Leo ni Siku ya Bia duniani

Leo ni Siku ya Bia duniani

Kinyungu

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2008
Posts
19,484
Reaction score
38,416
Wakuu leo August 5 ni siku ya Bia duniani.
Siku hii husherekewa kila mwaka siku kama ya leo

Sisi tunaopenda kujiburudisha na kinywaji hiki adhimu ambacho kusema kweli hata Wamisri wa kale enzi za Mapharao waliamini bia ni zawadi toka kwa mungu tusiache kupita zile sehemu zetu za kujiburudisha siku ya leo ili kuenzi kinywaji chetu pendwa hasa ukitilia maanani leo weekend inaanza.....

istockphoto-933421992-612x612.jpg

---
Wakati ulimwengu ukiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Bia leo, wataalamu wameeleza kinywaji hicho kinapewa umuhimu kwa sababu ya kuwaunganisha watu katika jamii, hasa maeneo yenye changamoto za kiusalama.

Siku hiyo huadhimishwa kila Ijumaa ya kwanza ya Agosti na lengo lake ni kufurahia kinywaji hicho.

Bia ni kinywaji kinachopendwa na wengi na kina historia ndefu katika jamii tofauti na wamekuwa wakitumia kinywaji hicho kukaa pamoja na kujadiliana masuala mbalimbali au kufurahi pamoja katika matukio ya kijamii.

Ushahidi wa kale unaonyesha kwamba binadamu alianza kutengeneza bia katika miji ya Babylonia na Misopotania. Wataalamu wa historia wanabainisha kwamba viungo vya bia viliandikwa mwaka 4300 K.K.

Hata hivyo, siku hiyo ilianzia huko California, Agosti 2007 kabla ya kusambaa maeneo mengine duniani na malengo makuu yalikuwa ni kukusanyika na marafiki na kufurahia ladha ya bia, kusherehekea wanaotengeneza na kuhudumia bia na kuunganisha ulimwengu wote kupitia bia.

Akizungumza na Mwananchi jana kuhusu siku hiyo, Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia, Innocent Shoo alisema siku ya bia duniani ilianzishwa kutokana na umuhimu wa kinywaji hicho katika kuwakutanisha watu wakakaa na kuzungumza.

Advertisement
“Umuhimu wa bia kama kinywaji ndiyo umefanya kuwe na siku ya kimataifa ya bia. Sasa watu wanapokaa pamoja wanaongea, inawakumbusha kwamba bia inaondoa msongo. “Dunia ina mambo mengi ya stress kama vita, ndiyo maana nchi zote zenye vita unakuta viwanda vya bia vipo, kama havipo lazima wataleta bia kwenye hiyo nchi. Nimekaa Burundi, nimekaa Congo kwenye gari kuna bia, nimekaa Sudan kwenye gari kuna bia, kwa sababu ni stress,” alisema Shoo.

Shoo alibainisha kwamba bia pia inaunganisha watu kwa sababu katika diplomasia ya utamaduni, lazima kuna sherehe ndogo inafanyika na sherehe hiyo inahusisha pia unywaji wa bia.

Aliongeza kwamba siku hiyo pia inawakumbusha watu kunywa kistaarabu kwa sababu wakati mwingine imebainika kwamba watu wakilewa wanapigana, wanatukana watu na wakati mwingine kuchochea mauaji.

“Hii siku ni muhimu kwa sababu bia ni muhimu, inakutanisha watu wengi, lakini pia inawakumbusha watu kunywa kistaarabu,” alisema Shoo wakati akielezea kuhusu siku hiyo ya kimataifa.

Kwa upande wake, mnywaji wa bia, Chrispine Magoti alisema hakuwa anaijua siku ya kimataifa ya bia, hata hivyo anakiri kwamba bia imekuwa na umuhimu katika jamii kwa sababu inawaleta watu pamoja na kuwapunguzia msongo wa mawazo.

“Ukifuatilia watu wanaokunywa pombe, mara nyingi hata familia zao zina amani kwa sababu wanapuuzia mambo mengi ya maudhi kutoka kwa wake zao. Ukinywa pombe unarudi nyumbani kulala, kero zote unazipuuzia tu,” alisema.

Wakati ulimwengu ukiadhimisha siku hiyo, kampuni ya bia Tanzania (TBL) imezindua kwa mara nyingine kampeni yake ya unywaji bia salama, iliyoanza Agosti mosi hadi Agosti 5, ikiwa na nia ya kuwaelimisha wanywaji na kuwakumbusha hatua za unywaji salama wa bia.

