Leo nimemkumbuka member wa JF Folk (RIP)

Nimerudia mara 4 kusoma haya maneno na kugundua ni maneno ya kijasiri sana, wengine wangeishia kulia tu kitandani huku tukisubiri kifo kitufikie, ni kweli jamaa alikuwa ni mtu jasiri na mwenye maono.

Wangapi kati yetu wanaweza kuyasema haya huku wakijua fika kwamba ndani ya miezi 4 au less watakuwa wameshafariki na kuzikwa,

Je ni wangapi kati yetu wanaweza kutembelea makaburini kucheki watakapoishi milele na kuishia kutabasamu? je ni nani kati yetu mwenye ubavu wa kukisemea kifo chake?

RIP chief.


-----------------------------​

"Ripoti ya daktari inasema baada ya miezi 4 nitakufa kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4.)

Kwa hiyo miezi minne ijayo nitaweza kuona kile marehemu wanachoona sijui kufa kunaumaje?

Juzi nimepita kando ya makaburi nikaishia kutabasamu tu nilipogundua next 4 month nitafukiwa chini alafu watu watawanyike waniache pale nikiwa shimoni mwenyewe, upweke utakuwa mkubwa mno.


Nikiwa kijana kindakindaki wa miaka 28 tu nafukiwa ardhini. Masikitiko.
 
Labda kwasababu nilikuwa programmed kuwaza hivyo kupitia mafundisho.
One time nilikuwa kama wewe. Nilifundishwa mengi kanisani na home. Then nadhani nikiwa chuo na baada ya chuo nikaokoka. Hii ilikuwa kama imefungua akili yangu nikagundua kwamba sina uhakika wa mambo mengi ikiwemo uhakika wa Biblia, uwepo wa Mungu.

Hapo nilianza safari iliyochukua miaka kadhaa kutafuta ukweli. Ilinipitisha kwenye ku study uhindu, ubuddha, uislam, ukristo, ukana Mungu. Nilisoma scientific arguments, philosophy, nikaangalia debates nikatafuta archeology... kufupisha stori niliishia pale wengi wa safari hii huishia.

kwamba Biblia iko accurate kwenye matters zote inazogusa, science, history, archeology na prophecy. Nikajua historically Yesu wa Nazareth alikuwa ni mtu aliyekuwepo kweli, aliyeishi maisha ambayo yalikuwa si ya kawaida. Na kuwa alihukumiwa zamani za Tiberius kama sikosei Pilato akiwa gavana na Herode akiwa mfalme wa kale kaeneo.

kwamba kuna ushahidi kuwa alikufa na kuzikwa. Kwamba kaburi lake halijawahi kuwa na mwili na kuwa kuwa wanafunzi wake walidai, kati kati ya Yerusalem alipofia kuwa amefufuka. Na kwa sababu njia rahisi ilikuwa ni kuileta maiti ya Yesu ili kuua uvumi wakuu wa dini walishindwa kwa kuwa hakuwemo kaburini.

kwa ushahidi wa kihistoria huyu Yesu alifufuka. Extraordinary event iliyo prove uungu wake. Lakini ukiacha haya yote, alibadilisha maisha yangu for good. To me that is a huge personal evidence.

kwa hiyo nakuhakikishia ukimtafuta Mungu kwa bidii hayupo mbali nawe. Nikikumbuka siku zile za mahangaiko ya kutojua nitaamkia wapi nikilala kwenye kifo, huwa natamani kuwaambia watu kile nimekipata:Yesu Kristo ambaye anakupa uzima wa milele. Njia halisi ya kwenda mbinguni.

Nina hakika nikifumba macho hapa duniani yuko ng'ambo ya pili kunilaki. Kwa hiyo kuishi ni Kristo na kufa ni faida!

Incarnation kwangu nawaza hivyo kutokana na story za watu niliosoma kuwa walizaliwa wakawa wanakumbuka mambo ya zamani kama vile waliwahi kuishi mfano yule kijana wa India na yule dada aliedai kuwa alikuwa mke wa Pharaoh na wengine.
Bahati mbaya hii dunia sio binadamu pekee tunaishi. Tuna mashetani yamekuwepo vizazi na vizazi na yana taarifa za ndugu na watu ambao hujawahi kuwajua. Yanaweza kutumia hizi taarifa ili kuwadanganya wanadamu ili kuwakosesha.

Kuwa makini sana, maana hata masangoma wana hizi taarifa na source ni the same
 
Mkuu, katika kusoma soma nilikuja soma kwenye vyanzo mbalimbali kuwa Jehanamu yani Hell limetokana na Jamaa anaitwa Dante wala halikuwa kwenye Biblia.

Ni kwamba kwenye toleo la mwanzo la Biblia ya Hebrew kwenye Agano la kale "Hell' ilikuwa ni "She'ol" ambapo ina maana ya "grave" yani kaburi "abyss" shimo refu. Katika kutafsiri ikatafsiri kama "Hades" kwa Kigiriki ambapo hilo neno Hades katika hadithi za Kiimani za Kigiriki limeambatana na mambo ya kuzimu na stori za kutisha.
 
Mimi nimesoma na imani ya Kiislamu na Kuswali pia, japo nimezaliwa katika imani ya Kikristo. Now napenda soma mambo ya Kihindu in my free time.
 
Namwamini Mungu moja,kanisa takatifu kufufuliwa kwa mwili na uzima wa ulimwengu ujao......

Je Mbinguni Ni wapi?Jehanamu Ni wapi?Ulimwengu ujao Ni upi?

Nina maswali mengi.

