Leo nilimuwekea mtego mwizi kariakoo na nikafanikiwa kumkamata

Leo nilimuwekea mtego mwizi kariakoo na nikafanikiwa kumkamata

craq

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
859
Reaction score
1,866
Siku ya leo nilikuwa na mishe kidogo kariakoo hivyo nikabeba mgongoni kibegi changu nakuelekea mitaa ya msimbazi sasa nikiwa katika ile barabara ya msimbazi nikajisemea leo nataka nimkamate mwizi nikajiwekea nadhiri lazima nitampata mwizi na nikajisemea lazima atajilenga hivyo tembea yangu ilikuwa ya mitego ya kumvizia mwizi

Kwa wasiofahamu barabara ya msimbazi haswa wa mikoani katikàti kuna barabara ya mwendo kasi na pembeni kabisa barabara ya magari lakini nyembamba halafu kijibarabara cha juu ni cha watembea miguu hapo watu hutembea nyomi msongamano na kwa vile mie nimezaliwa migo migo nikajua sehemu hii na nimebeba begi lazima wazee wakupiga ndole ,kufungua mazipu watakuwepo


Mungu sio mzee mkumba bwana kuna kijamaa kikajileta na kwakuwa lengo langu lilikuwa hilo maana nilijua tu kwa vile nimebeba begi na njia hii watu hutembea resi sana lazima hawa wafungua zipu watakuwepo ,kwanza nikahisi kama zipu inataka kufunguliwa ile nataka nigeuké majamaa wajanja sana nikajisemea nisigeuke mpaka nipate target nzuri nikaendelea na safari huku macho yangu yakiangalia side mirror ,mara paap nahisi zipu inafunguka na kwa yeyote ambaye hakuwa na nia kama ya kwangu haki ya Mungu hauhisi chochote mie japo nilikuwa na adhma na nia hio lkn 50%/50% nisingegundua ile nageuka kwa spidi nimtie nguvini daah kazuga utamu sana pembeni mita kadhaa huku akitizama pembeni kama sio yeye alivalie kapelo na T-shirt nyekundu

Ñdugu zanguni hii barabara ya msimbazi naijua kitambo sana na njia hii watu huwa hawapo makini na kwa wingi ule wa watu kila mtu yupo resi sasa wenye vibegi hufunguliwa begi sana


Kwa mnaopenda kuweka vitu kwenye mabegi na kupita njia ile watch out ile njia zipu hufunguliwa sana mie nilijifunza miaka kadhaa nilimuona jamaa akifunguliwa zipu so nikibeba begi njia ile huwa nipo care sana
 
Leo nmeibiwa wallet kkoo nmekuja kushtuka sina wallet nipo dukani nataka kununua kitu
 
Mkuu pale mi wananifahamu wote maana nilicho wafanyia kamwe hawatakuja sahau. Unawafahamu wale wauza smartphone kwa 20000 ?nikisema hivyo wajanja wanawafahamu
 
Tatizo la Dar ukikamata mwizi wengine hawakusaidii. Wanaangalia kama sezon.
Utadhani wote ni wezi
 
mkuu kwa vyovyote unaonekana mshamba, yani siyo mjanja wa town, mimi nikipita kariakoo hamna kibaka atakayejaribu kunisogelea kulingana na muonekano wangu
Sio muonekano wa ushamba hata uwe mjanja baunsa ,vaa begi halafu tembea barabara ile utafuatiliwa tu wapate angle nzr ..na begi vgm kwa mtu kujua kwa resi ya njia ile

Haha mkuu unafurahisha na nakupa ushauri na muonekano wako ukivaa begi usiweke vitu kwenye kimfuko kidogo ,sababu muonekano hautakusaidia wale hawakabi wanakuchomolea
 
Kwanza ujione una bahati nzuri sana, hawa jamaa wako wengi na mmoja akiwa anakufukuzia wengine wanakuwa karibu naye, ukigundua unaibiwa ukipiga kelele wale wanakuja kukusaidia, sasa hapo kwenye kukusaidia ndipo utaijua kkoo, ila wa mwisho atakupa buku ya nauli. Ukisikia mtu anasema yeye ni mjanja hawezi kuibiwa kkoo ujue huyo ni mgeni. Polisi pamoja na kuvaa gwanda alijikuta hana cm mfukoni wamekwisha chukua [emoji45] [emoji45] [emoji45]
 
Nina video nilikuwa nawarekodi wezi maana nilipowaona tu pale Msimbazi nikajua tu ni wezi wako wawili muelekeo wao ulikuwa ni msimbazi mataa ghafla nikawaona wamegeuka wakimfuta mdada kanona amebeba pochi lake akiambaa ambaa kando kando ya barabara nikatoa simu na kuanza kurekodi nikisema leo wakikamatwa na ushahidi juu napeleka basi wakamsogolea mdada karibu kabisa mmoja ndio amevalia tshirt nyekundu basi mwendo wangu nikawa kama naweka foleni nikamsogelea mdada karibu nikamuambia dada hao nyuma yako ni wezi kisha nikasepa maana honi nyuma yangu zilikuwa nyingi...

police wanaweza kuwakamata kabisa hao jamaa na kuwapoteza au kuwatwanga kama alivyosema mkulu.
 
Sio muonekano wa ushamba hata uwe mjanja baunsa ,vaa begi halafu tembea barabara ile utafuatiliwa tu wapate angle nzr ..na begi vgm kwa mtu kujua kwa resi ya njia ile

Haha mkuu unafurahisha na nakupa ushauri na muonekano wako ukivaa begi usiweke vitu kwenye kimfuko kidogo ,sababu muonekano hautakusaidia wale hawakabi wanakuchomolea
hilo ni moja, ninaend kariakoo nivae begi la nn?
 
Wale wa mitaa ile vibaka dawa yao ni ndogo tu, ukiwa na begi yako uwe na electric gun,kiasi kwamba wakati unatembea ukiwa umeshika electric gun mkononi na kawaya kembamba ndio kimepita kwenye begi kuelekea kwenye Zipo, huyo atakaeshika lazima adondoke
 
Back
Top Bottom