Leo ni kumbukizi ya miaka 11 ya shambulio kali la kimtandao dhidi ya JF, CCM maji yalikuwa shingoni

Leo ni kumbukizi ya miaka 11 ya shambulio kali la kimtandao dhidi ya JF, CCM maji yalikuwa shingoni

Dr Matola PhD

Platinum Member
Joined
Oct 18, 2010
Posts
62,453
Reaction score
111,795
JamiiForums Message
Tumerejea: Tupo imara zaidi!

Wakuu,
Tunafarijika kuwafahamisha kuwa tumerejea hewani baada ya kupata mashambulizi ya makusudi yenye kulenga kuzuia upatikanaji wa huduma kwa watumiaji wa JamiiForums (DDOS Attack) kwa takribani masaa 7, kuanzia saa 7 mchana hadi saa 2 usiku.

Mashambulizi haya yaliyolenga kuidhoofisha miundombinu yetu, yamefanywa kwa kupangwa na kwa kiwango tulichobaini kuwa yalifanywa na wataalamu waliobobea katika masuala ya mashambulizi ya kimtandao.

Tunalaani kwa nguvu zetu zote kitendo hiki na vingine vya mwelekeo kama huu vyenye kulenga kunyamazisha sauti za wananchi.

Timu yetu ya wataalamu itaendelea kufanya kazi kwa umakini zaidi katika kipindi hiki cha Uchaguzi na tunaomba ushirikiano wa wanachama na wadau wa JamiiForums pale mtakapoona huduma zetu zinasuasua kwa namna yoyote ile katika upatikanaji. Wasiliana nasi kupitia [email protected]

Tunawashukuru sana kwa uvumilivu wenu katika kipindi hiki na tunawatakia kila la heri katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu.

Uongozi,
JamiiForums

Pia soma: Baada ya mashambulizi: Tumerejea hewani, Tupo imara zaidi!
 
Kipindi hicho uzi ukipanda unapanda na pdf za kutosha....
 
Back
Top Bottom