Leo nimeanza siku yangu na balaa

Ila alinikera kwa kweli.
We ndo mchokozi. Umemkuta dada wa watu nje ukaleta kiherehere cha kuwahi kwenye foleni. Ningekuwa mimi ningekuzaba kibao.

Naamini nimezidi kukuharibia siku yako.

BTW nimeingia chaka... mi nlijua umeanza siku yako ya kubleed... title ya thread yako imekaa kihengahenga
 
Hapo tayari umeshamuadhibu, ataumia sana atajiuliza sana why yule jamaa? ni nani yule? ana nini yule?

Umetumia busara sana!

Sent from my iPhone 8 using JamiiForums mobile App
 
Wala hujaanza siku vibaya, tafsiri unayoijipa ndiyo unayoiishi, kwani hujui duniani kuna watu zaidi ya tirion 6 na kila mtu anamawazo yake?, hivyo hakuna ubaya kukutana na watu wanaokwenda kinyume na utaratibu/ustaarabu wako. Angalia ulivyoianza siku vizuri mno kwanza umeanzia zinakowekwa hela, harafu wa kwanza kuongea naye ni mdada ambaye kimantiki ni msaadaizi wako kwa mujibu wa maumbo ya dunia , wala hupaswi kumchukulia kiihivyo kwani inawezekana amevurugwa vibaya mno aliko toka.

Focus endelea nayako, kwani hii nayo ni siku njema iliyoumbwa na MUNGU ili wewe upige hatua nyingine mpya kwenye maisha yako.
 
Umeianza vibaya kwa kukosa kuheshimu wenzako waliofika kwenye mlango wa benki kabla yako.

Yaani wewe kwa kifupi ndio unatabia mbaya sana sana. Jirekebishe

Nimekushangaa umekuja kuiandika huku umejionyesha tabia yako ilivyo

Huyo dada alifanya vizuri, tena na wengine wangefanya hivyo pia.
 
Umeianza vibaya kwa kukosa kuheshimu wenzako waliofika kwenye mlango wa benki kabla yako.

Yaani wewe kwa kifupi ndio unatabia mbaya sana sana. Jirekebishe

Nimekushangaa umekuja kuiandika huku umejionyesha tabia yako ilivyo
Mie niliona niko kwenye haki kwa kuwa mlango ulivyofunguliwa nilienda kupanga foleni lakini yule dada alienda kaunta, pia sijawahi kuona utaratibu kuwa aliyewahi kufika kwenye jengo la benki kabla haijafunguliwa lazima awe wa kwanza kuhudumiwa. Huwa wakishaingia wateja wanapanga foleni. Ahsante kwa kucomment kwenye uzi wangu.
 
Ulifanya jambo Jema sana kukaa kimya kutoshughulika nae, ulitumia busara ukimya nalo jibu la mjinga
ni kweli Jovitha kuna wanawake washari kuanzia mtaani kwao hadi benki.
 
mkuu lkn umesema umekuta watu pale nje. kwa hiyo kufungua mlango na wewe kuwa wa kwanza kuingia haikufanyi kuwa wa kwanza kufika bank.

kwa logic hiyo kama dada yule ulimkuta pale nje alikuwa sahihi.
pole lakini
Lakini baada ya milango kufunguliwa yeye alikwenda kule kaunta, mie nikawa nimeenda kupanga foleni. hakuingia moja kwa moja kwenye foleni alianzia kwanza kule kaunta.
 
Kukaa kimya ni jibu la mjinga ameshatoka kwake amevurugwa
hahaha, wengi tunavurugwa lakini ukiwa na wenzio unasahau "mivurugo" yako. hahahahahah. Upo Shunie umepotea kidogo
 
Ukigombana na mwanamke anakufanya kama mwanamke mwenzake,vizuri kumdharau,atakuwa kanyimwa dudu na mtu wake ndio maana ana kisirani
Na mimi pia ni mwanamke sio mwanamme, hahahahahaha
 
Busara ni kipimo cha akili.umetumia akili ya busara, nakupongeza.
 
Pole sana na hongera kwa kubarikiwa hekima.

Kwakua amejibu kwa shari, haswa hapo kwenye "...umechanganyikiwa..." Mimi ningekua nisharusha ngumi.
hahaha, ukirusha ngumi si tutashitakiwa kupigana hadharani, hahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…