Leo nimenunua maembe 3 kwa Sh. 10,000/- bila kupenda

ommytk

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
520
Reaction score
1,143
Wadau leo nimezidiwa ujanja nimebaki nacheka kweli mjini shule nimemkuta mtu ana maembe dodo mazuri Mbagala stand nikayapenda, nikauliza bei akasema ni sh. 800 na yapo 4 Mimi nilitaka mawili tu.

Nikampa 10,000 akawa chenji hana ikabidi aniache na maembe yale manne na kiroba chake anaenda kuchukua chenji na kuleta mfuko aisee nimekaa Masaa nawili hajarudi. Nikawauliza majirani pale wanauza vitu wanasema hawamjui. Basi nimeondoka, kiroba nimetupa, nimechukua embe nipo home.

Pia soma: Uzi maalumu wa kupeana njia wanazotumia MATAPELI

 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Pole mkuu
 
Ni bora mwizi wa namna hii, kuliko yule anakuchukua, kisha anakuweka ndani, mwaka mzima, unateseka, huioni familia yako, unakula hovyo kisha unampa hela anayoitaka ndio anakuachia.

Mwizi wa hivi ni mbaya, sbb anakuibia huku anakupora haki zako za kijamii na kibinadamu, ila huyo mwizi wako yeye anakuibia lakini hakuchukulii haki zako, si unaona time hii uko kwako!
 
Unataka kusemaje kwa mfano?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…