Leo ndio nimejua kwanini wanawake wanajiingiza katika tabia za udangaji

Leo ndio nimejua kwanini wanawake wanajiingiza katika tabia za udangaji

Kwa aambao hamjui kozi ya maendeleo ya jamii yaani Development studies (DS) ni kozi mpya ipo UDOM na UDSM kwa ngazi ya degree

Nafikirii hapo tufunge kurasa kama huelewi nenda google
Course mpya na wewe ulisema umemaliza chuo una miaka miwili nyumbani na ulimalizia Mzumbe..hahaha
 
Hapa nilipo nina majonzi, roho imeniuma sana kwa kuzaliwa kwenye familia maskini

Ipo hivi mimi kwetu ndio wa mwisho msichana peke yangu kati ya watoto 6.. Mzee wangu alitangulia mbele za haki hivyo tumebaki na mama tu.. hao ndugu zangu wote hawana maisha ya kueleweka isipokuwa mmoja tu angalau yeye ameajiliwa serikalini ndio kidogo anaibeba familia, yeye ameshaoa ana familia yake

Mimi nimeshahitimu chuo nina kama Miaka miwili nyumbani.. nimepata sehemu ya kujishikiza wananilipa 250000.. Kwetu ni bunju nafanyia kazi magomeni kila siku natumia 5000 yaani 3000 nauli 2000 nakula mchana hapo Ndio najibana mno..

Sasa kwasasa Hivi nyumbani Hakuna mtu nipo peke yangu mama ameenda kijijini kwao bibi anaumwa, mama yangu hana kazi ile ya kumtegemea anauza chupa za maji hivyo siwezi kumsumbua kwa chochote, amesafiri hajaniachia hata shilingi 100.. Hakuna chakula ndani Hakuna chochote, nachofanya nikitoka kazini nashukia kwa brother nakuta wamepika nakula naondoka

Leo nimeumia sana sijaenda kazini Nina siku 2 sina nauli hela niliokuwa nayo akiba imeisha nimemuomba bro kasema yeye hana hela hawezi kuwa anatoa hela mara mbili mbili kwa familia yake na kwangu, Kama niliweza kutafuta kazi basi nijitegemee nauli nikitaka kula nije nyumbani,, nikamuuliza sasa nitatoa wapi na Ndio naanza kazi akanijibu nitajua mwenyewe

Hiyo kauli imeniuma yaani anamaana gani kusema nipambane nitafute nauli yaani naitafutia wapi ..

Leo nimeacha kuwa judge Watu na maisha wanayoishi Kama ndugu yangu wa damu ananiambia maneno haya hao wa nnje watanijibu vipi

Ni hayo tu wakuu
Weka namba pm dogo nikuchangie nauli ya kazini
 
Sasa ndugu si uachane na uzi wa wasio na akili mbona unaniganda!!

Kama unanifahamu si utume picha yangu ili uwathibitishie watu

Sema nini nilichogundua wewe una roho mbaya [emoji120]
Me kweli roho mbaya ninayo, hujakosea. Lakini ni watu kama wewe ndo mmenifanya niwe na roho mbaya kwa sababu wengi wenu sio wa kweli. Duniani hapa mmetufundisha ukatili sana. Kwanini mdanganye kwenye maswala serious..?
 
Back
Top Bottom