Fortunately,hakuna kisicho na mwisho!"Kila kitu kitapita,vizazi vitapita,dunia itapita,Mimi na wewe tutapita neno la Mungu litadumu milele.
 
Angalau hata umefanya uchunguzi kwa kina,Huko Mbinguni Ni wapi Kaka?na Jehanamu Ni wapi?Mimi nipo kwenye hiyo stage ya kutokuwa na uhakika wa uwepo wa baadhi ya vitu.....Naamini tu Mungu yupo,Ni roho,na tunaishi nae siku zote kwenye Maisha yetu,kwenye uwepo wetu...yaani yupo nae nyakati zote...na Iman yangu ya akili yangu isio ya mapokeo Naamini hakuna huo Moto tunaoaminishwa upo.
 
Sitamsahau Dena Hamsi...Apumzike kwa Amani...nilikaa nae JF zaidi ya 10 yrs
 
Hivi ndo alikua akijiita pia mpauko au ?maskin rip,tuache kubeza watu jaman, sometimes people go through a lot in silent
 
Tumeumbwa kwa udongo, na kwa udongo tutarudi...
 
Angalau hata umefanya uchunguzi kwa kina,
Wengi huamini wasicho na uhakika nacho labda kwa sababu alipozaliwa wanaamini hicho. Ni vizuri haya mambo tukatafiti ili tuwe na hakika na tunakoelekea.
Huko Mbinguni Ni wapi Kaka?
Mbinguni kwa sasa ni dimension tofauti na hii, mahali ambako Mungu aliyeko kila mahali ameamua kuweka kiti chake cha Enzi. Kibinadamu tungeita HeadQuarters ingawa bado haisemi kwa fulness yake. Angalau inaweza kutoa picha. Haipo kwenye dimension ya time-matter-space ambayo sisi tumefungwa nayo. Hata Yesu ilibidi afufuke kwenye mwili ambao una uwezo wa kuishi kwenye dimension ile. Ni topic ndefu kidogo, ila huwa napenda kuandika majibu kwa kirefu kwenye PDFs na kushare kwa emails.

Kama wewe au mwingine hapa angependa kupokea sehemu ya mafundisho na kuwa na access ya kuuliza na kujibiwa kwa kina nitumie email kwa address raccqa@gmail.com Itakuwa rahisi kufanya ile to and fro discussion. Nilikuwa na group la Telegram back then but kwa sasa haliko active. So tumia email kama ungependa kuwa na discussion na followups
na Jehanamu Ni wapi?
Jehanamu ni gereza ambalo Mungu alimwandalia shetani alipoasi. Ni sehemu yakutisha hakuna mfano wake. Yesu alitumia mifano kadhaa kuetupa picha, lakini kwa sababu hakuna mfano wake tena ni vigumu kuelewa asilimia mia. Watakaokwenda huko wataelewa 100%.

Ila tunajua kuwa ni sehemu ya moto wa sulphur (brimstone), kuna giza kuu, kuna funza ambao hawafi na watu wanateswa usiku na mchana. Ni mbali na wema wa Mungu na hakuna cha kufurahia. Yesu alishauri mkono ukitaka kukukosesha bora uukate maana ni bora uingie mbinguni na mkono mmoja au jicho moja kuliko kwenda na yote miwili Jehanamu. Alichomaanisha ni kuwa Jehanamu ni mahali pabaya hapafai.

Wanadamu tunaenda huko kwa sababu tulijiunganisha kwenye uasi wa shetani kuanzia kwa Adamu mpaka leo.

Mimi nipo kwenye hiyo stage ya kutokuwa na uhakika wa uwepo wa baadhi ya vitu.....
Kama utahitaji msaada wowote toka kwangu kwa maswali au ufafanuzi tuwasiliane kwa email hapo juu. Nitajisikia fahari kama nitakuwa wa msaada kwenye safari yako hii, kama ambavyo wengine walikuwa wa msaada kwenye safari yangu. Nakuhakikishia kuwa ukimtafuta Mungu kwa bidii atajifunua kwako. Nakuombea mafanikio!
Naamini tu Mungu yupo,Ni roho,na tunaishi nae siku zote kwenye Maisha yetu,kwenye uwepo wetu...yaani yupo nae nyakati zote...na Iman yangu ya akili yangu isio ya mapokeo Naamini hakuna huo Moto tunaoaminishwa upo.
Ni kweli Mungu yupo, na ni Roho, na yupo karibu nasi kuliko tunavyowaza. Shida mafundisho mengi duniani yanafundisha mambo ambayo hayana uhalisia na kuna wengine wamefikia mahali kuziweka akili mfukoni. Mtafute Mungu kwa moyo wako wote, kwa akili yako yote pia. Mtafute maadam anapatikana!
 
Nadhani maswali ni mengi na mengine kuandika hapa itachukua muda. Kama utakuwa willing tunaweza kuwasiliana kwa email raccqa@gmail.com ili kuweza kuwa na mtiririko wa maswali na majibu. Ni rahisi maana hapa kuna comments nyingi na zinatembea haswa.

Ila swali la mbing nimegusa hapo ju, pamoja na Jehanamu. Kuhusu ulimwengu ujao ni wakati ambao historia itafikia mwsho. Wakati kuna kipindi haukuwepo then ukawepo na kuna kipindi utafika mwisho. Na hapo ndipo Utakuja ulimwengu wa umilele. Ambao kila mtu kwa uamuzi wake ataishi huko pasi na mwisho. Ukisoma ufunuo sura ya 21 na 22 itakupa hint ya ulimwengu ujao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…