LEO naomba niongee na Wazee wa Kubet almaarufu kama Maafisa Wakamalia ambao ni walipa KODI

AXIOM APEX VERBOSE

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
13,769
Reaction score
23,676
Kwanza, kwenye mada hii nitaanza na kusema kwamba salamu kwenu wote ziwafikie popote mlipo.

Pili, nina jambo langu muhimu nataka kushea na nyinyi wote. Najua humu mpo wengi sana.

Tatu, mada hii ni ndefu sana ila nitahakikisha naifupisha kwa kadri ninavyoweza.

Nne, unapoingia kwenye betting tembea na Mungu. Zingatia sana hapo. Kushindwa na kushinda inategemea Mungu amesimama na wewe kiasi gani.

Tano, unapoingia kwenye betting jua ni muda gani una shinda na muda gani unashindwa. Hapa inabidi utulize kichwa ili unielewe hauwezi kushinda wewe kuanzia asubuhi mpaka usiku. Lazima ushindwe tu.

Sita, unapoingia kwenye betting jua mlango wa kuingilia na mlango wa kutokea. Zingatia sana hii itakusaidia usiendeshwe na tamaa. Kuna muda inakupasa utembee na kuna wakati inakupasa ukimbie. Usipokua makini utakimbizwa.

Saba, unapoingia kwenye betting usiwekeze kiasi ambacho utajutia kukipoteza. Hapa ndipo pa muhimu zaidi. Chukua ziada weka kwenye betting hata ukipoteza haikuumizi.

Nane, unapoingia kwenye betting jua kutenganisha muda wa betting na muda wa kazi zako binafsi. Hauwezi muda wote wewe ukawa unabet na ukashinda hio haipo.

Tisa, hii ni siri nakupa na ni siri muhimu sana, unapoingia kwenye betting ukapiga mshindo, chukua pesa zako ondoka. Naomba hii usiniulize kwanini majibu unayo.

Kumi, unapoingia kwenye betting usichukulie km mchezo chukulia km mashindano maana kuna kushinda na kushindwa, usipumbazwe na wanaokwambia michezo ya kubahatisha ule sio mchezo ni shindano la kubahatisha, anaeshinda ndie anaelipwa hakuna kucheza pale ni kushindana mwanzo mpaka mwisho.

Kumi na 1, nitagusia kwenye biblia kidogo, km wewe ni mpenzi wa kusoma biblia utakubariana na mimi kwamba betting sio haramu km wengi wanavyoiongelea. Kwanini? Kwa sababu kwenye kitabu cha Ayubu tunasoma kwamba Mungu alibet na Shetani juu ya Ayuby. Ukisoma Ayubu 1:6-12 kila kitu kinajieleza. Na mwishoni tunaona kwamba Mungu alishinda na Shetani akashindwa.

Kumi na 2, ni kwamba bet kiistaarabu unapoingia kwenye betting jitahidi ujidhibiti mwenyewe. Hapa nitakupa siri nyingine usiyoijua ukishinda usiziache pesa ndani zitoe nje hio itakufungulia milango ya pesa nyingi kutoka nje. Unapoziacha ndani pesa zote zitarudi ndani.

Kumi na 3, hii ni ya kumalizia kwa wewe ambae hujawahi kushiriki mashindano ya kubahatisha cha kukushauri kabla hujaingia kwenye hayo mashindano usome mchezo ulivyo ndipo na wewe uingie usiingie kichwa kichwa.

Kumi na 4, hii ni km bonus, chagua mchezo unaouweza na ucheze huo tu usitake kuchezacheza kila mchezo hio haipo utaishia kujilaumu tu.

Sijasema mchezo unaoupenda nimesema mchezo unaouweza.

Mfano mimi mchezo ninaouweza ni mpira wa miguu basi nitashiriki kwenye mashindano ya kubatisha mpira wa miguu tu na sio vinginevyo, sitoingia kwenye basketball, tennis wala 3 mzuka. Sababu mchezo ninaouweza kubahatisha ni mpira wa miguu.

Kumi na 5, zingatia sana ibada. Tunasema kazi na sala. Usijione km kila unapopata ushindi ni wewe unaeshinda hapana nyuma yako yupo Mungu anakushindia. Mshukuru yeye kwa kidogo anachokupa wagawie na wengine utaongezewa, ukitoa 10 utapewa 100.

Nimemaliza.
Una swali uliza, nitakujibu.
 
Nimekuelewa mkuu
 
Attachments

  • IMG-20260925-WA0001.jpg
    IMG-20260925-WA0001.jpg
    147.5 KB · Views: 11

Umesomea chuo gani hicho kinachofundisha utaalam wa kubet?
 
Kumbe tunaobett tuna akili namna hii
Akili zipo tu hata kwa wasiobet ila jua kuzungusha coin vizuri ujue muda gani linakua kichwa na muda gani linakua mwenge

Kabla mpira haujaanza refa huwaita makaptein wa timu zote 2 pale kati waende wakabet mara moja, mmoja anachukua kichwa mwingine anasema mimi mwenge refa anaitupa shilling juu kisha ikitua chini wanaangalia nani kapata aliesema kichwa au aliesema mwenge
 
Noted usiweke hela ambayo ukiliwa unapararaiz😂😂
At your own risk unaweza kustake all ukijua kabisa hapa kuna uwezekano 100% nashinda hapo unasogeza kibunda chote ndani, tumia ziada pekee usiwekeze kiasi cha kukuumiza ukaanza kutoa milio weka kiasi aambacho hata ukipoteza utaishia kucheka tu na haiumi
 
Kingine ,, lazima ujuelize kwanini una bet ?? ,,, ukijibu Tena jiulize Tena nikiasi gani ungependa ushinde ( hii umeshaisemea kwa namna Fulani ) . Na katika huo mchakato wa kutafuta hicho kiasi upo tayari kupoteza kiasi gani ? Hii itasaidia kujua ni muda gani uache ndala ..
 
Back
Top Bottom