapa we mbwa mweusi, nikufunze jinsi ya kuheshimu”
Jacob alijua kitakachotokea , aliinuka pale kitandani na kupita kwa kasi pale mlangoni akamsukuma baba yake kwa kiwiko cha mkono na kumwangusha chini.Hakujali alichokifanya na alitoka nje moja kwa moja akimwacha baba yake akilalamika na kutukana pale chini. Leo varangati lilianza mapema sana kuliko kawaida , ilikuwa saa mbili na nusu ya usiku tu na Martin alianza vurugu. Jacob hakuangalia nyuma wala kushtuka na aliendelea kuondoka kuelekea kule ambapo atapata kitu cha kumfanya atulize kichwa chake. Alikatisha katika vichochoro ambavyo ndio njia zake kuu kila alipoenda kupata kitu.kipindi anatembea alitoa kisu alichokichomeka kwenye kiuno na kukiangalia .
Kilikuwa ni kisu cha wastani kilichokuwa kikali sana ambacho hakuwahi kukiacha kila alipokwenda .Alikificha kile kisu haraka baada ya kumwona mwaamke mmoja aliyetokea ghafla katika kona ya mbele yake. Bila ya yule mwanamke kumwona alirudi nyuma na kujificha kwenye kona ya nyuma yake. Hakuwa na hili wala lile lakini bahati kama hizi haziji mara mbili maishani. “Zari la usiku usiku” alijisemea kimoyo moyo.
Yule mdada alipotokeza tu kwenye ile kona aliyojificha, Jacob alimuwahi na kumkaba shingoni huku akimwonyeshea kisu “oya saula kila ulichokua nacho” alimwambia kwa sauti nzito .Yule dada hakuwa na lakufanya kwani kisu kilikua mbele ya uso wake, alimpatia simu janja aliyokuwa ameishika mkononi ili kuinusuru nafsi yake . Jacob alivyochukuwa ile simu alimwachia na kukimbia haraka kadri alivyoweza akimwacha yule mdada akilia na kupiga kelele za mwizi , lakini haikusaidia kwani Jacob alikwishatoweka eneo lile
Jacob alikimbia bila kusimama mpaka kwa rafiki yake Daniel na kugonga mlago huku akihema. “Oya dompo ... fugungua ….oya” Daniel alifungua mlango haraka kwani alishajua kuwa Jacob kashaliamsha huko. Haraka Jacob aliigia mpaka ndani na kujibwaga kitandani akicheka huku anahema “Oya ……kuna ndezi mmoja kajipitisha saiti ….. halafu mi nna mikazo kama yote .. dah! Nikasema zari hili” alimwbia Daniel huku akihema . “ kwahiyo ukaunga” aliuliza Daniel huki akifunga mlango “oya ……sa nifayaje, nikamtolea kubwa akaanza kulia lia pale …. Nikamwambia saula basi ndo akanifosia tambo” alijibu Jacob na kutoa ile simu na kumpatia Daniel “Dah sema hichi kifaa mwanangu , leo kweli umepata zari” alisema Daniel alipokuwa akiiangalia ile simu “Oya ilo tambo utalisukuma kesho basi, mi nifosie kete tano mana hata sielewi man” alisema Jacob “Tano?” aliuliza Daniel kwa mshangao “ndio kwani vipi?” alisema Jacob “oya tano sio mchezo man, utadorora” Daniel alimwambia Jacob kwani si kawaida yake kutumia kete tano za bangi kwa usiku mmoja. “ oya vipi nipe basi , mbona unanizingua, Mi sielewi mwanangu “ alisema Jacob . Daniel hakutaka kulipeleka lile swala mbali , alimpatia Jacob zile kete tano za bangi kama alivyotaka . “oi kesho man , mi ngoja nisepe” alsema Jacob na kuondoka kuelekea nyumbani.
Alitumia dakika ishirini mpaka kufika kwao na sasa ilishatimu saa tatu na dakika arobaini usiku. Alifungua mlango na kuingia moja kwa moja mpaka chumbani kwake na kuketi juu ya kitanda chake . Alishusha pumzi na kuchukua kibiriti kilichokua kwenye stuli mpembrni yake na kukiweka pembeni yake . Alitoa zile kete zote alizochukua akazifungua na kuanza kuzisokota kiganjani mwake.
Hakutaka kujisumbua kutengeneza vipisi vidogo vidogo na akaiviringisha ile bangi yote kwenye karatasi moja . Alipomaliza aliiwasha ile sigara ya bangi yenye ukubwa kama kidole cha kati na kuanza kuivuta taratibu huku akitoa moshi mdomoni na puani. Baada ya dakika tatu aliimaliza ile sigara yote na akajilaza kitandani .
Ghafla Buh! Mlango wa chumbani kwake uligongwa kwa nguvu sana na kumfanya ashituke. Alitoka kwenye ulimwengu wa mbali alioenda kimawazo na kuanza kusikia matusi ya Martin . Martin aliendelea kupiga kelele kwa sauti ya juu na kumtukana Jacob huku akipiga ule mlango kwa mateke.
Jacob hakuweza kuvumilia alitoka na akausukuma ule mlango na kumwangusha baba yak chini. Kabla Martin haja inuka pale chini Jacob alimkalia na kumchoma kisu cha shingo. Aliendelea kumchoma na kumchoma huku akicheka kwa sauti ya juu sana kana kwamba alichanganyikiwa , Alimchoma hadi sehemu kubwa ya nyama pale shingoni ilitoka na kuacha shimo, kisha aliinuka na kukimbia nje huku akicheka na kumuacha baba yake akikata roho.

Upvote
0