Leo nimekumbuka hiki kitu nilipokuwa uwanja wa vita

Leo nimekumbuka hiki kitu nilipokuwa uwanja wa vita

STUNTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
13,076
Reaction score
17,247
Katika uwanja wa vita, askari STUNTER nilijiandaa vyema
kwenda kumrudisha rafiki yangu aliyekuwa kaumizwa
vibaya sana kwa risasi na aliyekuwa kaanguka
umbali kidogo kutoka tulipo.
Captian akaniambia,“ STUNTER Huna hata haja ya
kwenda kumchukua kwani lazima afe tu hata kabla ya matibabu kwani kaumia vibaya” Lakini mimi
niliendelea kwenda kumfuata rafiki yangu na Captain
alipofika karibu yangu akaona yule askari
akiwa keshakufa. Captain akaniambia
“Nilikuambia lazima atakufa tu” ndipo nilipomjibu
Captain kwa macho ya ushujaa: “Hapana Mkuu, Limekuwa jambo la faraja kwangu….....Kwani nilipo
mkaribia, rafiki aliponiona akatabasamu na kusema
maneno yake ya mwisho kabla ya kukata roho:
“Nilijua tu lazima unifuate, Asante rafiki yangu wa
kweli na kwaheri……"
Funzo
Ukipata rafiki anayekujali, kukupenda, kukuthamini,
na kukuheshimu kamwe usimwache aende zake
kwani maumivu yake huwa hayaponi kamwe. Ni
ushujaa kuwa na wale tunaowajali na
kuwapigania mpaka tone la mwisho...
R.I.P
Fella...
 
Ujumbe mzuri...kwani nembo kubwa ya amani ni urafiki. Rafiki yako wa kweli huweza kubadilisha misimamo yako chanya/hasi na kukufanya uwe adui/rafiki wa wote.
 
Hahahaaa ila mkuu mi ninavyojua kwenye uwanja wa mapambano kama rafiki yako au mwenzako amejruhiwa na ukaona anatesaka!!wewe mwenzake unaruhusiwa kummalizia!!!
 
ahaha et post ya maana
 
Yeah ni kweli kabisa na vilevile utashangaa unaemwamini ndo anakuekea sumu hawana alama binadamu anaekuja kukuhukumu
 
Ile operation ya Makonda ya kutimua vijana wote wanaoishi dar bila kazi maalumu haijaanza?
Maana huyu jamaa hamalizi siku bila kuweka Uzi humu, ata Kama unasubiri ajira rudi kijijini ukasubirie huko, huku ukifanya Shughuli zingine za kilimo cha mboga mboga.
 
Ujumbe mzuri...kwani nembo kubwa ya amani ni urafiki. Rafiki yako wa kweli huweza kubadilisha misimamo yako chanya/hasi na kukufanya uwe adui/rafiki wa wote.
URafiki ndio kilakitu... Live long
 
Hahahaaa ila mkuu mi ninavyojua kwenye uwanja wa mapambano kama rafiki yako au mwenzako amejruhiwa na ukaona anatesaka!!wewe mwenzake unaruhusiwa kummalizia!!!
Captein wetu alishaona kwamba si wakupona, ndomana alimuacha tu...
 
Ile operation ya Makonda ya kutimua vijana wote wanaoishi dar bila kazi maalumu haijaanza?
Maana huyu jamaa hamalizi siku bila kuweka Uzi humu, ata Kama unasubiri ajira rudi kijijini ukasubirie huko, huku ukifanya Shughuli zingine za kilimo cha mboga mboga.
Dar ndo wapi?
 
Dah mzee wa ATC hii post imekaaje leo, machine ina bugs.
Nimemkumbuka rafiki angu, 2015 June aliaga dunia, alikua askari mzuri wa taifa hili na alikufa kishujaa akiwa na jezi za kutulinda. Mungu aziangazie roho za vipenzi wetu walotangulia
 
Back
Top Bottom