Leo ni siku ya Prof. Kigoma Ali Malima (Julai 16)

Leo ni siku ya Prof. Kigoma Ali Malima (Julai 16)

Fred Katulanda

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2011
Posts
380
Reaction score
550
Mwaka 1995 ndiyo mwaka ambapo vyama vingi vilianza nchini Tanzania, lakini ni mwaka huu ambapo mwanachama wa CCM na aliyekuwa waziri katika serikali ya awamu ya Pili alipoamua kujiondoa CCM.

Nakumbuka ilikuwa 16/7/1995 siku hii CCM walipata mtikisikiko Mkubwa na kumfanya mwalim Nyerere kudondosha chozi hadharani kwani KADA wa CCM na aliyekuwa Waziri wa Elumu wa wakati huo Profesa Kighoma Ali Malima alipotangaza uwamuzi wake wa kuihama CCM. Katika uamuzi huo Mgumu kwake na mchungu kwa CCM na Mwalim Nyerere.

Lakini maskini hakudumu kwani baada ya kujiunga na chama cha NAREA (NRA) National Reconciliation Alliance na kufanya mkutano mkubwa huko Tabora, siku chache baadaye alifariki nje ya nchi.

Maswali bado ni mengi juu ya nini kilimsibu.......,
Nini kilisababisha kifo chake.....,

Je, wewe unakumbuka nini kuhusu yeye?
 
Me nakumbuka j.kikwete na j kambarage walishrkiana kumuua
 
Kazi za Green guard hizo!!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Alikwenda na nyumba ndogo huko Ulaya na kwa bahati nzuri akakuta wahindi wake waliomsaidia kutuibia fedha zetu kutokana na misamaha ya kodi , wamekomba hela zake zote na akaunti ilikuwa na centi kumi!!! Mwizi huyu akafa kwa mshituko!!! Nyerere asingeweza kumlilia mwizi , hizo ni hadithi za kufikirika.
 
binafsi namkumbuka kama waziri aliyeandamwa sana ndani na nje ya bunge kama fisadi, mbadhirifu na mdini, haya ya ufisadi na ubadhirifu sina uhakika nayo ila la udini laweza kuwa na ukweli maana alipotoka tu CCM akajiunga na NAREA wakabadili kifupi kuwa NRA yeye akiwa mwenyekiti na Shehe Abubakar Ulotu akiwa katiba, wakaanza kupita misikitini na mikoa yenye waislamu wengi na pia wakafanikiwa kuingiza wanachama wengi sana waislamu huku bara,
 
alifanya ufisadi wa kutisha pale wizara ya fedha, alipolazimishwa kujiuzulu Jakaya Kikwete toka Msoga, alipewa nafasi ya kuwa waziri na kazi yake ya kwanza ilikua kugundua ni Kiasi gani Malima alifuja.
Uchunguzi inasemekana ulibaini maelfu ya pesa yaliibwa toka Hazina, na kupelekwa Ng'ambo....!
Alikufa wakati serikali ya Tanzania ilikuwa ikifunga akaunti zake ughaibuni, na baada ya Kighoma kugundua kuwa fedha zimekaushwa kwenye baadhi ya akaunti zake nono ndipo Hyper Blood Pressure ikachukua maisha yake.
 

Mwaka 1995 ambao pia ukiwa ndio mwaka kwa mara ya kwanza Tanzania ilifanya uchaguzi chini ya mfumo wa Vyma vingi.

Mwaka huo utakumbukwa na wengi na hasa Siku kama ya leo yaani tarehe 16/7/1995.

Siku hii ndio siku ambayo Chama cha Mapinduzi CCM kilipata mtikisikiko Mkubwa na kumfanya mwalim Nyerere kudondosha chozi hadharani.

JE NINI KILITOKEA NDANI YA CCM MPAKA MWALIM AKADONDOSHA CHOZI..?

Ni siku ambayo KADA WA CCM Na aliyekuwa Waziri wa Elumu wa wakati huo Profesa Kighoma Ali Malima alipotangaza uwamuzi wake wa kuihama CCM.

Katika uamuzi huo Mgumu kwake na mchungu kwa CCM na Mwalim Nyerere.

Prof Malima alimfuata Mwalim jioni pale Msasani na kwmwambia kwa vile ameshindwa kuipata hakii yake ndani ya CCM na ameshindwa kuleta Mabadilko basi anaenda kuyatafuta Nje ya CCM.

Mwalimu Nyerere alimbembeleza sana na kumsihi asihame kwani alitambua nguvu na ushawishi wa Prof Kighama Malima.

Prof alimgomea na kweli akaenda Tabora kutangaza kuondoka CCM, ambapo akiwa Tabora alivunja Rekodi ya mkutano wake kuhudhuriwa na wengi.

