Leo nimejuta kupanda daladala

Leo nimejuta kupanda daladala

Nimesikitika sanani Bora ungepitiliza kituo tukuchangie nauli ya kurudi
 
shida ilikua nini hasa mkuu naona maelezo ni mengi
Haya,mtu ameshaelezwa stori,anauliza shida ilikuwa nini.
Svetavastara Upanishad.
Nilikuwa naisoma hiyo Upanishad na pale towards towards the end,in fact,the very last statement of the Upanishad is:
VI-23: These truths, when taught, shine forth only in that high-souled one who has supreme devotion to God, and an equal degree of devotion to the spiritual teacher. They shine forth in that high-souled one only.
Yaani,mpende Mungu,na pia mpende Spiritual Teacher wako vile vile unavyompenda Mungu.
Waislamu na watu wengi wengine watasema hii ni shirk.
Lakini hawa watu wanaposema love for God and love for the guru,sometimes they mean the sahasrara chakra in the center of the cerebrum and the guru chakra which is below the sahasrara chakra.
 
Nasra yupo kwa bodaboda analala uchi anapika na kupakua na kuangalia season azamtv.
 
Katikati ya safari si akapanda jamaa mmoja akawa anaongea kwenye simu na mwenzake. Namnukuu ( nukuu yangu ni baada ya jamaa kuongea kwenye simu kuhusu mada hiyo kwa kama dakika 20 hivi)

" Basi bana yule binti wangu wa kufikia Naa ambae yupo form four mwaka huu akawa amepotea nyumbani.

Siku hiyo ilikuwa jumamosi mtoto kaenda sokoni hakurudi.

Usiku hatukulala. Tukaanza kuhangaika polisi na hospitali kote huko hatukufanikiwa.

Siku 4 zote bila bila.

Baadae mke wangu akashawishiwa na rafiki zake waende kwa mganga.

Mganga akawaambia Naa ametekwa na wachawi na hao wachawi wana taka kumtoa sadaka kwa jitu kubwa ( limsukule) limnyonye damu .

Lilikuwa linasubiri siku ya saba ifike tu limnyonye damu na hiyo ilikuwa siku ya 5 so 2 days are loading. Mke wangu kusikia hivyo kazimia. Alipo zinduka wakanipigia simu kuniambia hiyo taarifa. Mke wangu kapanic vibaya sana.

Na Mimi kama unavyo nijua ndugu yangu mambo ya kipuuzi puuzi ( uchawi) huwaga siamini kabisa. So nikamwambia mke wangu hebu Achana na hayo mambo Naa atarudi tu kama ni kumtafuta tutumie njia nyingine sio hizo.

Mke wangu akaniambia " ooh au kwa sababu sio Mtoto wako?"

Siku hiyo sikulala kwa amani nyumbani mke wangu anakesha analia kesho yake asubuhi hakula siku nzima anasema twende tukamsikilize mganga Anacho kitaka. Mimi msimamo wangu ukawa pale pale. Mara ikafika siku ya saba ambayo ndio mganga alisema Naa ananyonywa damu na hilo lijitu.. kweli bana siku hiyo mida kama ya saa 7 mchana tukapigiwa simu na mama mkwe wangu analia anamtaja Naa. Mke wangu kusikia mama ake analia huku anamtaja Naa na yeye akazimia ... Nilipomuuliza mama mkwe kuna nini, akaniambia.....

STORY IKAKATISHWA,MPIGA STORY AKASEMA " KONDA ZUIA HAPA NIMEFIKA"

Abiria wote tulibaki na huzuni hatujui story imeishia wapi...

Ulivyo sikitika wewe kutoa jua muendelezo wa hiyo story ndio na Mimi nilivyo sikitika hivyo hivyo. Nimeileta hii story hapa ili tusikitike wote.

Nyie mnaopiga story za hivi muwege mnazimalizia basi wajameni
Kwanini ukushuka nae?
 
Back
Top Bottom