Leo ni siku ya Kimataifa ya Elimu

Leo ni siku ya Kimataifa ya Elimu

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Kutokana na tabia yetu ya kutoijali elimu wananchi hatujui kuwa leo ni siku ya kimataifa ya elimu, ingekuwa ni siku ya walevi tungetangaziwa, siku ya wanawake tungetangaziwa, siku ya kuondoa mkonosweta tungetangaziwa, lakini siku ya elimu, acha ipite kimyakimya!
 
UNESCO hawako "aggressive" enough!
 
Ona hata comments hakuna,aisee inasikitisha .Elimu yetu Ina mambo mengi ya hovyo ambayo wakati mwingine mtu unaweza kuhitimisha kuwa yanafanyika kwa kusudio maalumu.

Mfano,kwanini shule za kata zina majengo mabaya yaliyochoka na ambayo hayafanyiwi ukarabati?
Kwanini Kila mwaka serikali inatenga fedha ya kujenga madarasa ila inasahau kutenga fedha ya kukarabati madarasa ya zamani?

Kwanini daktari analipwa posho inaitwa consultation fee(posho ya kumuona daktari),lakini mwalimu halipwi teaching allowance?

Mtu anaweza akaleta hoja kuwa hakuna fedha za kutosha kugharamia hayo kwakuwa mahitaji ni makubwa.Hii hoja kwangu haina mashiko kwakuwa inaibua maswali zaidi.Mfano,kwanini afisa mmoja kama mkuu wa mkoa anapewa gari lenye kununuliwa gharama kubwa, mengine yananunuliwa hadi milioni 500, pamoja na gharama kibao za kuyaendesha? Kwetu sisi nadhani tatizo la uduni wa elimu na miundombinu yake linatokana na mgawanyo mbaya wa rasilimali kuliko ukosefu wa fedha.
 
Back
Top Bottom