TBL pamoja na kampuni mama ya AB InBev, wamechukua jukumu la kusaidia kupunguza matumizi hatarishi ya pombe ulimwenguni. Mwaka 2015, AB InBev ilizindua malengo ya dunia ya unywaji salama ambayo yanatarajiwa kufikiwa mwishoni mwa mwaka 2025.

Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Jose Moran alisema: “TBL inataka kuwapa wateja wake wote dondoo za unywaji salama kwa kuwa tabia ya unywaji salama imekuwa ni sehemu ya utamaduni wa TBL na AB InBev na tungependa kuiendeleza na kuileta kwenye jamii.”

“Unywaji salama ndio unatufanya tufurahie bidhaa zetu kila mara. Unywaji salama ni zaidi ya kunywa kistaarabu, kwani unaruhusu wanywaji kufurahia bia zao kwa kiwango cha juu zaidi,” aliongeza Moran.

Kwa upande wa Tanzania, TBL inalenga kuwahamasisha kuwa na tabia ya unywaji salama na kupunguza matumizi hatarishi ya pombe na vilevi.

Maadhimisho ya wiki ya unywaji salama ya mwaka huu, yamelenga kubadilisha baadhi ya tabia hatarishi za unywaji zilizozoeleka na kuhamasisha unywaji salama kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanywaji wanafurahia bia kila mara bila kupata athari.

Kupitia kampeni hiyo, TBL inahamasisha unywaji salama kwa kuhimiza wanywaji kunywa maji wakati wa kunywa bia, kula chakula wakati wa kunywa na kuita usafiri wa kurudi nyumbani mapema.

Mwananchi
---
Beer Brewing in Ancient Egypt
Picture: The Trustees of the British Museum (Copyright)
 
ukitaka niache bia...nisimulie maboko niliyotoa...kuna siku nipo harusi ya jamaa angu..sasa meza niliyopangiwa karibia meza nne zinazo nizunguka..naona kila mtu ananifaham na huwa nafanya nao bussiness...nikatoka nje nakutana na mpishi na karibia vifaa vyote vya kaz nimesupply mwenyewe..akanipa supu na chakula kabla ya ratiba ya msosi...baada ya hapo nikajongea kwenye kamati ya vinywaji..pale wana kamati walivyoniona tu..wakanishushia vyombo kama vyote...nimesimama sehemu vinywaji vinapotolewa...bwanaa nikachakaa haswa..akil ikaruka nikahisi nipo bar..nikaanza mwambia nipe bia za 15,000 huku nampq hela..wakaanza kunicheka...nikawaambia naomben k vant kubwa nimpelekee jamaa angu amekaa sehem..Mungu wee ila napewa hapo confidence kama zote ile natembea tu kutoka pale lichupa likaniponyoka pwaah... likapasuka..meza zikanigeukia..nikatimua mbio na hapo hapo nikarud home haraka na saa kumi na mbili nikaondoka kabisa mkoa...😂😂😂
 
😁😂😂 Ukumbi mzima ukanukia k vant
Mkuu yan cjui..aliyeona kaona...ambae hakubahatika ndio hivyo..na ikawa kama kasheria kila nikienda harusin kama nikikosa siti ya mwisho kabisa tna kwenye kona..basi pombe wataniletea nje ya ukumbi meza inakuwa juu ya gari ovr...
 
naunga mkono hii siku kwa kweli hata mimi namuambiaga mke wangu ningekuwa sinywi tungeshatengana siku nyingi maana huwa mambo madogo na bullshit siku ziende.
Ila nauliza sijui wapiga viroba nao siku yao ni lini.Hiyo kitu sigusi kabisa
 
Aliye sema pombe ni shetani ni mwehu kabisaa...
 
🤣🤣🤣😂😂 Mkuu hizo pombe au unazidisha inapita kiasi, duuu
Mimi huwa kama nakunywa najisemea kabisaa nataka kuchakaa...lakin sijawah kunywa na mwanamke bar..hapo nipo na jamaa zangu na kila mmoja lazima alinde usalama wa mwingine..😂😂 hutokuja kujuta maana kuna muda unaamka unaanza kumpigia mmoja baada ya mwingine caz kama k vnt ni kifutio kile..kinapoteza kumbu kumbu haswa..hutokuja kujuta bt jitahid uwe financial stable na wanao kuzunguka wawe pia atleast
 
Kwa niaba ya wasiokunywa bia mwakilishi wenu nipo hapa nasubiri siku ya wanywaji juisi worldwide
 
Back
Top Bottom