Leo nimefukuzwa duka moja Kariakoo na mwenye duka mwenyewe kasema mimi namchunguza

Uaminifu ndo msingi wa biashara mkuu.

Karibu sana.
Bado hujajenga mazingira ya kuaminiwa.
Fungua ofisi isajili, utspiga kazi hadi ukimbie..
Unamfaha backtown?
Alikuwa hapo kariakoo mtaa wa swahili sasa amehamia pembeni ya hodpital ya Amana.
Alianza hivi hivi kutuma mizigo mkoani, sasa anamiliki mafuso na maskania ya kumwaga.

Ninatafuta tshet plain kwa bei ya jumla
1. Zenye kola
2. Zisizo na kola

Pc sio chini ya 100
 
Nimekuelewa mkuu,naenda taratibu nishasajili jina la biashara.

Haina shida mkuu nakutafutia hizo tisheti,naomba namba yako PM au nicheki wasup kwa kutuma neno tisheti plain the mm kesho nitakutumia picha na bei.
 
Nimekuelewa mkuu,naenda taratibu nishasajili jina la biashara.

Haina shida mkuu nakutafutia hizo tisheti,naomba namba yako PM au nicheki wasup kwa kutuma neno tisheti plain the mm kesho nitakutumia picha na bei.
Ukinipatia bei nzuri nitakupa kazi 5 zaidi hapo hapo na nitakulipo poa.

Nina dogo hapo lkn alinipa bei sikuiamini.
 
Unaingia kariakoo kuulizia bei aise, hata mimi ningekutimua.

Utakuwa umekutana na yule.manka wa majaliwa
 
jamani wewe mbona uwatu ni shs.6000 per kg nilichukua hapo kariakoo sokoni duka la jumla la muhindi
 
Ndo mambo ya kariakoo ayo inataka uzunguke kweli kabla hujanunua kitu
sure wale wanauza kwenye meza walitaka wanipige nashukuru Mungu akaniongoza kwenye lile duka bila kuuliza mtu kwasababu lipo mtaa ambao huwa nanunua vifungashio mara nyingi nilikuwa naliona lakini sikuwahi kuhangaika nalo, siku hizi ndo chimbo langu la viungo paprika robo kilo ni 2000/ , hivyo viungo vya vipalau vya 1000/ ni sawa na makopo matatu ya viungo vya dukani.
 
Chai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…