Kaanza kwa kumsafisha Maharagwe
" wewe huna tatizo , source ni sisi wote" swali kwanini umewatoa? Kama wao sio chanzo. Je wamekuwa kafara ya kujisafisha kisiasa? Ili kuleta attention kwa watu kuwa wamewajibishwa. Na mkuu anaupiga mwingi.
Sasa sikia chanzo cha tatizo na suluhisho.
Tatizo.
1. Mashine zilikuwa hazikarabatiwi kwahiyo tunazima na kuzikarabati. Shiiiiti. Sababu hii ilitolewa na yule PCM wa secondary ya Tanga. Eti kipindi kile mashine zilikuwa zilazimishwa tu kutumika bila service.
2. Maji yamekauka na kupungua kina.
Sasa ukisikiliza sababu hizi na kusoma sura ya muongeaji unaona Tz bila serious action tuko kwenye mbio za kijiti ambapo mwenzetu ameanguka na tunasubiri ushindi kupitia mbio zake.
Miezi sita ya nini kama maji hayapo? Ubabaishaji kabisa na anayeambiwa ana salute. Miezi sita ya nini kama mashine zinazimwa makusudi zifanyiwe service. Huwa naishia kulaumu vyombo vya usalama haviko kwa viapo vyake na hukumu ya Mkuu wa Malimwengu haitawaacha salama bora ukatae kazi kuliko kudanganya umma. Jamani hata intel ya Jeshi haichukui hatua? Hata ya fedha? Neno linasema
"Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini, Yeye naye atalia, lakini hatasikiwa."
Mithali 21:13
Kwahiyo miezi 6 ni kwa tegemeo la maji kiwa ya mejaaa au service kuwa imekamilika? Itokee service tayari mvua haijanyesha atatekelezaje?
Why Rwanda wanaenda mbele?