Leo nimekula hasara tatu; Chelsea imefungwa, likaka-poa limenifanyia fujo na nimepunjwa chenji Tabata Mangengeni

kilambimkwidu

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2017
Posts
6,097
Reaction score
7,199
Leo game ya Chelsea na Barcelona nilienda kuchek mitaa yaTabata Magengeni nikiwa na washakaji zangu na mahasimu mashabiki wa Man United, waliniita tujumuike kwenye Bar flan maarufu maeneo hayo. Na matokeo ni kama mnavojua....Chelsea tumekula tatu bila majibu pale New Camp japo refa alitunyima penati ya wazi kabisa. Kilio cha kwanza hiki!

Cha pili: kuna jamaa flan alikua kavaa jezi ya Man U alikua hatulii anatokatoka nje kumbe ni mtu maarufu pale anafahamika kwamba ni kaka-poa. Sasa alikua kila mara anapita mgongoni kwangu kwa kunipiga kikumbo kama anaenda toilet. Kama mara mbili hivi, mara ya tatu si nikamkoromea asipite kibabe, daah jamaa kaniwakia sana kaleta kelele pale hadi mabaunsa wakanitoa nje eti nasababisha fujo. Washkaji wakauchuna kama hawana habari na mimi eti wanachek game Barca anavoiburuza timu yangu, wananicheka mie nimebebwa natolewa nje. Dakika 20 za mwisho nimezuiwa kuingia, nimekaa nje nawasubiri washkaji ndani naskia makelele ya washangiliaji tu nje hapakuwa na screen.

Mwishowe jamaa wametoka wananiletea jero badala ya 5500 wamepewa chenji yangu niliiacha kwa mhudumu. Asalaaleh, niliacha nimempa elfu 10 nikachukua bia ya 2500 na maji makubwa ya 2000 ye amesema nilimpa elfu 5. Nimeomba kuonana nae nimueleweshe dada amekuja amekataaa katakata halafu anajilalamisha kwa sauti "huyu mteja mbabaifu sana nilimuona tangu mwanzo".

Sina hamu!!
 
Usiende tena Tabata, mimi Huko siendagi kabisa, baa zao zina wapiga mizinga wa kutosha. The Great ukizubaa bia yako imeibwa, ukinunua msosi jamaa wanakuja kukuomba wapige mtungo, ukiwakaribisha wanakupiga mizinga ya bia
 
Usiende tena Tabata, mimi Huko siendagi kabisa, baa zao zina wapiga mizinga wa kutosha. The Great ukizubaa bia yako imeibwa, ukinunua msosi jamaa wanakuja kukuomba wapige mtungo, ukiwakaribisha wanakupiga mizinga ya bia
Tabata yan kumbe kila mtu mhuni, nimepachukia sana.
 
usiku wa mabingwa mkuu[emoji23]
 
Messi kakutenda na shoga linakutenda tena..
Ungelisubilia njiani ukalizaba hata makofi mawili matatu.
Maana messi yeye huwezi kumfwata ulaya
 
Mimi yalinikuta mechi ya arsenal Na man city tumepigwa misumari mitatu afu nikapunjwa chenji na baa medi wacha ni mvae huko huko ndani kaunta changanya kufungwa na konyagi kichwani
 
Huyo alikupunja chenchi yako kwa makusudi kwa sababu alijua kuwa hakuna m2 anayeweza kukutetea,kuna jamaa alishawahi kutaka kunifanyanyia kitu kama hicho maeneo ya Buguruni sheli,namshukur Mungu nilicheza na akili za watu wakanisaidia!
 
Duuu jamana mm ni mwana mpotev naomben ushilikian wenu wa jamii forum
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…