Japo mpaka leo Hakuna vyomba vya habari vimepata ujasiri wa kuliripoti hili tukio kiufasaha na ikiukweli.

HUZUNI ZAIDI KWA WANA MAGAEUZI MWKA 1995.

Baada ya kuhama CCM Prof Malima aliatangaza kuhamia NAREA (NRA) National Reconsiliation Alliance.

Lakini katika mazingira yasiyo ya kawaida Profesa Malima alifariki Kabla ya Uchaguzi wa mwaka 1995.

Moja ya maneno yake kwa mwalimu ni Kuwa Prof alimlaumu Mwalim Nyerere kwa kuleta Mgawanyiko ndani ya Nchi na matabaka ya kijamii.

Na Zaidi Profesa Malima Atakumbukwa na Masikini wengi pamoja na 'Waswahili wa Pwani na Kusini'

Kwani yeye ndio alianzisha Mfumo wa kufanya mitihani kwa kutumia Namba za mtihani hali hiyo ililenga kuondoa Uoenvu Baraza la Mitihani.

Ambapo kwa wakati huo kulikithiri kuwaonea watu wa kuangalia Majina yao.

PRO MALIMA ALI KIGHOMA AMBAYE PIA NI BABA WA ADAM MALIMA.

ATAKUMBUKA KWA MENGI NA HASA MCHANGO WAKE KATIKA SAKATA LA MCHAKATO WA URAIS DODOMA 1995.

KWA HAKIKA TUTAZIENZI FIKRA NA MCHANGO WAKO PROFESA KIGOMA ALI MALIMA. (R.I.P)
 
Hili jukwaa linapaswa kuwa la watu weledi. Mleta uzi unaposema mwaka 1995 ndipo Tanzania ilipofanya uchaguzi wa kwanza, ni kuwadanganya watu, hasa watoto wetu walio shuleni na vyuoni. Pengine ungesema Uchaguzi Mkuu, hapo ingekuwa sawa. Kabla ya mwaka 1995 tayari uchaguzi wa vyama vingi ulishafanyika. Nitarejea kuperuzi kwenye kumbukumbua zangu, lakini ulikuwapo uchaguzi wa kiti cha ubunge kule Zanzibar, na CCM wakashinda. Baadaye ukawapo uchaguzi mwingine Bara, na CCM wakashinda.

Pili, hili la Mwalimu kumwaga chozi linahitaji ushahidi. Sidhani kama kweli mleta uzi alikuwapo au kaelezwa na nani. Kama Mwalimu hakumwaga chozi mwanawe wa kumzaa-Makongoro- alipoihama CCM, sidhani kama kwa Malima alimwaga chozi. Kama Mwalimu huyo huyo alikuwa tayari kuihama CCM kwa kigezo kwamba CCM si mama yake, sidhani kama alikuwa na machozi mepesi ya kumwaga kwa Malima kukihama chama hicho ambacho tayari kilishapoteza dira na mwelekeo (kwa mujibu wa H. Kolimba).

Nimeona nijaribu kuweka sawa hilo.
 
Unakumbusha ukolimba wa CCM kwa kila anayekinzana naye?.
 
Asante sana bwana Kashaga kwa kumbukizi hii, umetujuza na kutufunza. R.I.P Prof. Malima
 
Hili jukwaa
linapaswa kuwa la watu weledi. Mleta uzi unaposema mwaka 1995 ndipo
Tanzania ilipofanya uchaguzi wa kwanza, ni kuwadanganya watu, hasa
watoto wetu walio shuleni na vyuoni. Pengine ungesema Uchaguzi Mkuu,
hapo ingekuwa sawa. Kabla ya mwaka 1995 tayari uchaguzi wa vyama vingi
ulishafanyika. Nitarejea kuperuzi kwenye kumbukumbua zangu, lakini
ulikuwapo uchaguzi wa kiti cha ubunge kule Zanzibar, na CCM wakashinda.
Baadaye ukawapo uchaguzi mwingine Bara, na CCM wakashinda.

Pili, hili la Mwalimu kumwaga chozi linahitaji ushahidi. Sidhani kama
kweli mleta uzi alikuwapo au kaelezwa na nani. Kama Mwalimu hakumwaga
chozi mwanawe wa kumzaa-Makongoro- alipoihama CCM, sidhani kama kwa
Malima alimwaga chozi. Kama Mwalimu huyo huyo alikuwa tayari kuihama CCM
kwa kigezo kwamba CCM si mama yake, sidhani kama alikuwa na machozi
mepesi ya kumwaga kwa Malima kukihama chama hicho ambacho tayari
kilishapoteza dira na mwelekeo (kwa mujibu wa H. Kolimba).

Nimeona nijaribu kuweka sawa hilo.

