Leo nimeanza siku yangu na balaa

Leo nimeanza siku yangu na balaa

Wala hujaanza siku vibaya, tafsiri unayoijipa ndiyo unayoiishi, kwani hujui duniani kuna watu zaidi ya tirion 6 na kila mtu anamawazo yake?, hivyo hakuna ubaya kukutana na watu wanaokwenda kinyume na utaratibu/ustaarabu wako. Angalia ulivyoianza siku vizuri mno kwanza umeanzia zinakowekwa hela, harafu wa kwanza kuongea naye ni mdada ambaye kimantiki ni msaadaizi wako kwa mujibu wa maumbo ya dunia , wala hupaswi kumchukulia kiihivyo kwani inawezekana amevurugwa vibaya mno aliko toka.

Focus endelea nayako, kwani hii nayo ni siku njema iliyoumbwa na MUNGU ili wewe upige hatua nyingine mpya kwenye maisha yako.
Ahsante kwa nasaha zako, ila sijaelewa inakuwaje mwanamke mwenzangu awe msaidizi wangu?
 
...wanawake bhana!
..basi umesifiwa ulitumia busara umejisikia rahaaaaa!
.ila makavu yalikuingia dadeki!
 
pole sana ila ulifanya uamuzi mzuri sana,ila sorry kama nimekusoma vibaya hapo kwenye uzi wako,shida ya huyu dada ilikuwa kuangalia salio lake,kama ni hivyo mbona ni rahisi kufanya kwenye ATMs,maana ni nafuu zaidi,hizi mashine unaweza fanya deposit of cash,withdraws,bank statements,paying of differents accounts,etc etc na gahrama zake ni nafuu kuliko kwenda kwa bank teller.
 
Pole mkuu,tumia huduma za premium

Sent from my G7-L01 using JamiiForums mobile app
 
Umeianza vibaya kwa kukosa kuheshimu wenzako waliofika kwenye mlango wa benki kabla yako.

Yaani wewe kwa kifupi ndio unatabia mbaya sana sana. Jirekebishe

Nimekushangaa umekuja kuiandika huku umejionyesha tabia yako ilivyo

Huyo dada alifanya vizuri, tena na wengine wangefanya hivyo pia.
Kweli leo nimeianza siku yangu vibaya, lakini kwa kuwa nimeanza na kunyamaza ngoja na wewe nikunyamazie. Unajua mie ni mzaliwa wa Tanzania Bara sipendi ushari.
 
We ndo mchokozi. Umemkuta dada wa watu nje ukaleta kiherehere cha kuwahi kwenye foleni. Ningekuwa mimi ningekuzaba kibao.

Naamini nimezidi kukuharibia siku yako.

BTW nimeingia chaka... mi nlijua umeanza siku yako ya kubleed... title ya thread yako imekaa kihengahenga
hhaahahahhaahh, jamani sawa bwana
 
Umekosea sana huyo ni mjinga hajui kama foleni haianzii nje hivyo ulitakiwa umsaidie kumuelimisha ili kesho asije fanya tena akizani kuwa yuko sawa

Sent from my SM-G930V using JamiiForums mobile app
 
Umekosea sana huyo ni mjinga hajui kama foleni haianzii nje hivyo ulitakiwa umsaidie kumuelimisha ili kesho asije fanya tena akizani kuwa yuko sawa

Sent from my SM-G930V using JamiiForums mobile app
Jinsi alivyokuwa mshari hata sikuweza kumsemesha, kwanza mdada mwenyewe katoboa pua amevaa kidude kimening'inia kuelekea kwenye mdomo
 
Back
Top Bottom