Leo ndio nimeamini kwamba hizi "Odometer" zinachezewa!

Mbalamwezi1

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2013
Posts
2,073
Reaction score
2,026
Kuna jamaa yangu kanunua gari ndogo, odometer inasoma elfu ishirini na kitu(20,6..) Gari imetengenezwa mwaka 2003/02 na imeingia TZ mwaka 2016. Sasa nilivyoiona hyo gari inamuonekano mzuri bado nje mpk ndani ila hizo odometer zikanistua, nikajiuliza ina maana huyu jamaa mmiliki wa kwanza alinunua ikiwa zero km au?! Basi nikaanza ufukunyuku bahati nzuri nikaliona file la ile gari, nikapekua nikakuta doc moja ina maelezo kuhusu hilo gari, sasa nikafika kwenye kipengele kimeandikwa "Inspected odometer(reading km)" nikakuta kimeandikwa '194,856' nikajisemea tu oohooo jamaa kishapigwa!
MY TAKE:
Unaponunua gari used bongo kuwa makini sana hasa ukikuta gari inasoma chini ya laki moja, wauza magari wengi si waaminifu hasa linapokuja suala odometer, na ukienda kununua gari usiangalie odometer peke yake kagua gari vzr ujiridhishe maana unaweza kujikuta unanunua gari lililokuwa linatafuta wa kumfia!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwan jamaa alivonunua alikwambia kanununua kwa ajil ya odometer ...na kapigwa kivp kama wewe mwenyewe unaona gari kali hata ingefikisha kilometa laki saba
 
kwan jamaa alivonunua alikwambia kanununua kwa ajil ya odometer ...na kapigwa kivp kama wewe mwenyewe unaona gari kali hata ingefikisha kilometa laki saba
Mkuu unafanyaga kazi kushusha odometer nikuletee gari maana kila nikilipeka kuliuza jamaa wanasema imetembea sana?!nataka nizishushe ili liuzike fasta!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu wenzetu mataifa yaliyoendelea gari za engines ndogo huwa hawapigi nazo masafa.. unakuta ilikuwa inatumiwa na dogo kwenda college na kurudi alivyomaliza akamuachia mdogo ake naye akamuachia mdogo ake sasa wote wamemaliza shule likapelekwa mnadani..

tofauti na sisi huku gari ya 1.2 engine unapiga nayo trip ya 1500km wenzetu huwa wana magari maalumu kupiga hizi trips

ndio maana kununua ist ya 2005 ikiwa na 65000km na mark x ya 2012 ikiwa na 150000km sio kitu cha kushangaza
 
My concern ni kwamba, mfano hyo mark x si inasoma 150000km, ikija bongo hyo wanashusha, na hyo ist ya 65000km inakuja bongo mtu anatembelea kwa muda/miaka kadhaa lets say inakuwa 130000km then akitaka kuiuza anaishusha mpk inakuwa 80000km kwa mfano ndo anaiuza!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kununua gari used bongo ni mikosi mkuu,kuna watu huwa wanaangalia Reg no nao huwa siwaelewi.Kuna magari no B au C hasa land cruiser na bado zipo mbichi kabisa na Engine zake zipo ok
 
Odo sio inshu bro, kikubwa ni ubora wa gari engine kinanda gear box gitaa,hayo mengine wapelekee wakolomije
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…