kilambimkwidu
JF-Expert Member
- Jul 21, 2017
- 6,097
- 7,199
Leo game ya Chelsea na Barcelona nilienda kuchek mitaa yaTabata Magengeni nikiwa na washakaji zangu na mahasimu mashabiki wa Man United, waliniita tujumuike kwenye Bar flan maarufu maeneo hayo. Na matokeo ni kama mnavojua....Chelsea tumekula tatu bila majibu pale New Camp japo refa alitunyima penati ya wazi kabisa. Kilio cha kwanza hiki!
Cha pili: kuna jamaa flan alikua kavaa jezi ya Man U alikua hatulii anatokatoka nje kumbe ni mtu maarufu pale anafahamika kwamba ni kaka-poa. Sasa alikua kila mara anapita mgongoni kwangu kwa kunipiga kikumbo kama anaenda toilet. Kama mara mbili hivi, mara ya tatu si nikamkoromea asipite kibabe, daah jamaa kaniwakia sana kaleta kelele pale hadi mabaunsa wakanitoa nje eti nasababisha fujo. Washkaji wakauchuna kama hawana habari na mimi eti wanachek game Barca anavoiburuza timu yangu, wananicheka mie nimebebwa natolewa nje. Dakika 20 za mwisho nimezuiwa kuingia, nimekaa nje nawasubiri washkaji ndani naskia makelele ya washangiliaji tu nje hapakuwa na screen.
Mwishowe jamaa wametoka wananiletea jero badala ya 5500 wamepewa chenji yangu niliiacha kwa mhudumu. Asalaaleh, niliacha nimempa elfu 10 nikachukua bia ya 2500 na maji makubwa ya 2000 ye amesema nilimpa elfu 5. Nimeomba kuonana nae nimueleweshe dada amekuja amekataaa katakata halafu anajilalamisha kwa sauti "huyu mteja mbabaifu sana nilimuona tangu mwanzo".
Sina hamu!!