Leo nimekumbuka namna mpenzi/ mama wa watoto wangu alipoanza kunishinda kipato baada ya kupata kazi kila kitu kikaparaganyika

Pole sana. Ni kweli haya mambo yapo sana. Asije mwanaume kusema hawezi umizwa na mapenzi. Huyo wakati ukifika anakufa kabisa
 
Bahati mbaya sana ni kuwa wale wote wanaofurahia ndoa zao kwa amani huwa wapo kimya na kamwe hutowasikia.. Ila ndugu zangu waliitendwa utawasikia Kila sehemu wakilalamika..

Sitaki kuamini kuwa kila mahusiano ni mabaya.. Vijana oeni na mabinti oleweni.. Jipe muda, hakikisha huyo unayeingia naye kwenye ndoa ni mtu sahihi.. Mtangulize Mungu naye atakuongoza..

NB; NDOA NI JELA.. NDOA NI KIFUNGO.. CHAGUA VYEMA UTAKAYEISHI NAYE NDANI YA KIFUNGO/JELA HIYO..
 
Naomba kutoa ushuhuda tofauti na huu. Siyo sahihi kusema wanawake wote ni vigeugeu.

Kuna kijana mmoja wakati yupo msingi, mwalimu alikuwa anamchapa mwanafunzi mwingine, kipande cha kiboko kikamchoma jicho moja.

Alipowekewa dawa ya macho AKAPOFUKA.

Wazazi wake walihangaika ajabu lakini mpaka kesho ni kipofu.

Kijana ni mwenyeji wa wa Lindi, ilibidi wampeleke Mvumi akasoma huko katika shule ya vipofu. Akasoma msingi na sekondari akafaulu kwenda kusoma Chuo Kikuu UDOM.

Akiwa mwanafunzi UDOM akapata rafiki wa kike ambaye baadaye akawa mchumba miaka mitano iliyopita.

Jumapili ijayo wataposana (engagement) kanisani kwao. Kanisa lipo karibu na Sinza Makaburini.

Binti hakubweteka bali alipambana na shule pia na kwa sasa ana Masters.

Wanadamu hatupo sawa kuna wengine wapo ni tofauti. Mifano ni mingi sana ya wenye upendo wa kweli. Wakati mwingine wanawake wanakuwa na upendo wa kweli ila sisi midume tukianza kuchepuka ovyo tunawakatisha tamaa. Kumbuka nao ni binadamu wana mioyo yenye nyama. Sikatai kuna wanawake nao ni vichomi bali na kuna wengine ni Gifts from God.

Tulale sasa
 
Experience yangu hata umfanyie wema gani atakuacha tu..
Arusha 2014 jirani yangu alikuwa anafanya kazi taasisi fulani, financially alikuwa yuko poa sana. Kulikuwa kuna binti alikuwa anakuja kwake mostly on weekends... Siku ndo akani tambulisha hii ni pisi yake ila inasoma mkoa x chuo kikuu mwaka wa pili... Miaka ikaenda ile pisi ikawa haionekani kumbe ilikuwa chuo.
Mambo yakaenda vibaya kwa yule dada alifeli chuo so hakuweza kumaliza chuo. familia ikamtema mazima kwamba atajua na maisha yake. Familia ilienda mbali na kumuambia pesa walizo nazo niza kusomesha wadogo wa yule binti. So binti akamshirikisha boyfriend wake ambaye ni jirani yangu. Jamaa akamuambia aje tu maana hata kwenda nyumbani aliogopa.
Basi jamaa kwa kujua one day in this life atakuwa mke wake, akalibeba lile jambo na kuamua kumpeleka chuo kikuu kimoja kiko Arusha, alim somesha, chakula, mavazi yaani kwa kifupi alikuwa mzazi na boyfriend at once. akawa anaenda chuo for all the three years tumekaa nae pale, ila this time alitoboa graduation kila kitu fresh. Walikuwa poa sana kiukweli, ilikuwa ni couple moja strong sana ile unajua demu aki graduate wanafunga ndoa.
Demu aliendelea kukaa pale hadi akapata nafasi katika kampuni flani hivi alianza kwa kujitolea baadae akapata ajira ya kudumu, ila kupatikana hii kazi ni kwa juhudi za huyu mwamba. sijui salary yake but alikuwa ana safiri sana. Matatizo ndo yakaanza kule ndani. Demu alikuja kubadilika ndugu zangu siyo poa, kama mara tatu wameshikiana visu mule ndani, alikuja kumuacha mwamba kama hamjui and familia ikamuambia arudi nyumbani huyo jamaa siyo mume wake.
Jamaa alifanya attempt kama mbili za kutaka kujiua, alikuja kuwa mtu wa pombe sana, sigara nyingi sana (wakati hakuwa mnywaji kivile, wala mvutaji wa sigara) alikuja kukonda, kwenda job late, ananukia na pombe, kwa kifupi aliyumba sana ile kampuni ilijaribu kumbeba sana because bosi pia alijua what he was going through. Alivyoachishwa kazi akaja kuniaga akarudi kwao. That brother he was torn apart because of love. he couldn't take it anymore... Dada yake alikuja kunipigia March 2023 the brother died. Yule dada yupo tu huwa namuona mjini na life lake tu.
Kwa kifupi after that scenario nimeona unaweza ukaigiziwa maisha vizuri tu, riziki ikapatikana zaidi kwa mke au mpenzi wako hamuwezi toboa tena...! Dharau zitaanza tu kama hiyo pisi ilishamrudia jamaa na lovebite. . . !
 
d
kwa haya, sitakuja oa ,wala kusomesha mwanamke, nisipopata pisi kwenye huu uchakavu wangu, i swear ndoa hainihusu.
 
Mwenyezi Mungu amjalie kupumzika kwa amani, imeniuma mno .
 
Kuna mshikaji wangu maarufu sana wa mambo ya real estate kwanza mshikaji mjanja wa mjin pesa ipo ana vaa vizur ana gar kali nyumba kali dah juz nimeshangaa analia mtandaoni dem kasepa na watoto kosa alilofanya alimfungulia mkewe saloon na duka la urembo aisee Demu kaona ahame na nyumba kabisa

Sijui uwa wanataka nini hawa dada zetu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…