Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Miaka 20 ilopita, Marekani na washirika wake akiwemo Uingereza waliivamia nchi ya Iraq baada ya kushindwa kulishawishi baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Marekani na Uingereza walishindwa kulishawishi baraza la usalama la umoja wa mataifa kuweka azimio au "resolution" la kuwawezesha kuwa na sababu za kisheria za kuivamia Iraq na kisha kumng'oa kiongozi wake alie madarakani Saddam Hussein na kisha kuhalalisha mauaji yake.
Raisi wa Marekani wa wakati huo George Bush na waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair walihangaika na umoja wa mataifa ulokuwa ukiongozwa na katibu mkuu Kofi Annan kutafuta sababu za kuivamia Iraq. Viongozi hao wakaja na madai kwamba Saddam Hussein alikuwa amehifadhi silaha za maangamizi.
Aliekuwa waziri wa ulinzi wa Marekani wakati huo merehemu Collin Powell aliwasilisha Umoja wa Mataifa taarifa ndefu na ya kina iloshiba ujasusi wa picha za satelite na vielelezo vingine kutaka kuthibitisha kuwa Saddam Hussein alikuwa ana silaha za maangamizi.
Wanachama wengi wa Umoja wa Mataifa hawakukubaliana na hali hiyo ikiwemo Ufaransa na waziri wake wa mambo ya nje bwana Dominique de Villepin alikuwa akiongoza upingamizi huo. Le Villepin aliungana na nchi za Ujerumani, Russia, Belgium na China kupinga uvamizi huo wa Iraq na pia kupinga azimio jingine lilotaka kupinga matumizi ya nguvu dhidi ya Saddam Hussein.
Lakini bado George Bush na Tony Blair walikuwa wakizidisha nguvu katika hoja zao kubwa tatu kwanza, kuondoa silaha za maangamizi walodai alikuwa nazo na pili, kumzuia Sadam Hussein kusaidia shughuli za kigaidi na tatu kuwaondoa wairaq katika shida ya utawala wa Sadam Hussein na kuwa huru.
Itakumbukuwa mwaka 2002, Hans Blix aliekuwa akiongoza tume ya umoja wa mataifa ilokuwa ikisimamia na kuchunguza na kisha kuthibitisha uhalali wa matumizi ya nyuklia chini ya IAEA, alitumwa kuchunguza silaha za maangamizi nchini Iraq.
Blix akaja na taarifa ambayo ilisema tume yake hawakukuta silaha zozote za maangamizi ambazo zilikuwa zimetengenezwa na na kuhifanyiwa na Iraq. Tarehe 17 March 2003 raisi Bush akatangaza Marekani kuivamia Iraq ndani ya masaa 48 na kumtaka Blix aondoke nchini Iraq na Saddam Hussein pia aondoke mwenyewe nchi humo.
Tarehe 19 March 2003 uvamizi ukaanza kwa mashambulizi ya angani na kuweka NFZ (No Fly Zone) baada ya kuua nguvu yote ya jeshi la anga la Iraq na tarehe 20 March 2003 majeshi ya Marekani yakaingia nchini humo yakishirikiana na majeshi ya Poland, Uingereza na Australia. Majeshi ya wakurdi wa kaskazini mwa Iraq wanojulikana kama Peshmerga nao walikuwa wakitoa msaada wa kimkakati.
Baadae mwaka 2004 Kofi Annn akaita uvamizi huo ni kinyume cha sheria za kimataifa na ulivunja kanuni za umoja huo yaani "UN charter". Kulikuwepo maandamano katika baadhi ya nchi kupinga uvamizi huo katika nchi za Ufaransa na Uingereza waandamanaji waliita maandamano hayo Stop The War.
Miaka 20 imepita Iraq imo kwenye matatizo makubwa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, uhalifu ulopitiliza na mauaji yasoeleweka. Vikundi kama ISIS, Al-Qaeda vilishamiri chini ya uongozi wa Al Zaqawi ambae aliwasumbua sana majeshi ya uvamizi kwa mbinu zake za vita iloitwa "Urban Warfare" na "Asymmetrical Warfare". Ni vita zilokuwa mtaa kwa mtaa na pia utegaji mabomu katika njia ambazo majeshi ya uvamizi yalikuwa yakipita ama kwa miguu au kwa magari ya kivita.
Baada ya vita hivyo kumalizika Marekani na washirika wake hawakuwa na jinsi ya kudhibiti hali ya vurugu ilijitokeza nchini Iraq, hali ilosababisha kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe hivyo wakurdi, wasuni na washia wote wakawa maadui na wanapiagana na kuuana hovyo.
Lakini jambo la msingi la kukumbuka ni kwamba Marekani na nchi za NATO ikiwemo Uingereza wanafanya mambo yao kwa akili sana ingawa nchi nyingi za dunia ya tatu zikiongozwa na Urusi na China ambazo ziliona uvamizi ule wa Iraq ulofanywa na Marekani na washirika wake.
