Mwalimu wa tuisheni
JF-Expert Member
- Oct 19, 2019
- 6,602
- 10,801
Kilo moja ya mdalasini wa india bei gani...?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bei zinapanda na kushuka.jamani wewe mbona uwatu ni shs.6000 per kg nilichukua hapo kariakoo sokoni duka la jumla la muhindi
Karibu,njoo na chapati.Chai
Sio Kila changamoto unailet humu utageuka kuwa mmbeya.Una maanisha nini mkuu,nipe madini?
pole sana mkuuHapana mkuu ni tukio la kweli
🤣🤣Sawa sawaSio Kila changamoto unailet humu utageuka kuwa mmbeya.
Kuwachukulia una maanisha nini?eti 'Wakati napita na mzigo mbele yake nilimuona anashusha miwani akanitazama akavaa tena miwani nadhani amejifunza kitu leo maana kamzigo nilikonunua sio haba kwa ile jioni.'
unachukulia vipi watu humu ndani
Wajinga sanaHuu Ujumbe uwafikie vidada vinavyojudge watu kwa muoneokano maofisini,boss wake akikushobokea au ukitoa check pesa mingi ndipo uanza kushoboka
Ni kweli.Kariakoo Kila mtu Yuko suspicious dhidi ya utapeli, ushirikina n.k
HAhahahaHellow members,leo jioni angu haijawa powa sana baada ya kufukuzwa na mwanamama mmoja mmiliki wa duka la viungo pale kariakoo akidai kuwa mimi namchunguza.
Ilikuwa hivi mida ya saa saba mchana leo kuna mteja wangu mmoja hivi kutoka mkoa x kanipigia kuwa anataka viungo vifuatavyo kwa bei ya jumla (zabibu kavu,mdarasini wa india,corriander seeds, fennel, uwatu, kungumanga na star anise),Sasa toka nianze kuagiza mizigo kutoka kariakoo kwenda mkoani sikuwahi agizwa bidhaa za namna hii hivo ikanilazimu kuingia chimbo kutafuta.
Baada ya kuzunguka sana kule sokoni kariakoo nikawa napishana na wale wauzaji wa reja reja wa kwenye vimeza kila nikiwauliza wapi wanachukua mzigo wakawa wanakaza hadi mzee mmoja wa makamo alipoamua kunielekeza duka la bei ya jumla.
Baada ya kuelekezwa duka husika nikafanikiwa kufika na kweli kwa muonekano wa pale nje nikajihakikishia hapa wanauza kwa bei ya jumla kwani nilikuta kuna bidhaa zipo kwenye maroba makubwa pia kuna mizani na mifuko mikubwa mikubwa tu sio kama kule nje.
Basi nikaanza na duka la kwanza nilimkuta mama hivi kakaa nje,nikamsalimu baada ya salamu nikamuuliza kama naweza kupata hizi bidhaa huku nikumuonyesha majina ya hizo bidhaa kutoka kwenye simu.
Yule mama akajibu ingia ndani kwa hao vijana mimi sioni bhana, nikaingia ndani nikakuta washikaji wawili wanachezea simu nikawauliza vipi hizi bidhaa kwa bei ya jumla unauzaje. Mshikaji mmoja akaanza kunitajia,alinitajia zabibu kavu,mdarasini na kungumanga gafla yule mama akamkatisha wewe mteja unanunua au unauliza bei au umekuja kunichunguza.
Mimi nikamjibu hapana nauliza bei namtumia boss wangu apa ananitumia hela sasa hivi natoa hapo nachukua mzigo mama.Yule mama akaanza kuwaka toka dukani kwangu na wewe x( yule kijana wa dukani) fanya mambo mengine achana na huyo mteja.
Yule jamaa akajaribu kunitetea wapi yule mama akakaza nitoke kwamba mimi namchunguza ila sio mnunuzi.
Basi na mimi nikaona isiwe kesi nikasogea duka la mbele ake ambapo nilikuta wateja wawili wanahudumiwa,baada ya wale wateja wawili nikamueleza shida yangu yule muuzaji.Akanisikiliza na akanipa ushirikiano mzuri sana,na mimi bila kuchelewa nikampa feedback boss akatuma kibunda nikatoa chapu nikachukua mzigo.
Yule muuza duka niliponunua mzigo alinisaidia na box kabisa la kuwekea nikaufunga vizuri pale coz ulikuwa mkubwa nikatoka kuwaita washikaji wale wa vitolori wakabeba uku tukipita nao mbele wa yule mama mwenye gubu.
Wakati napita na mzigo mbele yake nilimuona anashusha miwani akanitazama akavaa tena miwani nadhani amejifunza kitu leo maana kamzigo nilikonunua sio haba kwa ile jioni.