Leo nimefukuzwa duka moja Kariakoo na mwenye duka mwenyewe kasema mimi namchunguza

Leo nimefukuzwa duka moja Kariakoo na mwenye duka mwenyewe kasema mimi namchunguza

Kariakooking1978

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2023
Posts
549
Reaction score
1,078
Hellow members,leo jioni angu haijawa powa sana baada ya kufukuzwa na mwanamama mmoja mmiliki wa duka la viungo pale kariakoo akidai kuwa mimi namchunguza.

Ilikuwa hivi mida ya saa saba mchana leo kuna mteja wangu mmoja hivi kutoka mkoa x kanipigia kuwa anataka viungo vifuatavyo kwa bei ya jumla (zabibu kavu,mdarasini wa india,corriander seeds, fennel, uwatu, kungumanga na star anise),Sasa toka nianze kuagiza mizigo kutoka kariakoo kwenda mkoani sikuwahi agizwa bidhaa za namna hii hivo ikanilazimu kuingia chimbo kutafuta.

Baada ya kuzunguka sana kule sokoni kariakoo nikawa napishana na wale wauzaji wa reja reja wa kwenye vimeza kila nikiwauliza wapi wanachukua mzigo wakawa wanakaza hadi mzee mmoja wa makamo alipoamua kunielekeza duka la bei ya jumla.

Baada ya kuelekezwa duka husika nikafanikiwa kufika na kweli kwa muonekano wa pale nje nikajihakikishia hapa wanauza kwa bei ya jumla kwani nilikuta kuna bidhaa zipo kwenye maroba makubwa pia kuna mizani na mifuko mikubwa mikubwa tu sio kama kule nje.

Basi nikaanza na duka la kwanza nilimkuta mama hivi kakaa nje,nikamsalimu baada ya salamu nikamuuliza kama naweza kupata hizi bidhaa huku nikumuonyesha majina ya hizo bidhaa kutoka kwenye simu.

Yule mama akajibu ingia ndani kwa hao vijana mimi sioni bhana, nikaingia ndani nikakuta washikaji wawili wanachezea simu nikawauliza vipi hizi bidhaa kwa bei ya jumla unauzaje. Mshikaji mmoja akaanza kunitajia,alinitajia zabibu kavu,mdarasini na kungumanga gafla yule mama akamkatisha wewe mteja unanunua au unauliza bei au umekuja kunichunguza.

Mimi nikamjibu hapana nauliza bei namtumia boss wangu apa ananitumia hela sasa hivi natoa hapo nachukua mzigo mama.Yule mama akaanza kuwaka toka dukani kwangu na wewe x( yule kijana wa dukani) fanya mambo mengine achana na huyo mteja.

Yule jamaa akajaribu kunitetea wapi yule mama akakaza nitoke kwamba mimi namchunguza ila sio mnunuzi.
Basi na mimi nikaona isiwe kesi nikasogea duka la mbele ake ambapo nilikuta wateja wawili wanahudumiwa,baada ya wale wateja wawili nikamueleza shida yangu yule muuzaji.Akanisikiliza na akanipa ushirikiano mzuri sana,na mimi bila kuchelewa nikampa feedback boss akatuma kibunda nikatoa chapu nikachukua mzigo.

Yule muuza duka niliponunua mzigo alinisaidia na box kabisa la kuwekea nikaufunga vizuri pale coz ulikuwa mkubwa nikatoka kuwaita washikaji wale wa vitolori wakabeba uku tukipita nao mbele wa yule mama mwenye gubu.

Wakati napita na mzigo mbele yake nilimuona anashusha miwani akanitazama akavaa tena miwani nadhani amejifunza kitu leo maana kamzigo nilikonunua sio haba kwa ile jioni.

Anyway ndo changamoto za kazi yangu.Lakini sijakata tamaa naendelea na kazi yangu kama ifuatavyo:

NANUNUA,NAFUNGA NA KUSAFIRISHA BIDHAA KUTOKA KARIAKOO KWENDA MIKOA YOTE TANZANIA NA NCHI JIRANI.