Hiyo ndo sababu nchi kama Afrika Kusini na zingine zilikuwa nchini Russia katika mkutano wa pamoja katika kuidhinisha ushirikiano wa kibiashara baina ya nchi za Afrika na Russia. Nchini Chad kundi la Wagner limejikita katika kurahisisha shughuli za Urusi nchini humo. Wenyewe wananchi wa Chad wamewekewa mabango yenye maneno kama "Be Afrika Mamboko na Mamboko na Russie". Yaani yakimaanisha kwa kiswahili kuwa Afrika Mkono kwa mkono na Urusi.
Afrika Kusini hivi mapema mwezi huu walifanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi na majeshi ya China na Russia wakitumia pwani ya bahari ya Afrika Kusini. Nchi 30 za Afrika zimekemea uvamizi wa Russia nchini Ukraine na nchi 22 hazijafanya hivyo. Waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Lavrov tayari mwaka huu ametembelea nchi zaidi ya 7 akitumia mgogoro wa Ukraine kusafisha njia kwa vikozi vya jeshi la kukodi la Wagner kupewa nafasi ya ulinzi wa rasilimali za nchi hizo dhidi ya uvamizi wa magaidi wakisaidiwa na majeshi ya kigeni kutoka Ufaransa.
Akizungumzia mkutano wa viongozi wa Afrika na Russia ulofanyika leo raisi Putin amesema uhusiano wa Afrika na Russia wapewa kipaumbele kwa uzito wake. Raisi Putin amesema nchi yake imedhamiria kuhakikisha inajenga ushirikiano wa kimkakati baina yake na marafiki wa Afrika na kwamba Russia na Afrika zipo tayari kubadili ajenda ya kidunia kwa pamoja.
Putin anaamini kuwa Afrika kama Russia wanalinda maadili ya asili (traditional moral values) na kupinga mawazo ya kikoloni mamboleo yanopenyezwa kutoka nje.
Juhudi za Urusi kuhakikisha anapata washirika wengi katika kumsadia kupunguza nguvu ya Marekani na nchi za NATO yaelekea kuzaa matunda kwani tayari nchi za Iran, Korea Kaskazini na Venezuela zashirikiana na Russia katika nyanja mbalimbali kukiwemo Iran kuiuzia silaha Urusi aina ya AUV ndege zisizo na rubani. Venezuela pia yashirikiana na Russia kiuchumi kwa kupokea watalii wa Russia wanokwenda katika kisiwa chake kiitwacho Isla Margarita. Ndege za Urusi (Norwind Airlines) zaruka moja kwa moja kutoka Moscow kwenda Caracas na raisi Maduro wa Venezuela amesaini mkataba na Russia kuchukua watalii hao.
Watalii wa Russia wana nafasi ya kutembelea vivutio kadhaa kama maporomoko ya maji ya Salto Angel yaliyomo katika mbuga ya Canaima. Pia kuna kisiwa kiitwacho Coche, sehemu iitwayo Nueva Esparta na mji wa Caracas wenyewe.
Russia imepanga mkutano mwingine mkubwa wa siku tatu nchini unoitwa Russia Africa Summit ambao utafanyika mwezi Julai kuanzia tarehe 26 hadi 29 mjini St Petersburg. Raisi Putin mwenyewe amesisitiza umuhimu wa mkutano huo na amewaalika viongozi karibu wote wa Afrika.
Mkutano wa kwanza mkubwa kabisa kufanywa kati ya Russia na Afrika ulikuwa mwaka 2019 ambao ulihudhuriwa na nchi zipatazo 54 wakiwemo maraisi 43.
Kitendo cha Russia kuivamia Ukraine kimepaliliwa na Marekani na NATO wenyewe kwa tamaa yao ya ubepari ulokithiri. Akiandika katika kitabu chake cha " Imperialism the Highest Stage of Capitalism" mwaka 1916 na kuchapishwa mwaka 1917, Vladmir Lenin ameongelea kitu kiitwacho "Exploitation Colonialism". Hii ni hali ya kuutumia ukoloni kwa kupanua eneo la kibepari na kuleta maendeleo yasiyowiana na mifumo ya kiuchumi ambayo husababisha sehemu (nchi) moja kuwa na nguvu na hivyo kuzitawala sehemu (nchi) zingine.
Urusi ana rasilimali nyingi na zote zipo eneo la mashariki kujumuisha Donbas yote. Marekani anahitaji rasilimali hizo kwa kutumika kwenye viwanda vyake vya vyuma, magari na kila aina ya bidhaa zilizopo dukani. Urusi anakataa hiyo na kufanya kuwepo na mvutano mwingine wa vita baridi.
Rasilimali hizo ni pamoja na madini ya Nickel, Lithium, Dhahabu, gesi asilia na zinigne lukuki.
Je, Marekani na washirika wake wa NATO wataweza kazi ya kuivunja Russia taifa kubwa lenye watu milioni 142, silaha za nyuklia na kiti cha kudumu baraza la usalama la umoja wa mataifa, iwe vipande na iwe nchi isojielewa?