Tatizo unakurupuka, nyie ndo wale waandishi makanjanja na vihiyo
mnaokurupuka na kuandika hata mambo ya uzushi, nimeeleza vizuri kabisa
uchaguzi chini ya mfumo wa vyama vingi ulifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1995 kama
unabisha haya
 
Hili jukwaa linapaswa kuwa la watu weledi. Mleta uzi unaposema mwaka 1995 ndipo Tanzania ilipofanya uchaguzi wa kwanza, ni kuwadanganya watu, hasa watoto wetu walio shuleni na vyuoni. Pengine ungesema Uchaguzi Mkuu, hapo ingekuwa sawa. Kabla ya mwaka 1995 tayari uchaguzi wa vyama vingi ulishafanyika. Nitarejea kuperuzi kwenye kumbukumbua zangu, lakini ulikuwapo uchaguzi wa kiti cha ubunge kule Zanzibar, na CCM wakashinda. Baadaye ukawapo uchaguzi mwingine Bara, na CCM wakashinda.

Pili, hili la Mwalimu kumwaga chozi linahitaji ushahidi. Sidhani kama kweli mleta uzi alikuwapo au kaelezwa na nani. Kama Mwalimu hakumwaga chozi mwanawe wa kumzaa-Makongoro- alipoihama CCM, sidhani kama kwa Malima alimwaga chozi. Kama Mwalimu huyo huyo alikuwa tayari kuihama CCM kwa kigezo kwamba CCM si mama yake, sidhani kama alikuwa na machozi mepesi ya kumwaga kwa Malima kukihama chama hicho ambacho tayari kilishapoteza dira na mwelekeo (kwa mujibu wa H. Kolimba).

Nimeona nijaribu kuweka sawa hilo.

mkuu ubishi ni asili yako, point hapo ni swala la kumrekebisha wala si vijembe. alimaanisha uchaguzi mkuu wa kwanza 1995
 
Tatizo unakurupuka, nyie ndo wale waandishi makanjanja na vihiyo
mnaokurupuka na kuandika hata mambo ya uzushi, nimeeleza vizuri kabisa
uchaguzi chini ya mfumo wa vyama vingi ulifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1995 kama
unabisha haya
Rudisha kule FB upuuzi wako na Sambala
 
mkuu ubishi ni asili yako,
point hapo ni swala la kumrekebisha wala si vijembe. alimaanisha
uchaguzi mkuu wa kwanza 1995

labda atuambie ni uchaguzi gani mwingine ulishirikisha vyama vingi katika nchi ya Tanzania kabla ya 1995
 
Tatizo unakurupuka, nyie ndo wale waandishi makanjanja na vihiyo mnaokurupuka na kuandika hata mambo ya uzushi, nimeeleza vizuri kabisa uchaguzi chini ya mfumo wa vyama vingi ulifanyika mwaka 1995 kama unabisha haya

Revo, huna sababu ya kurusha maneno ya kashfa na dharau. Kuwa mpole. Sote tunajifunza, tunakosoa na kukosolewa. Nimesema kwamba kabla ya mwaka 1995 kama ni uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi Tanzania, ulishafanyika kwenye ubunge na hata udiwani. Lakini kama ni UCHAGUZI MKUU, sawa; mwaka 1995 ndipo ulipofanyika wa kwanza. Huu ndiyo ukweli. Usikasirike.
 
Revo, huna sababu
ya kurusha maneno ya kashfa na dharau. Kuwa mpole. Sote tunajifunza,
tunakosoa na kukosolewa. Nimesema kwamba kabla ya mwaka 1995 kama ni
uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi Tanzania, ulishafanyika kwenye ubunge
na hata udiwani. Lakini kama ni UCHAGUZI MKUU, sawa; mwaka 1995 ndipo
ulipofanyika wa kwanza. Huu ndiyo ukweli. Usikasirike.

okey sawa, kwavile tunajifunza ebu tuambie ni mwaka gani basi uchaguzi ulifanyika na uliusisha vyama gani ili watu tujifunze! Asante
 
Bahati mbaya sana kumbukumbu imenitoka, lakini uchaguzi wa kwanza ulioshirikisha vyama vingi Tanzania (siyo Tanganyika), ulikuwa Zanzibar. CCM walishinda. najitahidi kujua lilikuwa jimbo gani. Uchaguzi wa pili mdogo ulifanyika mwaka 1994 Igunga. Ulifanyika baada ya Mbunge wa CCM, Kabeho kufariki dunia. CCM wakampitisha Rostam Aziz, na akashinda. Kwa hiyo kabla ya mwaka 1995, tayari kulishakuwapo uchaguzi wa vyama vingi mara mbili. That were the first ever multiparty by-election in Tanzania history! Najitahidi kutafuta jimbo la Zanzibar.
 
Back
Top Bottom