HUDUMA ZA ZIADA
📌Nafuata,nafunga na kusafirisha bidhaa iliyokwisha kununuliwa Kariakoo kupitia mitandao kama fb na insta.
📌Nafanya ukaguzi na kuhakiki ubora wa bidhaa uliyonunua kariakoo kupitia mitandao kama fb na insta.
📌Nafanya malipo ya bidhaa uliyonunua kariakoo kupitia mitandao kama fb na insta baada ya kuhakiki na kukagua ubora wa bidhaa.
📌Nakusanya bidhaa,nazifunga kwa pamoja kisha nasafirisha kama mzigo mmoja kutoka kariakoo kwenda mikoa yote Tanzania na nchi jirani.

SIMU:0745645035 (PIGA/SMS/WHATSAPP)

"HUDUMA ZA HARAKA NA KUAMINIKA"
 
Kwanza kbl cjasoma maelezo yko mkuu embu nikupe pole kwa yaliyokukuta (kutimuliwa mbio)[emoji23]
Yani nimesoma tu kichwa cha HABARI nimecheka kwa sauti ndugu yng, shukraan sn
An acha tu so powa,kutafuta kuna mambo mengi sana.
 
Hellow members,leo jioni angu haijawa powa sana baada ya kufukuzwa na mwanamama mmoja mmiliki wa duka la viungo pale kariakoo akidai kuwa mimi namchunguza.

Ilikuwa hivi mida ya saa saba mchana leo kuna mteja wangu mmoja hivi kutoka mkoa x kanipigia kuwa anataka viungo vifuatavyo kwa bei ya jumla (zabibu kavu,mdarasini wa india,corriander seeds, fennel, uwatu, kungumanga na star anise),Sasa toka nianze kuagiza mizigo kutoka kariakoo kwenda mkoani sikuwahi agizwa bidhaa za namna hii hivo ikanilazimu kuingia chimbo kutafuta.

Baada ya kuzunguka sana kule sokoni kariakoo nikawa napishana na wale wauzaji wa reja reja wa kwenye vimeza kila nikiwauliza wapi wanachukua mzigo wakawa wanakaza hadi mzee mmoja wa makamo alipoamua kunielekeza duka la bei ya jumla.

Baada ya kuelekezwa duka husika nikafanikiwa kufika na kweli kwa muonekano wa pale nje nikajihakikishia hapa wanauza kwa bei ya jumla kwani nilikuta kuna bidhaa zipo kwenye maroba makubwa pia kuna mizani na mifuko mikubwa mikubwa tu sio kama kule nje.

Basi nikaanza na duka la kwanza nilimkuta mama hivi kakaa nje,nikamsalimu baada ya salamu nikamuuliza kama naweza kupata hizi bidhaa huku nikumuonyesha majina ya hizo bidhaa kutoka kwenye simu.

Yule mama akajibu ingia ndani kwa hao vijana mimi sioni bhana, nikaingia ndani nikakuta washikaji wawili wanachezea simu nikawauliza vipi hizi bidhaa kwa bei ya jumla unauzaje. Mshikaji mmoja akaanza kunitajia,alinitajia zabibu kavu,mdarasini na kungumanga gafla yule mama akamkatisha wewe mteja unanunua au unauliza bei au umekuja kunichunguza.

Mimi nikamjibu hapana nauliza bei namtumia boss wangu apa ananitumia hela sasa hivi natoa hapo nachukua mzigo mama.Yule mama akaanza kuwaka toka dukani kwangu na wewe x( yule kijana wa dukani) fanya mambo mengine achana na huyo mteja.

Yule jamaa akajaribu kunitetea wapi yule mama akakaza nitoke kwamba mimi namchunguza ila sio mnunuzi.
Basi na mimi nikaona isiwe kesi nikasogea duka la mbele ake ambapo nilikuta wateja wawili wanahudumiwa,baada ya wale wateja wawili nikamueleza shida yangu yule muuzaji.Akanisikiliza na akanipa ushirikiano mzuri sana,na mimi bila kuchelewa nikampa feedback boss akatuma kibunda nikatoa chapu nikachukua mzigo.

Yule muuza duka niliponunua mzigo alinisaidia na box kabisa la kuwekea nikaufunga vizuri pale coz ulikuwa mkubwa nikatoka kuwaita washikaji wale wa vitolori wakabeba uku tukipita nao mbele wa yule mama mwenye gubu.

Wakati napita na mzigo mbele yake nilimuona anashusha miwani akanitazama akavaa tena miwani nadhani amejifunza kitu leo maana kamzigo nilikonunua sio haba kwa ile jioni.

