Mkuu ahsante kwa bandiko zuri la kufikirisha, kizuri zaidi umeeleza jinsi ambavyo mtu anawezakuwa na matatizo ya afya ya akili (kichaa) na asiokote makopo, akawa anaonekana mtanashati na bado isimuondoe kwenye kundi la vichaa.
Lakini napingana na wewe kwa kutumia hoja ya chanjo kama kigezo cha ukichaa na afya bora ya akili.
Ni sawa na kusema kati ya hizi timu mbili Simba na Yanga, ukiwa Yanga au Simba afya ya akili yako ina mushkeli.
Au kutumia dini ( madhehebu) kwamva ukiwa mkristo au muislam akili ina tatizo.
Ukitumia kigezo cha chanjo inakua umejibana kwenye eneo dogo sana lusilotosheleza kuhitimisha uzima au upungufu wa afya ya akili.
Hapo tutazalisha swali lingine, mtu anaweza kuwa na ukichaa kwenye suala la chanjo pekee na akawa genious mambo mengine?
Huo ukichaa una maeneo au afya ya akili inapokua mbovu inasthiri maamuzi na mambo yote anayofanya mtu?
Mwingine anaweza kyamua kigezo cha ajira kwamba ni ukichaa, kwamva kutokuajiriwa inaonyesha matumizi ya akili na kuajiriwa ni ukichaa.
Hali kadhalika mwingine ataenda mvali zaidi kwamba kujenga au kutokujenga inafanya wahusika kuwa kwenye kundi la ukichaa au akili yenye afya.
Ni hadi pale utakapomsikiliza kila mmoja atoe sababu zake kwanini yeye anapendelea kuajiriwa au kutokuajiriwa, maelezo yake yatafanya uone kama yana mantiki au la.
Kwa muktadha wa bandiko lako, mtu mwenye tatizo la akili akienda kuchanjwa anaodoka kwenye hilo kundi kisha amechanjwa?
Kuna mtu ukimuuliza kati ya kuishi na kufa bora nini, atakwambia kwa hali yake angetamani afe jana, ukipata kumsikiliza unaweza kujikuta unaenda kumnunulua sumu kwamba yuko sahihi.
Binafsi nakubali watu wengi sana wana matatizo ya akili sema madhara ndio yanatofautiana kiwango.
Ukiongeza na haya mambo ya tozo, utafiti ukirudiwa unaweza kukuta wenye shida ya akili wameongezeka.
Kutumia kigezo cha chanjo ya corona kupima afya ya akili inaweza isitoe picha halisi ya tatizo.