Wanabodi, nadhani wengi mtakumbuka kuwa taarifa za vyombo vya habari hasa magazeti zilitueleza kuwa ndoa ya Slaa na mchumba wake (Josephine) imepangwa kufanyika Julai 21, 2012 yaani leo hii Jumamosi huko Karatu. Lakini kulikuwa na uingiliaji wa Mhe. Rose Kamili (mke na mzazi mwenzake Dk. Slaa) ambaye alikwenda mahakamani. Lakini licha ya kwenda mahakamani kulikuwa na maelezo ndoa hiyo ni lazima ifanyike. Mwenye updates plse tuleteeni kuhusu kiongozi huyu ambaye tuliona watoto wake na Mhe. Rose wakitambulishwa bungeni wakati bajeti ya wizara ya kilimo ilipokuwa ikisomwa. Tupeni taarifa kuhusu Slaa.