WAFANYABIASHARA ACHENI DHARAU KWA WATEJA
Any way kwa faida ya wote,bidhaa nilizoagizwa leo zilikuwa hizo apo chini nakuwekea na bei yake ya jumla kama na wewe ukihitaji.

1. Zababu kavu- 12000/= kilo moja
2. Mdarasini wa india wa unga -12000/= kilo moja
3. Mdarasini wa india wa mbegu-12000/= kilo moja
4. Fennel=12000/= kilo moja
5. Corriender seeds=10000/= kilo moja.
6. Uwatu= 10000/= kilo moja
7. Kungumanga=40000/= kilo moja
8. Star anise= 48000/= kilo moja.

Pia nawakaribisha kuendelea kupata huduma zifuatazo:

Nakununulia,nakufungia na kukusafirishia bidhaa kutoka kariakoo kwenda mitaa yote ndani ya Dar es salaam na mikoa yote Tanzania.Huduma hii unaipata kwa tsh 10000/= tu.

Nakutafutia bidhaa pamoja na bei zake za jumla na reja reja ndani ya soko la kariakoo.Huduma hii unaipata kwa tsh 2000/= tu.

Nakutafutia basi au lori zuri pamoja na gharama zao kwaajili ya kusafirisha bidhaa zako kutoka kariakoo kwenda mikoa yote Tanzania kwa uharaka na usalama zaidi.Huduma hii unaipata kwa tsh 5000/= tu.

AGIZA BIDHAA KAMA:
  • Simu aina zote
  • vifaa vya simu aina zote mfano: chaji,covers,protectors.
  • Vifaa vyote vya kieletronic kama TV,SABUFA,SPEAKER,FRIJI,HEATER nk
  • Vyombo vya ndani aina zote
  • Nguo za kiume za watu wazima aina zote
  • Nguo za kike za watu wazima aina zote
  • Nguo za watoto aina zote
  • Nguo za ndani aina zote mfano chupi,sidiria,boksa nk
  • Urembo aina zote kama heleni,bangiri,kacha,saa nk
  • Vipodozi na mawigi
  • Vifaa vya stationary aina zote.
  • Vifaa vya ushonaji aina zote kama cherehani,vitambaa,vitenge,sindano,nyuzi nk
  • Material ya furniture aina zote.
  • Vijora
  • Mitumba aina zote
  • CD na Movies kwa wale ote wenye library
  • Hardware na Vifaa aina zote vya ujenzi.
  • Spea za pikipiki na bajaji
  • Baiskeli aina zote
  • Betri na matairi aina zote
- Mashine za bekari
  • Vifaa na material ya keki aina zote.
  • Mapazia na mashuka aina zote.
  • Mabegi,pochi na mikoba aina zote
  • Viatu aina zote
  • Na bidhaa zinginezo ambazo sijataja hapa.

MAWASILIANO: 0745645035 (PIGA/SMS/WHATSAPP) AU PIGA *149*46*30# KWENDA VODACOM,TIGO NA AIRTEL BURE

Karibu sana kwa huduma bora na za uhakika kila siku masaa 24.

Uaminifu ni mtaji,okoa muda na gharama za nauli kwa kuniagiza mimi bidhaa aina zote kutoka kariakoo kwenda mitaa yote ndani ya dar es salaam na mikoa yote tanzania kila siku.
binafsi huwa natembea na nguvu za Mungu, kiufupi uchawi kwangu huwa haufanyi kazi. nilishawahi kufukuzwa kwenye duka moja nilipotaka kununua kitu, akaniambia sitaki wewe ununue, ondoka tafadhali. sababu nilikuja kugundua kuwa mashetani yake yalipata shida mimi nilipofika pale.
 
Daah so powa kwa kweli.
 
Aloooooooooo.
watu mnajiona wajanja sana sikuhizi ila wahenga wanasema funika kombe mwanaharamu apite.
 
Mkuu wew ni dalali nin mkuu

Uwezi ukajuwa vitu vyote hapo fanya vichsche zaid kama unataka kila siku uondoke na 60000 yako
Sio dalali mimi mkuu wala sipigi ganji,mimi kazi yangu kununua bidhaa,kuifunga bidhaa na kuisafirisha bidhaa then nalipwa service fee yangu.Hivyo siwezi kuchagua cha kusafirisha mkuu.

Karibu.
 
Back
Top Bottom