Leo ngoja nivisanue hivi vitoto va Gen Z

Of course ni kawaida kabisa kwa kizazi kikubwa kuwatazama kizazi kinachofuata kwa jicho la kuwatoa dosari kwa kila jambo.

Hata sisi wazazi walitodadisi kwa mengi kama uvaaji, mwenendo na kadhalika.

Wakati wetu umefika sasa kuwashangaa hawa madogo kwa uhovyo wao na kutoheshimu mamlaka.
 
No 6 For MeπŸ˜€
Watoto miyeyusho sana. Kuna mmoja niko nae ofisini juzi boss kamkuta anacheka na tiktok. Usiniulize yaliyofuataπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Kabisa mkuu! Na sisi tunasumbuka sana sababu ni kizazi cha transistion kutoka analogia kwenda digitali.

Tumezaliwa enzi mtu mwenye TV anaheshimika mtaani, sasa hivi kuna TV mpaka kwenye bajaj.

Enzi zetu mtu akinunuliwa "Brick Game" anafeli mitihani yake yote, sasa hivi watoto wana PS5 na games za kutosha kwenye simu.

Level ya distraction wanayopitia ni kubwa mno. Yaani ukiwaangalia kwa jicho la pili, utawaonea huruma.

Fikiria wamekuwa na internet viganjani mwao, social media zimewazunguka kila kona. Movies on demand, enzi zetu mzee anafungia deki mpaka siku kuu. Wao wanajiachia tu. Music videos ndio usiseme. Yaani ni vurugu sana.
 
Angel Nylon piti hapa ucheke...
Hivyo vitoto vya GenZ ndio vyetu tunavyo na tunatamba navyo na sisi ndio wazazi wao. Hata sisi wazee wetu walitulia tofauti na walivyolelewa wao. Zama zinabadilika. Kama yanavyobadika mambo mengine tunayoyafurahia na malezi nayo pia yamebadilika. Kumlea mtoto zama hizi kama tulivyolelewa sisi zama zetu ni ngumu kama ugumu wa ngamia kupenya kwenye tundu ya sindano..tutabaki na nadharia tu lkn implementation 0.
 
Umesoma mpaka mwisho lakini?
 
No 6 For MeπŸ˜€
Watoto miyeyusho sana. Kuna mmoja niko nae ofisini juzi boss kamkuta anacheka na tiktok. Usiniulize yaliyofuataπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Madogo wanaishi bila kanuni za msingi za kibinadamu.
 
Dah umenena ukweli mzee. Kunavigate malezi nyakati hizi inataka ufundi na utulivu sana. Ila tupambane tu hakuna namna.
 
Vina penda kuangalia Move kutwa nzima na Usiku kuchaa
 
Misingi ya familia tu, kaka na baba zao si ndio sisi. sasa watamuiga nani? Tatizo linaanzia nyuma then mazingira ya sasa yanavyoenda. Kuna mdau kagusia distractions mbalimbali hususan katika masual kama teknolojia, habari n.k

Vinatingwa sana kwa kweli, twende nao taratibu. Na kwa upande mwingine ni vijanja bana, tusiwalaumu sana. Sasa utawaambia wasome kitabu wakati hata mitaani ndra kuona watu wanajisomea, wanaona watu wana miaka 40 50 wanaongelea mademu, club,Simba na Yanga yeye atawazaje kusoma katiba?
 
Sisi Gen Y wa kuzaliwa 1990's na kuendelea, Gen X wa miaka ya 70 kurudi nyuma, nao wanatuona sisi hatuna adabu, Generation itatofuata miaka 20 mbele ndo itakuwa hatari, watatembea uchi barabarani mchana, watoto wa 2000 wataonekana wana nafuu.
 
Kizazi cha baba zao ndo kimelifikisha taifa hapa lilipo. Wizi, utapeli, tamaa, ujanja ujanja, udanganyifu nk. Hivi kweli angalia calibre ya viongozi tulio nao, unaanzia wapi kutuaminisha Gen Z ni wakorofi? Hata hii ya juzi 2910 ni uthubutu wa Gen Z. Wengine tulishakubali ujangili wa hawa matapeli, tunaowaita watawala.

Mimi naamini uthubutu wa Gen Z utalikomboa taifa kuliko hawa wazee matapeli.

TZ na Africa tulipofika, status quo is not an option.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…