Leo nimekumbuka namna mpenzi/ mama wa watoto wangu alipoanza kunishinda kipato baada ya kupata kazi kila kitu kikaparaganyika

Leo nimekumbuka namna mpenzi/ mama wa watoto wangu alipoanza kunishinda kipato baada ya kupata kazi kila kitu kikaparaganyika

unafkiri nmesahau ile sku ya kwanz ulinivamia kibabe 🤣😆 nilkua nmecoment uzi fulani ivi
Hahaha, enzi hizo sijakuzoea. Ila hata kama ni kutofautiana basi nadhani ni sababu ya mawazo tofauti tu ila sio sababu wanawake wananiumiza. I am happiest man ikifika kwenye maswala hayo, sina mwanamke anayenishupaza mishipa ya shingo in real life. Haha
 
Hahaha, enzi hizo sijakuzoea. Ila hata kama ni kutofautiana basi nadhani ni sababu ya mawazo tofauti tu ila sio sababu wanawake wananiumiza. I am happiest man ikifika kwenye maswala hayo, sina mwanamke anayenishupaza mishipa ya shingo in real life. Haha
aloooh ulinivamia bila hata kukukosea maskin,, nashukuru kwasasa nmejifinza jinsi ya ku lower temper
 
miaka 5 nyuma nilipatwa na hiki kisa, sijui huwa kuna nini kinatokea kwa wenzetu naweza kusema alikuwa mke kabisa maana kwao walinifahamu posa na mahari nilishamaliza na watoto wawili nimemzalisha sasa kipindi chote hicho alikuwa anafanya shughuli ndogondogo tu..

sasa ikatokea fursa sehemu nikamwambia mama kwa haya maisha tunayoishi itachukua muda kutoboa hapa ebu kamatia iyo fursa ya kazi tusaidizane bwana bwana bwana kumbe ndio nilikuwa namaliza familia yangu wakuu kitendo cha yeye kupata ile kazi tu na vile nilimtumia mtu ninayemjua ilikuwa rahisi sana kwake kutoboa..

picha linaanza kwanza amepangiwa mkoani akili ikacheza mmh nikiwa nipo kwenye dilema ya maamuzi kwao wakawa wapo karibu nae zaidi na wakamwambia aende huko kwa kuwa watoto bado wadogo waende kwa bibi yao yaani mama yake hadi mambo yatakapokuwa sawa kule then awachukue.

basi mwezi ukaisha mwezi wa pili mara miezi sita nikaanza kuona mapicha picha kwanza sikuwahi kuona hela yake ingawa alikuwa analipwa mara 4 ya mshahara wangu bado nilitakiwa kutuma pesa ya matumizi kwangu hakuwa shida maana naelewa mwanaume ndio mtunza familia kifedha..

alifanikiwa kurudi kipindi cha mwanzo mwanzo tu tena akaniletea nyodo hatari stori zake sasa ooh mwaka huu nanunua gari sijui wewe umeshindwa hiki na kile nikitaka tunda anajivutaa nikajisemea hii ngoma ndio imeshavuja hapa...kwakweli haikufika hata mwaka tukabwagana.

hakuna kipindi nilikonda kama kipindi kile full mawazo alafu ndugu zake wananichora tu kenge wale!
ilibaki kidogo nidondoke nifeee!

kuna mama mmoja mtu wa makamo akanifuata na kuniweka chini kisha akanipa ushauri mmoja wa nguvu sana akaniambia kijana wangu usiwe mnyonge hivyo tafuta mwanamke mdogo na mzuri kuliko mkeo then furahia maisha haya maisha ni mafupi sana na utamsahau.

kwa kweli namshukuru sana yule mama maana from there maisha yalibadilika taratibu nilianza kumsahau yule mwanamke na mambo yake ingawa bado muda mwingine naumia ila ndio maisha isee
tuishi nao kwa akili!
Haha basicaly hutoweza kumsahau kabisa because mna watoto lakin pia ni mtu amba moishare nae maisha, it good that umejifunza kuishi nalo. Keep moving
 
Back
Top Bottom