Leo ni 10 10 Tesla Event: We Robot!

Leo ni 10 10 Tesla Event: We Robot!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Baada ya kimya na ahadi za muda mrefu za CEO wa Tesla, Elon Musk, finally ile siku imewadia.
IMG_0371.jpeg

Ni tarehe 10 October, ambapo billionaire uyo atafanya uzinduzi wa huduma na bidhaa mbalimbali kutoka kwenye kampuni yake ya Tesla.

Event ina tittle “We Robot” ambayo tunaamini kaitoa kwenye series ya vitabu vya Isaac Asimov vya I, Robot wazee wa Movies, ya Will Smith I Robot.

Baadhi ya vitu ambavyo tunaweza kuvitegemea kutoka kwenye hii event ni:

1. Robotaxi (Cybercab)
IMG_0372.jpeg

Ulimwengu wa ku-request gari, linakuja bila dereva umefika. Utake usitake.

Robotaxi ndio event kuu leo, ambapo Tesla wanazindua huduma ya ride sharing (kama Uber) lakini ni autonomous vehicles.

Utaita gari, linakuja, halina dereva wala steering, unapanda mnaenda unakatwa online malipo.

2. Optimus hummanoid
IMG_0374.jpeg

Kwa muda mrefu Tesla wamekua wakitumia AI robots (Optimus) katika kazi mbalimbali za viwandani kwao.

Sasa ni muda wa kuziweka public. Tutaanza kupewa uwezo wa kununua AI robots na kuziajiri katika kazi za kila siku.

Tusubiri baadae.

3. Tesla semi-truck
IMG_0375.jpeg

Tesla trucka bado hazikua officially announced ingawa baadhi ya makampuni mfano Pepsi wameonekana wakizitumia.
IMG_0376.jpeg

Tunaamini leo ni siku ya kwenda officially.

4. Tesla Model 2
IMG_0377.jpeg

Kuna uwezekano mkubwa sana leo tukaletewa cheapest Tesla kuwahi kutokea duniani. Tesla Model 2.

Hadi leo katika Tesla zote (S 3 X Y Truck), Model 3 ndio cheapest kwa kuuzwa karibia $40,000 ila sasa tutaletewa Model 2 itakayouzwa $25,000.


5. Tesla Roadster 2.0
IMG_0373.jpeg

Yes, Elon alishasema sana kwamba second generation ya Roadster inakuja. Nadhani the wait is over.

Ikumbukwe Roadster first generation moja wapo ipo mwezini, Elon aliituma iende uko.

6. Tesla Mode Y Juniper
IMG_0378.jpeg

Ingawa Elon amekataa kwamba hakuna new refreshed Model Y (Juniper) lakini alisema kwamba hizi rumors zina haribu sales za current Model Y. Kwamba watu hawataki kununua hii Model Y iliopo wakisema wanasibiria refreshed Juniper.

Event itakua live twiter kuna link katika account ya Tesla, sema kidogo muda ni m’baya!
 
Aisee, naomba niulize tu, hivi hadi sasa kwenye nchi kama marekani huduma za hizo autonomuos vehicles zinapatikana kiurahisi? Au ni kama tu tiba za ukimwi zinazotangazwa so often ila kiuhalisia hazipatikani?
 
Aisee, naomba niulize tu, hivi hadi sasa kwenye nchi kama marekani huduma za hizo autonomuos vehicles zinapatikana kiurahisi? Au ni kama tu tiba za ukimwi zinazotangazwa so often ila kiuhalisia hazipatikani?
Nilichelewa kukujibu.

Hapa kuna smissue mbili, ya kwanza FSD na ya pili Robotaxi.

Full Self Driving gari inakua inajiendesha ila under supervision kwahiyo kuna steering wheel na pedal za breki na mafuta.

Magari mengi yanayo, na FSD ni aina mojawapo ya ADAS Advanced Driving Assistance System.

ADAS ni system inayokusaidia dereva katika kuendesha mfano gari kujipiga breki ikitaka kugonga kitu, kujiweka katikati ya barabara, kujiendesha katika speed flani nk.

ADAS ina level 5, kuanzia simple Level I hadi Level 5.

FSD ni level 3 na 4. Magari ya Tesla sahivi yana Level 3 ambayo unailipia kwa mwezi au unaweza nunua full package (ila lazima gari lako liwe lina support FSD, ambayo ni Tesla nyingi za kuanzia 2020).

Sasa tukija ya pili, Robotaxi hii ni level 5 ya ADAS kwani dereva sio lazima akae kwenye kiti au kama Tesla wao gari yao haina steering wala haina pedal.

Kwa USA, Waymo ambayo ni tawi la zamani la Google, wanayo Robotaxi na inafanya kazi kitambo sana. China pia Baidu wanayo kitambo.
 
Back
Top Bottom