Mkuu kuna kitu ambacho hujakijua kuhusu purchasing power ya USD ukiwa US usiilinganishe moja kwa moja na thamani ya hela ya nchi nyingine (hususan Tanzania). Kazi ya kibarua kwa saa Marekani ni hadi USD 30 kwa saa. Ikiwa na maana ni takribani Tsh. 75,000/= kwa saa. Ukifanya masaa 10 kwa siku ina maana umeingiza 750,000/= kwa siku. Sasa kama uelewi hali halisi ya maisha ya marekani ukaanza kulinganisha na bongo utadhani hiyo ni hela kubwa kumbe si chochote! Katika hiyo hela ukitoa kodi ya nyumba, usafiri, bills za maji, umeme, afya, simu, chakula, (au uamue useme ebu nikapate kinywaji sehemu nzuri, n.k) n.k. utajikuta huna kitu au kama huko smart unaweza kufanya savings lakini si kivile kukufanya utajirike! Kwahiyo, acha kabisa kulinganisha hali ya maisha ya USA na bongo!