Msekwa amezungumzia historia ya vyama vingi nchini na kusisitiza ni serikali ya CCM enzi za Mzee Rukhsa aliporuhusu mfumo wa vyama hivyo, hivyo CCM inataka upinzani wa kweli ushamiri.Msekwa ameukejeli upinzani uliopo bungeni na kusema ni upinza legelege ambao hauna uwezo wa kuendesha serikali kivuli.Alifafanua lengo la serikali kivuli kwenye bunge la vyama vingi, ni pale inapotokea hoja za serikali zimeshindwa bungeni, Waziri Mkuu anajiuzulu na serikali kivuli ndio inatwaa madaraka ya kuongoza serikali, akauliza kwa serikali kivuli ilipo bungeni, kutokana na uchache wao hata uwezo wa kuunda serikali kivuli hawana.Pia alizungumzia siasa za Zanzibar na kukiri ni mgogoro, tangu uchaguzu mkuu wa 1995, Zanzibar ilikuwa mgogoro, ule wa 2000 pia ni mgogoro, wa 2005 ni mgogoro tena na ujao wa 2010, dalili za wazi zimeshaanza kujitokeza, hali inayoashiria Zanzibar haina political tolarance ya mfumo wa vyama vingi.Msekwa alimalizia kwa kutoa changamoto vyamo vyote viwahamasishe wagombea wanawake na kuwapitisha kwa wingi kwenye uchaguzi wa 2010.Baada ya hotuba ya Msekwa, ndio ukawa mwisho wa maadhimisho ambapo MC ni mtangazaji Eshe Muhidin aliyesema na yeye atagombea ubunge mwaka 2010, japo hakusema kupitia chama gani.