Mbalamwezi1
JF-Expert Member
- Dec 20, 2013
- 2,073
- 2,026
Kuna jamaa yangu kanunua gari ndogo, odometer inasoma elfu ishirini na kitu(20,6..) Gari imetengenezwa mwaka 2003/02 na imeingia TZ mwaka 2016. Sasa nilivyoiona hyo gari inamuonekano mzuri bado nje mpk ndani ila hizo odometer zikanistua, nikajiuliza ina maana huyu jamaa mmiliki wa kwanza alinunua ikiwa zero km au?! Basi nikaanza ufukunyuku bahati nzuri nikaliona file la ile gari, nikapekua nikakuta doc moja ina maelezo kuhusu hilo gari, sasa nikafika kwenye kipengele kimeandikwa "Inspected odometer(reading km)" nikakuta kimeandikwa '194,856' nikajisemea tu oohooo jamaa kishapigwa!
MY TAKE:
Unaponunua gari used bongo kuwa makini sana hasa ukikuta gari inasoma chini ya laki moja, wauza magari wengi si waaminifu hasa linapokuja suala odometer, na ukienda kununua gari usiangalie odometer peke yake kagua gari vzr ujiridhishe maana unaweza kujikuta unanunua gari lililokuwa linatafuta wa kumfia!!
Sent using Jamii Forums mobile app